Dkt. Kigwangalla aliwashia moto gazeti la Jamhuri kwa 'kumchafua'

Huyo wakili aliyeandika hii barua nimemkubali alivyopangilia hoja na anavyowasilisha na sain yake hiyo...
Tuache kwanza pembeni "alivyopangilia hoja na anavyowasilisha"..., mimi ningeshukuru sana aniambie anatumia dakika ngapi kuiandika saini hiyo, na ningeshukuru akaweka sampuli ya pili hapa ili nilinganishe na hiyo ya kwanza kama zinafanana.

Nadhani huyu na Donald Trump ni ndugu wa tumbo moja.
 
Je, Professor Adolf Mkenda, ana andaliwa kugombea ubunge wa Rombo 2020?

Na baadae kuteuliwa kuwa waziri?



Je, Mwanri, ana andaliwa kugombea ubunge wa Siha 2020?

Na baadae kuteuliwa kuwa waziri?
 
Kwasbabu ni mzoefu, anaweza asikosee
 
Amesahau kuwa ukivuliwa nguo basi chutama
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hio ni ndoto huyu ni praise team
 
..ina tegemea nani yuko nyuma ya Jamhuri.

..Kigwangala anaweza kushtukia mazungumzo yake ya siri yanawekwa hadharani.
Alipoanza kubishana na Bashite juu ya yule kijana mchora 'cartoon' aliyejiweka kwenye nafasi aliyoambiwa amevuka mipaka ya kazi yake; angeanzia hapo kuhesabu maumivu yake

Mbona hakumwekea wakili huyo kijana kama alivyokuwa ameahidi?

Kigwa ni mtafuta sifa kama bosi wake, lakini hajui mipaka yake ipo wapi.
 
Kwani ni uongo? Umezidi waziri tabia mbaya mchafuzi wa mazingira kha mara kisarawe mara sijui wapi! Tulizana akina ebitoke na uchafu mwingine mnaogombania na mwenzio mnashangaza ati!
Mkuu akina Ebitoke wanaitangaza Tanzania,yaleyale aliyoyafanya Nyalandu ya kuwapeleka Marekani akiana Ant Ezekiel ndio anayoyafanya Kingwa na akina Ebitoke ,yale mahema ya mbugani mbona yanavopata shida Mungu ndie anajua.
 
Dr of Medicine na wanyamapori wapi na wapi! Sionagi hata anachokifanyaga zaidi ya kupenda kupost insta. Kazi atafanya sa ngapi!!!
 
Kigwangala mhuni sijui kwanini mh rais anamlealea yani hapo yupo kutafuta huruma kiongozi gani anapenda kiki kama msanii wa bongo movie or bongo fleva

Tarifa zake za kutengeneza matukio nakujifanya hajui tunazo na tunazijua tangu awamu ya nne akiwa mbunge wa jimbo la nzega

Aliwapanga askari eti anandamana kudai haki za wachimba madini waende wajifanye wanamkamata wanampiga wanamuweka mahabusu yote alifanya kuwahadaa wanainchi waone yupo nao pamoja kumbe ilikuwa sinema tu kwaiyo hata hili la gazeti la jamhuri kaenda yeye kuwambia wandike ili aje na huu ujinga wake kujifanya anawaburuza mahakamani tunakujua saidi acha utoto

Ulipokuwa wizara ya afya umefanya ujinga mwingi kwa maslahi yako issue ya dokta mwaka tupo kimya ila tunajua ulipiga pesa haya kitendo cha kwenda wizara ya afya unachukua majina ya wanafunzi walioomba wadahiliwe vyuo vya afya vya serikali wewe unawadahili kwenye chuo chako cha afya nakuwaongopea wazazi kuwa watoto wao wamepata chuo cha uma kumbe siyo huo ujinga umefanya sana umeumiza watoto wawatu unawapeleka uko chuoni kwako miundo mbinu tatizo wakufunzi tatizo

Wewe ni mpigaji tunakujua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…