Dkt. Kigwangalla aliwashia moto gazeti la Jamhuri kwa 'kumchafua'

Naanza ku conculde kwamba ni makosa kuwapa vijana uongozi. Tuwaachie wazee. Uongozi unahitaji utulivu na hekima vitu ambavyo vinapatikana uzeeni. Niliandika hapa kwa kirefu

Mkuu vijana wa Tanzania ndiyo shida. Wamezidi tamaa na wanataka kuabudiwa. Wanapenda ujiko na wana njaa ya kupanda ngazi kimadaraka kwa haraka. Hawana subra. Orodhosha vijana karibu wooote walio kwenye nafasi za uongozi kuanzia ukuu wa wilaya kwenda juu uone. Kwanza wengi ni wapiga dili. Sioni wenye busara au wanaofaa kuwa viongozi wa kesho. Huyu Kigwa ndiyo kabisaa.. hovyo kabisa. Hata ukuu wa Wilaya siyo saizi yake. Nashangaa Magufuli anatoka wapi na watu kama hawa.
 
Hili gazeti linachapishwa na kampuni gani?
 
Balile na gazeti lake aache kutumika ,atashindwa kama alivoshindwa issue ya Makonda,baada ya Nape Nnauye Kutaka kumtumia kummaliza Makonda.

Misheni hii itafeli tu,

Kigwangala ni kijana mtiifu na mchapakazi hodari wa Rais Magufuli,hili halina ubishi,

kuhusu mafanikio ya wizara ya maliasili alivyoikuta na ilipo sasa hata kabla ya Adolf Mkenda hajapelekwa wizara hiyo,kuna ufanisi sana,mapato yameongezeka
Ikumbukwe rais Magufuli ana vyanzo makini na vyenye weledi katika kumpatia taarifa muhimu kuhusu sakata hili ndani ya wizara ya maliasili.
Hategemei gazeti la Jamuhuri ,gazeti hili lilifanikiwa mishe moja tu ya sakata la mafuta bandarini na kupatiwa hongera na rais Magufuli,toka hapo Balile akavimba kichwa.

Kilichotakiwa ni Balile kuhakikisha anapata maelezo ya upande wa pili wa Kigwangala ili kubalance story kabla ya Ku release hadharani ili mbivu na mbichi sisi wasomaji tuchague.
Lakini kinachoonekana ni Balile kutumika na Adolf Mkenda kummaliza Kigwangalah.

Angalizo,
Wakati rais Magufuli anamuapisha Adolf Mkenda alimwambia anampeleka Maliasili na huko pia akavurunde,hatamuhamisha tena ,ispokua ni kula kichwa.

Mwisho
Wasanii ni kiungo muhimu Sana kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu,si kwa Kigwangalah tu hata Rais Magufuli mwenyewe anawahitaji sana tu.

Namalizia kwa kusema Rais Magufuli ni makini sana na maamuzi yake yatawashangaza wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo wakili aliyeandika hii barua nimemkubali alivyopangilia hoja na anavyowasilisha na sain yake hiyo...
 
Kigwangalla.jpg

Waziri wa Maliasili na Utalii, na Mbunge wa Nzega Vijijini, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Dkt. Hamisi Kigwangalla, amechukua hatua za kisheria kwa wahariri na wamiliki wa gazeti la Jamhuri kwa madai kuwa wamekuwa wakimchafua katika machapisho yao.

Ambapo amechukua hatua ya kuwaandikia barua na amewataka wamuombe radhi kwenye machapisho mawili ya gazeti hilo yatakayotoka ukurasa wa mbele, na yawe yanafuatana au kutoa fidia ya shilingi milioni 500 kwa kuchapisha habari ambayo hawakuwa na uhakika nayo na akidai kuwa wamemchafua na kumzushia uongo.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na kampuni ya Uwakili ya FMD Legal Consultants &Advocates kwa Gazeti hilo amesema kuwa kwenye makala iliyotoka tarehe 12 – 18 Novemba 2019 waliandika makala yenye kichwa cha habari ‘WANASWA UHUJUMU UCHUMI’, ndani yake ilihusisha kampuni za Kitalii za Ker and Downey, chini ya makampuni ya Friedkin, na gazeti hilo lilimtaja Dkt. Kigwangalla kwa jina na kwa cheo kuwa anawalinda kampuni hii dhidi ya makosa yao ya kikodi.

Waraka huo wa madai, ambao umevuja kwenye mitandao ya kijamii, unasema kuwa gazeti hilo lilichapa habari hizo bila kuwa na uhakika nazo, wakijua ni za uongo na walifanya hivyo kwa makusudi kwa malengo ya kumchafua Dkt. Kigwangalla ambaye ni mtu mwenye heshima kubwa na mamlaka ndani ya jimbo lake, Chama Chake na nchi yote’

Na kwamba walisambaza sana kwenye mitandao ikiwemo ya kijamii bila hata kufanya uthibitisho wa habari zenyewe wala kumuuliza Dkt. Kigwangalla ambaye anatuhumiwa.

Hata hivyo waraka huu, ambao umewafikia gazeti la JAMHURI tarehe 6 January 2020, umekutana na gazeti lingine la JAMHURI la tarehe 7 January 2020, likiwa limemuandika tena Dkt. Kigwangalla.

Zaidi soma:

IMG-20200106-WA0043.jpg

IMG-20200106-WA0044.jpg

IMG-20200107-WA0015.jpg

====

Akianza kushindana na magazeti, kutamfanya atumbuliwe mapema tu.
Bora angenyamaza. Mbona mwenzake katajwa lakini hajalalamika? au ndo kusema jiwelimerushwa gizani.
 
Tuko busy na Iran VS USA, huu upuuzi tutaujadili hali ikitulia hukomashariki ya kati.
 
Kwa huu upupu ulioandika hapa Wallah unalako jambo ama umetumwa.
Mkuu vijana wa Tanzania ndiyo shida. Wamezidi tamaa na wanataka kuabudiwa. Wanapenda ujiko na wana njaa ya kupanda ngazi kimadaraka kwa haraka. Hawana subra. Orodhosha vijana karibu wooote walio kwenye nafasi za uongozi kuanzia ukuu wa wilaya kwenda juu uone. Kwanza wengi ni wapiga dili. Sioni wenye busara au wanaofaa kuwa viongozi wa kesho. Huyu Kigwa ndiyo kabisaa.. hovyo kabisa. Hata ukuu wa Wilaya siyo saizi yake. Nashangaa Magufuli anatoka wapi na watu kama hawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa kama ana akili ya kuzaliwa ni afadhali ajiongeze kwa kutokugombana na watu ajikalie kimya tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Namkumbuka mzee wangu wakati akiwa mwana siasa tena zama za chama kimoja, alikuwa ana niambia ukitaka udumu katika nafasi yako au uwe na sifa nzuri ya uongozi, usibishane na waandishi wa habari. Chunga sana kutofautiana nao maana wataweza kukuangusha muda wowote.
Naona kama Kigwa yana kwenda kumtokea makuu sasa hivi.. Maana naamini yaliyo andikwa ni ya kweli kabisa.. Na sitegemei gazeti limuombe radhi zaidi ya kufichua siri nzito zaidi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom