Dkt. John Pima aliyekuwa DED Arusha na wenzake wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Dkt. John Pima aliyekuwa DED Arusha na wenzake wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Hao ndiyo "wasomi" wa Tanzania.

Walienda shule kusomea ujinga.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi...
Naunga mkono hoja,safi sana Serikali ya awamu ya 6 Kwa kupambana na Mafisadi Kwa vitendo.

Bado wale wa Mbeya,Katavi na Dar waliohujumu Mamilioni ya Wananchi.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi...
Gambo alikuwa akiongea mara nyingi watu wanamshambulia,haya Sasa Wameumbuka.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Agost 31, 2023 na Hakimu Seraphin Nsana, katika kesi namba 5/2023 ya uhujumu uchumi, iliyokuwa inawakabili Dk. Pima, aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5/2023, mbele ya mahakama hiyo, Hakima Nsana amesema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, mahakama imewatia hatiani washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili.

"Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini ukizingatiwa," amesema

Mbali na hilo, washtakiwa wana haki na nafasi ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu endapo hawajaridhika na hukumu hiyo.
 
Hawa jamaa walijenga soko Moja kioja sana pale mbauda kwa gharama ya 1.4B... yaani pale kama walitumia sana pesa ni 200M, siku ya kulizindua... PM majaliwa alifika akapigwa na butwaa, akageuza msafara akagoma kulifungua akasema ni uchafu ule, akaamuru wakamatwe... Ndo kilichowafunga hao.... Ila ile pesa walipiga wengi tu Hawa ni mbuzi wa kafara
😅😅😅Hiyo kesi watazungushana baada ya miaka 2 utakuja kusikia wameachiwa
 
Back
Top Bottom