Ukiwa na fikra nzuri huwezi kuyasema ulio ya sema, huwezi kukaa kusubiri sababu kwenye kitu unachojua ni mpango wa lazima unao paswa kutekelezwa. Basi namimi nikuulize, kwanini ilibidi kusubiri sababu ili kuhanisha mako makuu Dodoma?
Kwa Maoni au maelezo yako haya ndio unajiona kwamba una fikra nzuri??? Seriously???
Remember, I'm not among of the short-sighted mind persons like you.
Je, sababu zipi hasa za mwanzo kabisa ambazo ziliifanya Serikali ya nchi hii ya Tanzania kufikiria kuhamishia Makao yake makuu mjini Dodoma badala ya Dsm????? Jibu kwanza swali hili.
Kwani bunge kua dodoma na office za mawaziri kua dar uliliona ilo ni sawa? Swala la kutokua na mji wa kiserikali unaliona ni sawa?
Ni sawa ndiyo, kwani kuna ubaya gani??? Kwanza kitendo Cha kutawanya miji ya Serikali katika maeneo tofauti tofauti ya nchi kuna faida nyingi zaidi kuliko hasara. Kiendo Cha kuiweka au kurundika miji hiyo (Ofisi hizo) sehemu moja tu Kuna hasara zaidi, faida mojawapo ya kutawanya miji ya Serikali ni kufanya miji husika kuwa na maendeleo makubwa hence kuwa na Uchumi mkubwa.
Nakupa mfano Mdogo mmoja tu:
Nchi ya Afrika ya Kusini kuna miji mitatu ya Serikali, Yaani makao makuu ya mihimili yote mitatu ya Dola (Ikulu, Bunge na Mahakama) imewekwa katika miji tofauti tofauti kabisa ambayo ipo katika Mikoa (Majimbo) tofauti, miji hiyo ya Serikali ipo umbali mrefu kutoka kwenye mji mmoja hadi mji mwingine.
Mathalani;
1. Ikulu ya Rais ipo katika Mji wa Pretoria.
2. Makao Makuu ya Mhimili wa Mahakama yapo katika mji wa Bloemfontein, takribani umbali wa kilomita 400 kutoka Pretoria.
3. Bunge lipo ktk mji wa Cape Town, takribani kilomita 900 kutoka Pretoria.
Miji yote hiyo Ina maendeleo makubwa kutokana na kuwepo kwa makao makuu ya mojawapo ya mihimili ya Dola.
Therefore, no research no right to speak.