Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mbunge wa Nzega Mjini, Dkt. Hamis Kigwangalla ameshauri mashine ya kujifukizia iliyowekwa Hospitali ya Muhimbili ivunjwe na watu wafauate hatua za kujikinga na #COVID19 ikiwemo kupata chanjo.
Kigwangwalla amesema wataalamu wa Afya wana jukumu la kumshauri Rais Samia na yeye kama mbunge watalizungumza bungeni ili kuanza kufuata njia za kisayansi.
Amesema si sawa kwa taasisi kubwa kama Muhimbili kuwa na mashine za kupiga nyungu, ni muhimu watu kufuata hatua a afya kama kuvaa barakoa nk
Zaidi, Soma: Baada ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kusema hawatavunja mashine za kujifukiza, Kigwangalla ahoji zaidi...