wabongo tunapenda tu kuwasema watu maarufu, utasikia mbona hiki hajasema mbona kile kaacha. Hata mimi(ambaye sina umaarufu) nikiandika kitabu kuna mambo siwezi kuandika kwa sababu mbalimbali. Hata Mandela hakusema yote. ishu nyingine ni sensitive sana na zinaweza kuwakera wengine waliohusika.
kitabu cha 'kweli' kitakachosimulia habari za Nyerere ni kile cha aliyekua secretary wake bi Joan Wicken ambacho kwa bahati mbaya kitatoka 2034. Naona alikadiria kwamba kufika huo mwaka wahusika wote watakua wamefariki.
Mkapa alijua fika hatapata nafasi ya kukisoma na alisikita sana. Nadhani hata wazee wa mapinduzi ya 1964 wangeandika na kuruhusu hata kiachiwe baada ya miaka 80 lingekuwa jambo zuri.
waafrika tunakosa taarifa sahihi kutoka kwa wazee kwa sababu wana viapo vya kutosema baadhi ya vitu , wenzetu wanajifunza vingi sana kutoka kwenye hizi historia. Pengine Nyerere angeandika kitabu na kutuonyesha ni wapi sera zake zilifeli na tujirekebishe vipi leo hii kuna vitu tungejiepusha navyo.