Sawa na ccm watataachia nchi lini tangu ,1961 mpaka Leo hakuna la maana wamefanya zaodi ya rushwa na ufisadiIla kwa hali ya kisiasa ilivyo na yaliyotokea kwenye awamu ya 5 bado Mbowe ni kiongozi sahihi wa CHADEMA. Ukimtoa Mbowe hakuna kiongozi mwingine anayeweza kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa sasa. Lissu na ule uropokaji hafai. Mbowe ana busara na uvumilivu wa kisiasa. Pia anajua kudili na CCM kidiplomasia pamoja na madhila ya hapa na pale anayokutana nayo. Kina Lema, Sugu, Msigwa, Heche, Pumbulu ni hovyo kabisa.
╱◥██████◣Hili alilolisema kuhusu Mbowe na maelezo yakoo kuhusu Kijijini kwao yanashabihiana vipi?
Sawa Mkuu,Tujikite kwenye hoja yake
Mkuu matongee,Ila kwa hali ya kisiasa ilivyo na yaliyotokea kwenye awamu ya 5 bado Mbowe ni kiongozi sahihi wa CHADEMA. Ukimtoa Mbowe hakuna kiongozi mwingine anayeweza kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa sasa. Lissu na ule uropokaji hafai. Mbowe ana busara na uvumilivu wa kisiasa. Pia anajua kudili na CCM kidiplomasia pamoja na madhila ya hapa na pale anayokutana nayo. Kina Lema, Sugu, Msigwa, Heche, Pumbulu ni hovyo kabisa.
Chadema kama chama mbadala kilipaswa kuonesha mfano mzuri wa kuheshimu na kufuata misingi ya demokrasia. Kujificha kwenye madhaifu ya ccm ni kuutangazia umma kwamba chadema ni sawa na ccm.Sawa Mkuu,
Utaanzaje kutoa kibanzi kwenye jicho la mwenzio na kusahau boriti kwenye jicho lako mwenyewe..
Kila mwamba ngoma huvutia kwake lo
Aende wapi? Bado yupo sanaaa, hadi CDM wenyewe waamue!! Naona kuna kile ki dada kilikuwa chadema huko geita, UPENDO, kila muda kinahangaika kuisema chadema,!! Kweli ukiwa magamba hata kama prof. akili yako inazidiwa na mtu wa std sevenMBOWE aondoke
Whatever the name ndo huyohuyo nilitaka kumaanishaMkuu matongee,
nikusahihishe kidogo kwenye jina la bwana mdogo Ni pambalu sio pumbulu
Hakuna mwana ccm anayeitakia mema CDM!! Kipindi cha jiwe mlisema lazima kife, ikashindikana, na sasa kitawatesa sana, kwani wananchi wameshaanza kuelewaChadema kama chama mbadala kilipaswa kuonesha mfano mzuri wa kuheshimu na kufuata misingi ya demokrasia. Kujificha kwenye madhaifu ya ccm ni kuutangazia umma kwamba chadema ni sawa na ccm.
Babu zako waliokuwa wakitembea zaidi ya kilometa 10 kuitafuta shule ilipo wakisoma hii comment yako watakulaani.Sawa na ccm watataachia nchi lini tangu ,1961 mpaka Leo hakuna la maana wamefanya zaodi ya rushwa na ufisadi
Kwaio,Whatever the name ndo huyohuyo nilitaka kumaanisha
Kijani wala nyasi kwa urefu wa kamba😆Unaa ndio nini? Kijani kibichi au kipi?
Sawa mkuu,Chadema kama chama mbadala kilipaswa kuonesha mfano mzuri wa kuheshimu na kufuata misingi ya demokrasia. Kujificha kwenye madhaifu ya ccm ni kuutangazia umma kwamba chadema ni sawa na ccm.
Demokrasia ni katiba ya nchi au chama ambayo inampa kiongozi wa chama au nchi akae madarakani kwa muda fulani uliyowekwa na chama au nchi husika.kwani demokrasia kwa tafsiri yako ni nini?
Kushindana na mtu aliebadilisha katiba ili miaka yote aendelee kutawala ni kazi bure. Yeye ndio kiongozi wa wapiga kura na wahesabu kura, hivyo uwezekano wa uchaguzi huo kuwa wa haki ni mdogo sana. Ni sawa na mpinzani ashindane na raisi katika uchaguzi. Uwezekano wa mpinzani huyo kushinda uchaguzi huo ni mdogo sana hata kama yeye atakuwa amepata kura nyingi kushinda raisi.kwani hawaruhusu watu wengine kugombea? mbowe huwa anapita bila kupingwa? nisaidie mkuu maana mimi nimezaliwa 2010
Kama Kuna kitu kitafanya cdm kuonekana ni chama Cha hovyo ni kukubali Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti tena. Katika jambo ambalo siwezi kuunga mkono cdm, ni hiki kitendo Cha kuruhusu kiongozi mmoja kukaa madarakani muda mrefu hivyo. Kwenye hili siko tayari kuunga mkono, na Sina hofu na kamanda yoyote wa cdm hata watukane watakavyo, maana hayo matusi yenyewe nayamudu vyema.Miaka ile nilipendekeza CHADEMA ingeongozwa na Kamanda John Heche baada ya Kamanda Mbowe kumaliza muda wa uongozi wake. Maana huyu jamaa alikuwa ni Mwenyekiti wa ukweli sana wa bavicha ukimlinganisha na Wenyeviti wengine! Aisee nilishambulwa mpaka basi na Makamanda wa humu jukwaani.
Na nilitoa hoja nzuri tu! Ila sikueleweka hata kidogo. Na badala yake nikaonekana eti mimi ccm!!
