Dkt. Leonard Akwilipo: Wanafunzi waliopata mimba Tanzania kurejea masomoni kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi

ni sahihi kabisa maana ukiangalia nchi jirani kenya.. wao haijalishi mtoto wa shule ya msingi au sekondari.. haijalishi amepata mimba ndani au nje ya shule.. wanaendelea na masomo yao kama kawaida na ndoto zao zinatimika na bado wanatuzidi kimaendeleo.. ko haina haja wanafunzi waliopata mimba kusimamishwa masomo.

tuamkeni..
yawezekan one among the reasons that forces these female creatures to engage in love relationship and become pregnant may be their weak background economic status... and they engage in.. and later on accidentally they perceive..

kwahiyo kupata mimba kwa mwanafunzi ni ajali tu kama ajali nyingine.. na hakuna binadamu yeyote ambaye yupo tayari kuharibu maisha yake even if he/she ignorant to what extent. tuamkeni mama aangalie swala hili..
 
Sote tumetokana na mimba!

Sielewi kwa nini iwe stigmatized kiasi hicho!
Well, mimba kwa jamii za kiafrika ni kukosa maadili maana umeanza mambo kabla ya ndoa as you know huku kwetu jamii bado zinaamini mtoto akiwa mkubwa basi aolewe ndio azae kwenye mji wake sio anazalia nyumbani kwa babake.

There is a lot behind this, mtoto wa kike anaheshimika, kama anaheshimika basi asianze kutembea na wanaume wakati anaishi kwao maana inakuwa anadhalilisha ukoo, wanaume wanaomdharau babako ndio maana wanakubeba na wanakurudisha uzalie kwenu.

Story ni nyingi, lakini stigma inatokana na jamii zenyewe zinavyochukulia mtoto au binti kuanza mapenzi mpaka kuzaa ingali yupo kwao.

Stigma pia ni kama detterance kwa wengine wasifanye hayo lakini sasa bahati mbaya ndio inakuwa inamuaffect aliyepata mimba na mtoto anayezaliwa ambaye ni innocent.

Ila wakati mwingine mabinti bila kuwaweka sawa utapata shida watakuzalia hapo nyumbani utalea kila mtoto wa mtu na itamuathiri zaidi mwanao.

So better the lesser harm than the bigger one although zote ni athari.
 
Bado haijakaa poa. Wanatakiwa warudi shule na kuendelea masomo yao. Hao wa ufundi labda watake wao.
 
Kwa nini umtwike mzigo wote binti ambae tumemfundisha kuwaheshimu na kuwapigia magoti wanaume badala ya hao wanaume watu wazima ambao kusudi lao kubwa ni kuwalaghai kwa kutumia nafasi walizokuwa nazo katika jamii? Hatutaki kuwapa elimu kuhusu mambo yao kwa kusema kuwa tutawafundisha umalaya halafu tunashangaa anapopata mimba? Hawa watoto kosa lao ni kuzaliwa kwenye jinsia hiyo na si lingine. Ni unafik mkubwa kuwaweka watoto wetu kwenye pedestal wakati tunafanya kila jitihada kuharibu watoto ambao sio wetu. Na, ndio, hata mabinti wanaofanya kazi kwenye mabaa wanastahili heshima kama ile tunayotaka wake na mabinti zetu wapewe. Ovyo kabisa.

Amandla...
 
Kunyanyapaa aliyepata mimba ni jambo la ajabu sana. Kinachofanya mtihani ni kichwa na mikono sio viungo vya uzazi!
 
Wote waadhibiwe lakini tuwakanye nao sio kuwaambia jibebishe lipanue tu. NO, turudishe kampeni zile za FATAKI na SAY NO.
 
Wote waadhibiwe lakini tuwakanye nao sio kuwaambia jibebishe lipanue tu. NO, turudishe kampeni zile za FATAKI na SAY NO.
Hazijawahi kusaidia. Unadhani mabinti wameanza kupata mimba hivi karibuni tu? Wazee wetu walijua yote hayo ndio maana kulikuwa na vyuo vinavyoitwa jando na unyago. Watoto walipewa elimu tosha kuhusu mabadiliko katika miili yao. Na sio tamaduni yetu kuwanyanyapaa watoto waliopata mimba maana katika jamii zetu watoto walienziwa.

Kwa nini hatujiulizi inakuwaje huko ambako tunasema wanawapa mno uhuru binti zao hawana tatizo kubwa la mimba za utotoni wakati sisi ambao tunajifanya wakali kila siku watoto wanazaa watoto. Inabidi tuache unafik.

Amandla...
 
Hii kitu ya unyanyaoaa wa mabinti waliopata mimba inaweza kufaa kuwa thesis aisee kama haijafanyiwa bado although unaweza kuitwist namna nyingine tu .
 
Hii kitu ya unyanyaoaa wa mabinti waliopata mimba inaweza kufaa kuwa thesis aisee kama haijafanyiwa bado although unaweza kuitwist namna nyingine tu .
Kweli kabisa Mkuu. Mara nyingi tunahusisha mimba na promiscuity, kwamba wanaopata mimba ni wale wanaotembea na wanaume wengi. Tunajisahaulisha kuwa mtu anaweza kushika mimba hata kama ametenda kitendo hicho mara moja tu. Unaweza kukuta wale ambao ni promiscuous hawapati mimba bali wale ambao ni naive au ambao walishikwa kwa nguvu ndio wanapata mimba. Hili zoezi ni la uonevu uliopitiliza, Mkuu. Hatupaswi kutumia kitu arbitrary kama miamba kumuharibia maisha mama na mtoto wake.

Amandla...
 
Hii ni kumnyima mtoto wa kike elimu tu. Na jamii inayotoa adhabu ya namna hiyo Kwa yoyote kwenye Karne ya 21, achilia mbali mtoto, ni jamii backward.
 
Mbna unadharau kaz yangu????
 
Masikini MAGUFULI MAMBO YAKO YANAFUTIKA
 
Mmh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…