Dkt. Kahyoza: Magufuli alifanya makosa makubwa kuhamishia Serikali Dodoma, gharama zimekuwa mara mbili

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mtaalamu wa masuala ya Uchumi, Dr. Bravious Kahyoza amesema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ulikuwa ni kosa kubwa kwasababu umeongeza gharama zaidi za uendeshaji ikiwemo kutumia vibaya fedha za Walipa Kodi.

Ametolea mfano Safari za Viongozi na Watumishi ambao mara kwa mara wanaenda Dar au Dodoma kwa Ndege na wakati huo Magari yanasafiri kuwafuata Airport na kuwapeleka kwenye shughuli zao na baadaye wanarejea kwa Ndege tena huku magari yakiwafuata kwa njia ya Barabara.

Pia Soma: Ilikuwa ni jambo jema Serikali kuhamia Dodoma maana Kivukoni na Posta ni Bandarini, Ashukuriwe Shujaa Magufuli!
 
Huyu bwana, nakumbana naye katika chambuzi/ tafakuriza za

Yuvan Noah harari (21 Lesson's for 21 century),na

Ha joon chang (bad Samaritan:the myth of free trade & secrets history of capitalism , Kicking away the ladder).

Mambo mengine namuachia,

HUyu Bado ni mwanachama wa CCM?
 
Mtaalamu wa masuala ya Uchumi, Dr. Bravious Kahyoza amesema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ulikuwa ni kosa kubwa kwasababu umeongeza gharama zaidi za uendeshaji ikiwemo kutumia vibaya fedha za Walipa Kodi...
Mbona hakuna sababu yoyote na hasara yoyote ya kiuchumi aliyoisema zaidi ni kama amesema viongozi wanaotumia mali za umma vibaya.

Labda tusikilize interview nzima tunaweza kuona hizo hoja za kiuchumi ila kwenye hii clip anaonekana ni mtu ambaye anatafuta fursa kama tulivyo wengine
 
Huyo ni chawa yupo kazini.

Viongozi wa Serikali walishahamia Dodoma baada ya Ikulu kukamilika, hakuna Ofisi za Serikali Dar.

Sasa huyu chawa kwa kutumia maneno hayo hayo ya kukemea kufuja rasilimali za nchi, kwanini asiyaelekeze kwa viongozi wa umma waliopo madarakani wanaofanya hizo safari zisizokuwa na tija, kuanzia Rais kutotulia Dodoma, ambako kuna ofisi zake na makao yake, kila siku kiguru na njia kwenda Dar?

Kuendelea kubeza mambo yaliyokwisha kutengenezwa na kukamilika ni upumbaf wa kihayawani.
 
Mbona hakuna sababu yoyote na hasara yoyote ya kiuchumi aliyoisema zaidi ni kama amesema viongozi wanaotumia mali za umma vibaya.

Labda tusikilize interview nzima tunaweza kuona hizo hoja za kiuchumi ila kwenye hii clip anaonekana ni mtu ambaye anatafuta fursa kama tulivyo wengine
Gharama zisizo za ulazima za kwenda Dar kwa ndege ,Halafu dereva anaenda kwa gari tupu hadi Dar!
 
Mtaalamu wa masuala ya Uchumi, Dr. Bravious Kahyoza amesema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ulikuwa ni kosa kubwa kwasababu umeongeza gharama zaidi za uendeshaji ikiwemo kutumia vibaya fedha za Walipa Kodi.

Ametolea mfano Safari za Viongozi na Watumishi ambao mara kwa mara wanaenda Dar au Dodoma kwa Ndege na wakati huo Magari yanasafiri kuwafuata Airport na kuwapeleka kwenye shughuli zao na baadaye wanarejea kwa Ndege tena huku magari yakiwafuata kwa njia ya Barabara.
View attachment 3017571
Pia Soma: Ilikuwa ni jambo jema Serikali kuhamia Dodoma maana Kivukoni na Posta ni Bandarini, Ashukuriwe Shujaa Magufuli!
Jamaa boya sana
 
Kosa alifanya Nyerere back in 1973...Aliamua kuhamia dodoma bila ya yeye mwenyewe kuhamia kule...kama angehamia kikweli kweli dodoma, 50 years now Govt capital ingekuwa dodoma na Dsm ikabaki kuwa port and business capital.

Unfortunately baada yake hakuna Raisi aliyependa kwenda Dodoma, somehow, somewhere alitakikana mtu wa kufanya maamuzi, twende dodoma au tubaki Dsm na hicho ndicho Jiwe alikifanya...CCM kwa kuwa ni genge la wanafiki wamekuwa wakikwepa mjadala huu. Ilitakiwa baada ya Julius Nyerere waamue ikiwa dhamira ya Dodoma ingalipo au imekufa na mwasisi wake in 1999.

Kumlaumu hayati mwendazake kwa kufanya maamuzi ambayo chama kimejinasibisha kwayo tangu 1973 siyo haki na hivyo huyo msomi hakutenda haki!
 
BARD AI nadhani Dr hayuko sahihi....anachotakiwa kufanya ni kuwashauri viongozi kutulia katika mji wa kiserikali Mtumba ili kupunguza matumizi ovyo ya Kodi za wananchi....
Hawawezi kutulia kinachotakiwa kushauriana namna ya kupunguza gharama usafiri
 
Back
Top Bottom