Kiukweli mpaka sasa bado sijaona mantiki kwa Kamanda kuendelea kuishikilia hiyo nafasi ya Uenyekiti kwa vipindi zaidi ya viwili! Huku chama chenyewe kikifahamika kama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
Kwangu mimi nilitamani kiwe mfano wa kuigwa kwa vyama vingine vya siasa nchini kwenye kipengele cha Demokrasia na Maendeleo. Ni vizuri akasimama kwenye ile ahadi yake ya kutogombea kwenye uchaguzi wa mwaka 2023! Na baadaye huo uchaguzi kusogezwa mpaka mwaka huu wa 2024.
Uko sahihi sana, Mbowe must go. Kwa sasa Mbowe anaipotezea cdm haiba yake, kuliko anachoipa cdm.Demokrasia ni katiba ya nchi au chama ambayo inampa kiongozi wa chama au nchi akae madarakani kwa muda fulani uliyowekwa na chama au nchi husika.
Katiba ya Chadema iliyotungwa wakati wa uanzishaji wa chama ilikuwa ni ya mihula miwili tu ya miaka mitano mitano. Mwenyekiti wa chama aliechaguliwa kidemokrasia na chama aliruhusiwa kukaa madarakani kwa muda wa miaka mitano ya muhula wa kwanza, na endapo atahitaji kuendelea basi itabidi agombee tena na akishinda amalizie muhula wa pili.
Muongozo wa katiba hiyo ulifuatwa na viongozi wote waliotawala kabla ya Mbowe. Alianza mzee Mtei akatawala, mihula yake ilipoisha akatoka kwa mujibu wa katiba na kumpisha mgombea mungine aliegombea na kushinda uenyekiti (Bob Makani)
Marehemu Bob Makani nae akafuata katiba ya chama kwa kutawala mihula miwili kisha akaacha wagombea wengine wapambane, mshindi akawa Mbowe, Bob Makani akamkabidhi kijiti kwa mujibu wa katiba ya chama.
Mziki ukaja kwa Mbowe ambae hakutaka kutoka katika kiti, akaamua kubadilisha katiba ili aendelee kuwa anagombea miaka yote mpaka uzeeni. Na kwa mazingira yetu ya kiafrika ni vigumu sana mtu wa kawaida kushindana na kiongozi aliepo kwenye kiti, maana yeye ndo boss wa wapiga kura wote, na pia boss wa wahesabu kura wote.
So ni rahisi mno kuwadhibiti, kuwahonga au kuwatisha ili wampitishe. Nafikiri umeshasikia Lisu akilalamika juu ya rushwa inavyotembea katika chaguzi. Sasa kwa mantiki hiyo hata kama wanachama hawamtaki mwenyekiti yeye ataendelea kupita tu kwa sababu ana hela za kuwahonga.
Kushindana na mtu aliebadilisha katiba ili miaka yote aendelee kutawala ni kazi bure. Yeye ndio kiongozi wa wapiga kura na wahesabu kura, hivyo uwezekano wa uchaguzi huo kuwa wa haki ni mdogo sana. Ni sawa na mpinzani ashindane na raisi katika uchaguzi. Uwezekano wa mpinzani huyo kushinda uchaguzi huo ni mdogo sana hata kama yeye atakuwa amepata kura nyingi kushinda raisi.
So mkuu usidanganyike na watu kuchukua fomu kushindana na Mbowe, ile ni geresha na hata hao wachukuaji fomu hujua kabisa kwamba hawatoweza kushinda kwa namna yoyote ile.
BWANA mkubwa,Kama Kuna kitu kitafanya cdm kuonekana ni chama Cha hovyo ni kukubali Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti tena. Katika jambo ambalo siwezi kuunga mkono cdm, ni hiki kitendo Cha kuruhusu kiongozi mmoja kukaa madarakani muda mrefu hivyo. Kwenye hili siko tayari kuunga mkono, na Sina hofu na kamanda yoyote wa cdm hata watukane watakavyo, maana hayo matusi yenyewe nayamudu vyema.
Nilipinga Lowassa kupewa nafasi ya kugombea urais ndani ya cdm bila hofu. Na Sasa naendelea kupinga Mbowe kuwa mwenyekiti muda mrefu kiasi hiki, huku akiwa Hana tija tena.
Na mfumo unataka Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti, ili waendelee kumtumia yeye kama kiongozi wa chama kuwafinya kimya kimya wale wote wanaojaribu kuichalenji serikali.Uko sahihi sana, Mbowe must go. Kwa sasa Mbowe anaipotezea cdm haiba yake, kuliko anachoipa cdm.
Uongozi wa Mbowe ni aibu kwa democrasia. Kiongozi unaposhindwa kuandaa wengine kuchukua nafasi yako na kuona kama wewe pekee ndiye anayefaa, hapo umefeli kama kiongozi.Ni wazi Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema unafuatiliwa zaidi na viongozi wa CCM kuliko Wanachadema wenyewe
Dkt. Kigwangalla amechachamaa ukurasani X akidai Mbowe hataki kuachia Uenyekiti wa Chadema
Anasema ACT wazalendo ni Chama kidogo lakini tayari Kiongozi mkuu amestaafu baada ya mihula miwili lakini Chadema Mwenyekiti ni yule yule
Zitto alijaribu kugombea Uenyekiti lakini Mbowe akamfukuza uanachama, sasa kaka yangu Tundu Lisu naye ajiangalie huyu Mwenyekiti aitwe Kabaka Mbowe au Ayatollah Mbowe, amesema Daktari Bingwa Kigwangalla.
View attachment 2995118