Tetesi: Dkt. Kalemani kupewa mifugo huku Ndaki akipigwa chini

Tetesi: Dkt. Kalemani kupewa mifugo huku Ndaki akipigwa chini

Aamina [emoji2972]
Makamba akae nyumbani kama kina Lukuvi walahi!
 
Wakati wa Mwalimu, hususani miaka ya 1961-1969 Tanzania haikuwa na wasomi wengi.
Kwa hiyo Rais alipata shida kuteua Baraza la mawaziri, makatibu wakuu,wakuu wa mikoa na wilaya, Na RDD na ma DDD (Siku hizi wanaitwa Na RAS na DAS),wakuu wa Taasisi mbalimbali nk
Lakini miaka hii, Tanzania Ina wananchi wengi Wana elimu ya kutosha, lakini Mamlaka ya uteuzi,inashindwa kuteua watu sahihi wenye ubunifu wa kuisaidia Tanzania, kuleta Maendeleo endelevu.
Tunakwama wapi? Utakuta Mamlaka ya uteuzi inawaacha na kuwarejeshea walewale,kwa sababu ya technical know who badala ya technical know how.
Kwa utaratibu huu, Maendeleo yatakuwa ni ndoto,kwa sababu wateule wengi hawana mtizamo/mawazo mpya/ubunifu/mikakati ya kutatua masuala kulingana na hali halisi ya maisha au ulimwengu wa sasa.

Ushauri
-Serikali iwe inaandaa vijana wabunifu Ili waje kushika madaraka siku za usoni kwenye nafasi mbalimbali.
-sekta za taaluma za kisayansi na technolojia ni vema wakaandaliwa wanasayansi/technolojia kuja kuziongoza, badala ya kuweka watu ambao hawana misingi ya sayansi
Wataalam wameshindwa hasa kwenye uwaziri. Inavyo onekana Ili uwe waziri Bora inaitajika uwe na projo nyingi kuliko ujuzi.

Lejea afya , Dk Davide Mwacyusa , na Dk Gwajima hawajakaa sana.

Miundo mbinu wamepita ,DkShukuru kwambwa, mhandisi Isaki kamwelwe, mhandisi Greson Lwenge , hao wote hawajaweza kufurahisha hadila.

Elim nako hivohivo.
 
Mhhhh!

Tujiulize ameacha majanga mangapi kwenye Wizara aliyokuwa anaiongoza ndio aje arudishwe tena.

Ina maana hakuna Wabunge ambao wana uweledi wa kuongoza wapewe hizo Wizara kuliko kuwarudisha tena wale walioshindwa kuongoza.
 
Back
Top Bottom