Dkt. Kigwangalla: Mashine ya nyungu iliyo Muhimbili ivunjwe, viongozi wavae barakoa

Dkt. Kigwangalla: Mashine ya nyungu iliyo Muhimbili ivunjwe, viongozi wavae barakoa

Kila siku tulikuwa tunasema hapa JF kuwa Magu alikuwa anataka kuwafanya watanzania wote kuwa mataahira, yaani wasitumie akili zao. Sasa Magu ameshakufa, watu wale wale waliokuwa wamemzunguka na kumshangilia Magu wameanza kufunguka kwa akili zao na kumponda vikali.

Asante sana Covid kwa kurahisha safari ya kumzimisha mwamba. Ni huzuni kufa kwa Rais wetu lakini ni mwanzo wa kupona taifa letu.
 
Huyu si alituambia habari za head to head immunity au?

Viongozi wengi wa kisiasa wamejaa unafiki na uchumia Tumbo,kama kingwalla alikuwa hakubaliani na Sera za JPM ilipaswa ajiuzulu kipindi kile ni waziri,lakini sababu ya njaa na unafiki aliendeleea kuwepo,

Huyu mtu kama anadhani mama samia atampa uwaziri asahau,ni mpuuzi sana

Bora ya January na Nape ambao walionekana kumpinga JPM hadharani,hawa watu si wanafiki
Hapo mtoe January

Nape nae Ni yule yule fala tu na mnafiki hatari sana
 
Kingwangala mnafiki sana kuliko shetani, huyu huyu alikuwa ameandika insta kuwa the Late JPM anamlilia sana na hakuna kiongozi kama Magu, akataja sifa lukuki ikiwemo alikuja kumuona akiwa mgonjwa, mara alimpa ndege alipofiwa na mtoto wake, leo hata maombolezo hayajaisha kashamgeuka, mnafiki hana tabia za kujificha, unafiki huwa unaonekana wazi wazi.. Hivi ndio inafaa Mama Samia aangalie hawa watu awajue, who is who.. Kifo cha Magu kinawaonyesha wengi sura zao halisi. Kaa mbali na wanafiki
 
UKISOMA HII UTAJUA:

Stalin baada ya kifo chake alirithiwa na Nikita Khrushchev., Siku mmoja akiwa ana hutubia Kamati Kuu huku akipinga sera nyingi ya mtangulizi wake, Mjumbe mmoja bila ya kujitambulisha alikereka na akamundikia ki note cha kumshutumu na kumlaumu, "we Nikita ulikua msaidizi wa Stalin, "kwa nini hukusema haya kipindi hicho Stalin akiwa hai?" Khrushchev akakisoma na akaomba Mjumbe aliye andika anyooshe mkono juu amtambue ili amjibu .Hakuna mkono uliyo nyooshwa, Khrushchev akasema "kinacho kushinda wewe kunyoosha mkono leo , ndo hicho hicho kilicho nishinda mimi kusema enzi hizo"

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Kwani ni lazima kuongea, ni bora kukaa kimya kuliko kuwa mnafiki kiasi hiki.
 
Vile wataalam wa muhimbili wanavyoshangaa baada ya kusikia hii taarifa ya MNAFIKI..

IMG_20210318_083428.jpg
 
Wana bodi.

Kama wasemavyo wahenga paka akiondoka panya hujitawala ndivyo unavyoweza kusema kwa Kigwangala.
Corona ipo kwa zaidi ya mwaka ,waliokuwa wamefanya lockdown wamechoka, waliochanjwa wamechoka ,wanaovaa barakoa za N95 wamechoka.
Jana tabibu mkuu huko Uingereza amesema wamechoka na wameamua wataishi na Corona kama mafua ya msimu tu.

Yote haya yakiwa yanatokea duniani, huku kwetu Tanzania anatokea Kigwangala na kuwataka Muhimbili waachane na tiba mbadala na viongozi wavae barakoa na watanzania wote tuchanjwe.!
Kigwangala fafanua tuchanjwe chanjo ya wave ipi ya Corona? Kumbuka sasa hivi tuko third wave of Corona na chanjo feki zimetapakaa kila kona.

Maana yake huyu Kigwangala angekuwa rais tungelazimishwa kuvaa barakoa za N95 nchi nzima ,lockdown nchi nzima huyu ni
mzee wa copy and paste.

Bila shaka Kigwangala anatumika na atakuwa amelipwa hela nzuri ili apigie debe hizi chanjo!, lakini hao wanaomtumia wamechelewa maana kote duniani watu wameamka na wanakubali hayati Dr Magufuli alikuwa sahihi kwenye mbinu za kukabiliana na hili gonjwa.
 
Huyo itakuwa sio Dr Kigwangala aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii enzi.
Walivyokuwa wanashadidia tiba za asili, nyungu ikiwemo enzi za hayati Magufuli leo hii wanakumbuka kuna sayansi.
Waliosema mwanasiasa akikuambia habari za asubuhi, amka ukaangalia nje kama kumekucha hawakukosea.
 
Ana point sana, sema kaileta wakati ambao sio sahihi..
 
Back
Top Bottom