Dkt. Kikwete: Ninaandika kitabu cha historia yangu ambacho ninaelezea mambo mengi hata yale msiyoyajua!

Dkt. Kikwete: Ninaandika kitabu cha historia yangu ambacho ninaelezea mambo mengi hata yale msiyoyajua!

Aandike Hadi Yale ya ndani kabisa, watu tuyajue: binafsi nataka kujua baba yake alihusika vipi katika siasa ya Tanzania, aliwezaje kuwa mwanajeshi wakati muda mwingi alikuwa akitumikia chama sehemu mbalimbali, kwanini aliachana na mke wake wa Kwanza tunataka tumfahamu pia na yupo wapi kwa sasa(mama ridhiwani), kwanini suala la ufisadi hakulichukulia serious. Ni kujua tuu basi
 
Inawezekana hawa watu maarufu kama kina kikwete,mengi,mkapa,Chande n.k wana siri kubwa nyuma yao!Inawezekana wameuza idadi ya miaka yao kwa Lucifer ili wapate mafanikio!!!Ndio maana muda wa makubaliano ukifika wanaandika vitabu ambavyo hata mapato yao hawali vizuri wanakufa baada ya mwaka au muda fulani!!
Hivi unaweza kuuza miaka yako kwa Lucifer, ebu nielimishe hapa
 
Ongea kwani bado uko hai ili tukusikie live hayo makando kando mmmm
 
Anaandika yale anayotaka tuyajue lakini haandiki historia ya ukweli wa maisha yake, hiyo nakataa.
 
Haha mzee labda ahamasike baada ya kuona wenzake wote wametoka vitabu, lakini kwa umri ule atakuwa na kumbukumbu ya mambo yote yaliyotokea kipindi cha his reign?
Miaka zaidi ya tisini sidhani Kama hata kumbukumbu iko sawa,
 
Aandike Hadi Yale ya ndani kabisa, watu tuyajue: binafsi nataka kujua baba yake alihusika vipi katika siasa ya Tanzania, aliwezaje kuwa mwanajeshi wakati muda mwingi alikuwa akitumikia chama sehemu mbalimbali, kwanini aliachana na mke wake wa Kwanza tunataka tumfahamu pia na yupo wapi kwa sasa(mama ridhiwani), kwanini suala la ufisadi hakulichukulia serious. Ni kujua tuu basi
Mke wa kwanza alitangulia mbele ya haki.

Nitafurahi akiandika anayofahamu kuhusu pesa ya escrow iliyosombwa kwenye magunia na magari ya Ikulu.
 
Rais mstaafu wa awamu ya 4, Mh. Mrisho Jakaya Kikwete amesema kwa sasa anaandika kitabu cha historia ya maisha yake ambacho kitaelezea mambo aliyoshiriki, aliyoyashuhudia na aliyoyaona katika maisha yake binafsi na yale ya siasa.

Kikwete amesema hayo wakati wa mahojiano na mwandishi Salama Jabir katika kipindi cha Salama leo.

Chanzo: Eatv.

Maendeleo hayana vyama!

Kuna uzi mmoja ulikuwepo uliuliza inakuwaje mtu akishaandika kitabu kuhusu life lake then baada ya muda mfupi anakata kamba? Hilo swali halihusiani na vitabu vya Mengi,Mkapa au Le Mutuz.
 
Daah, ni kweli Ila upole nao ni mbaya, kipindi kile maandamano Kila wakati,matamko ya vyama vya wafanyakazi Kila wakati, sahizi kimyaaa
Wangetoka na misemo kama HATUOGOPI, TUTAPIGANA HADI KUFA ATOKE HUYU. HII NCHI SI YA BABA YAKE N.K
 
Rais mstaafu wa awamu ya 4, Mh. Mrisho Jakaya Kikwete amesema kwa sasa anaandika kitabu cha historia ya maisha yake ambacho kitaelezea mambo aliyoshiriki, aliyoyashuhudia na aliyoyaona katika maisha yake binafsi na yale ya siasa.

Kikwete amesema hayo wakati wa mahojiano na mwandishi Salama Jabir katika kipindi cha Salama leo.

Chanzo: Eatv.

Maendeleo hayana vyama!
Kwisha habari yake...!

Ningekuwa jirani naye ningemshauri asifanye upesi...!
 
Huyu Jakaya si alienda hadi marekani huko kufanya uhariri wa kitabu..ama hiki ni kingine tena.
 
Vitabu ni urithi mzuri sana kwa vizazi vijavyo. Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amelifanyia mengi taifa hili. Mbali na kuwa rais kwa kipindi cha miaka10 amehudumu kwenye serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania tangu akiwa kijana.

Kwangu mimi JK anabaki kuwa shujaa aliyeweza kutegua mtego wa kumuingiza mtuhumiwa wa ufisadi ikulu na kutuletea Chuma JPM💪

Naamini kuna vingi tutajifunza kupitia kitabu chake

Mungu ampe maisha marefu yenye afya na furaha tele Jakaya Kikwete
Mbona mnasema amejijengea mizizi ambayo JPM ndo anaing’oa? Yule mtuhumiwa wa ufisadi yeye JK alidhani ataifuatilia hiyo mizizi yake ndo maana akampiga chini au alifanya kwa maslahi mapana ya Taifa?
 
Yasjayo yanafurahisha tusubiri .....nani atakizindua ? Maana madongo kwa iwe yatakuwepo ....." Hakuna chaguo ......ikatokea ......." Bwana yule hatapenda mengi humo !!
 
Miaka zaidi ya tisini sidhani Kama hata kumbukumbu iko sawa,
Naona amechelewa, angekuwa yuko smart sana alipaswa atoe kabla ya Mkapa. Labda angekuwa ameshatangulia Kama wadau wanavyosema kuwa ukitoa kitabu Cha kuelezea maisha yako one to two year tunakuzika😆😆
 
Wanaandika wakiwa afya zao zina mgogoro sio suala la umri; Barack Obama ameandika na bado anaandika vitabu na hana dalili ya kuondoka siku za usoni kwasababu ya kuandika hivyo vitabu!! Carter, Clinton, Walker Bush na wengine wengi wameandika vitabu na bado wapo!!

Je Alhaj Mwinyi yupo nasi kwa muda mrefu kwasababu hajaandika kitabu?
Ongelea bongo mkuu
 
Back
Top Bottom