OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Hamis Kigwangala ambaye ni daktari wa afya ameandika meengi katika mtandao wake wa instagram. Kwa tafsiri rahisi ni kwamba anashauri herd immunity.
Kutokana na mwenendo wa serikali katika mapambano dhidi ya corona Je,huu ndio msimamo wa serikali?
Mbona maambukizi mapya hayatangazwi,mbona vifo havitangazwi. Upuliziaji wa dawa ya kuua virus huko Dar es Salaam mbona umesitishwa?
Naomba kuwasilisha hoja
----
Kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika...
Ugonjwa wa COVID-19 tunao na ushasambaa nchini kote. Ndugu zetu wenye umri mkubwa ama wenye magonjwa mengine wanaathirika zaidi ama wanapoteza maisha kabisa. Hatuna chanjo wala tiba, we are helpless kama binadamu.
Kipindi kigumu sana kwa walimwengu na ulimwengu. Maisha yetu yamebadilika sana na kamwe hayatokuwa sawa tena, baada ya janga hili. Life has changed and shall remain changed for good; pengine mpaka pale tutakapopata chanjo ama dawa ya kutibu COVID-19.
Kwa sasa tunahitaji utafiti wa namna ya kurudi kwenye maisha yetu taratibu. Utafiti utuambie lini tuwe tayari kurudi kawaida. Na siyo mbali sana. Maana tumechoka kuishi kwa mashaka. Pengine tujue tu kuwa haya ndiyo yameishakuwa maisha yetu. Our ‘new normal’.
Utafiti utuelezee new normal itakuwaje. Wananchi wasisitizwe kuishi kwa kuendelea kuchukua hatua za kujikinga dhidi ya Covid-19. Wajue namna ya kuzika sasa inakuwaje, serikali isaidie kushiriki mazishi ya watu wetu watakaopata bahati mbaya ya kifo dhidi ya ugonjwa huu, wawazike kwa mila na desturi za dini zao kwa kuzingatia misingi yote ya kujikinga dhidi ya maambukizi.
Hotel zifunguliwe, watu tuanze kutembea kwa amani, tujamiiane kwa kuzingatia ‘social distancing’ n.k. Hakuna haja ya karantini tena, hakuna haja ya ‘social isolation’ tena.
Kuvaa barakoa ndiyo our new normal. Tuanze kushona za kifashion fashion hivi. Tuzowee. Kunawa mikono kila wakati nayo Ndiyo ishakuwa another new normal. Tuzowee tu. Kukaa mbalimbali, kuto-shake hands ndiyo ishakuwa new normal. Tuzowee tu. Bajeti yetu tuielekeze kwenye tiba na kuwalinda askari wetu wa mstari wa mbele.
Tuwekeze kwenye kuiboresha mifumo yetu ya kuwatibu wale asilimia chini ya 5 watakaopata ugonjwa serious zaidi. Utafiti utakaoambatana na kupima utusaidie kujua ni watu wangapi wanaoweza kuwa wameambukizwa na wakapona na kiwango cha maambukizi kikoje kiasi tujue kama tunaweza kupata kinga ya jamii yote baada ya muda gani? (Herd Immunity).
Jamii ieleweshwe kuwatenga na kuwalinda wazee na wenye magonjwa mengine. Tunahitaji utafiti haraka turudi makazini kama mwanzoni tuishi na adui bila hofu ila kwa tahadhari kama Dance ya Simba na Swala.
Hatuwezi kuendelea kwenda mbele