Dkt. Leonard Chamuriho atajwa na Rais kuwa ni mtaalam wa kufanya mazungumzo - "Negotiation Expert". Je, hawa watu tunao wangapi?

Hivi huyu Dkt. Leonard Chamuriho kasomea wapi huo utaalam wa negotiation? Huyu si alikuwa Coet Computer Lab kama Lab Technician tu? Au A207 kusimamia installation ya OS tu? Huo utaalamu kautolea wapi?
 
Reactions: BAK
1. Maandalizi
2. Majadiliano
3. Kutanabaisha malengo ya majadiliano.
4. Kuafikiana kuelekea kila mtu kushinda kwa upande wake yaani "win-win outcome"
5. Makubaliano yaani agreement
6. Utekelezaji wa hatua za makubaliano.
Mbali na kanuni hizo za kufuata kwenye majadiliano, muhimu kuliko vyote ni kuwa mtu anatakiwa kuwa ni mtaalamu kwenye theme ya majadiliano. Zaidi anatakiwa kuwa ni mtua anayejua kujenga hoja, na ni fluent katika kuongea. Mtu mwenye kigugumizi (stammering) naweza akawa hafai sana kwenye majadiliano ya namna hii, ijapokuwa aweza kuwa mtaalamu

Ninachokiona mimi kwenye eneo hili, huhitaji kuwa na special qualities sana kuweza kufanya majadiliano, isipokuwa kikubwa zaidi kinachohitajika ni thorough knowledge ya kile kinachohitajika kujadiliwa, halafu uongezee na uwezo wa kujenga hoja pamoja na fluency katika kuongea.
Ukiwa ni expert kwenye area fulani halafu ukampa mtu sahihi theme ya majadala unaotkaiwa kufanyika kwenye eneo hilo, halafu ukambrush na mambo muhimu kwenye eneo hilo, anweza kujadili tena bila wasiwasi, unless mjadala uwe ni too technical kama ule uliohusu mambo ya Makinikia, kwamba lazima kuwe na wataalaum wa kujua hata compotion ya chemical element zinaunda mwamba
Big up sana Dr. Chamuliho. Hata hivyo huyu mjukuu wangu ametulia sana kwa hiyo atakuwa ni mahiri kwa mambo mengi tu na si katika hilo la mjadala tu. Halafu ana sauti nzuri nzito utafikiri anaongea kwa kutumia speaker. I like the man
 
Sawasawa naona umeongelea vipengele namba 1 na 2 yaani maandalizi na majadiliano.

1. Thorough knowledge, theme ya mjadala na vipo katika sehemu ya maandalizi kwani watakiwa kuwa ushajitosheleza kwa hayo.

2. Kujenga hoja na kuwa "fluent" ni sehemu ya kuwa na hizo "negotiating skills" katika majadiliano yenyewe.
 
Unahili kitu hatari sana yani ujumbe wa mtu 100 vs 15 tena hayo majamaa yana akili na exposure yakufa mtu. Jaman tumeliwa sorry kisema hivyo.
 
hata mimi ningeweza ni vile tu idadi ilitosha
 
Nashukuru kwa ufafanuzi huu. Actually hizi ni mbinu za kufanya majadiliano, na orodha iliyoko kwenye post yako yenyewe ndiyo inayobeba utaratibu wa namna ambavyo majadiliano yanatakiwa kufanyika
 
Hamna lolote kwenye masifa hayo zaidi ya kuwa mkusanya RUSHWA ya Meko itokanayo na miradi. Abishe kama hakuchukua mzigo wa Boeing
 
Hamna lolote kwenye masifa hayo zaidi ya kuwa mkusanya RUSHWA ya Meko itokanayo na miradi. Abishe kama hakuchukua mzigo wa Boeing
WAZUNGU HAWATOI RUSHWA, LASIVYO WANGEKUWA WAMEISHAMLIPUA WAKATI WAUCHAGUZI
 
WAZUNGU HAWATOI RUSHWA, LASIVYO WANGEKUWA WAMEISHAMLIPUA WAKATI WAUCHAGUZI
Labda wewe tu ndiyo hujawahi kupata. Usiwasemee wenzio.

Je unakumbuka rushwa ya British Aerospace iliyotolewa kwa ununuzi wa Radar? Je wadhani British Aerospace ni Wachina?
 
NI wapi hapa duniani umeona wafanya hivyo yaani mwananchi wa kawaida apewa nakala ya mikataba baina ya serikali za nchi mbili?
Mkuu, usiwalaumu hao jamaa kwa kutokujua kuwa kuna baadhi ya masuala ya kitaifa yanapaswa kujulikana na watu wachache tu.

Kinachowafanya wakusumbue ni kwamba, walipewa rasimu ya katiba mpya nchi nzima sasa wanafikiri na mikataba pia inakuwaga vivyo hivyo.
 
πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ Excellent question.
Hivi huyu Dkt. Leonard Chamuriho kasomea wapi huo utaalam wa negotiation? Huyu si alikuwa Coet Computer Lab kama Lab Technician tu? Au A207 kusimamia installation ya OS tu? Huo utaalamu kautolea wapi?
 
Yale Yale ya Kabudi na makinikia nayaona tena hapa! Mtu anasifiwa mwisho wa siku anakuja kuitoa nchi marinda bila hata huruma

Kabudi akiulizwa NOAH zetu mlizotuahidi kuwa mtatupa mkisha lipwa hayo makinikia ziko wapi, anang'a ng'a macho tu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…