Dkt. Leonard Chamuriho atajwa na Rais kuwa ni mtaalam wa kufanya mazungumzo - "Negotiation Expert". Je, hawa watu tunao wangapi?

Dkt. Leonard Chamuriho atajwa na Rais kuwa ni mtaalam wa kufanya mazungumzo - "Negotiation Expert". Je, hawa watu tunao wangapi?

Kwanini wanapenda kufichaficha mikataba ?

Ova

Sidhani kama wanaficha nafikiri ni suala la serikali ikikuwakilisha wewe mwananchi wa kawaida.

Hivyo serikali ikiharibu basi ni watanzania wote wameharibu.

Sidhani kama raisi John Mafuguli amekosea kwenye hii mikataba mipya hadi sasa.

Hivyo tumwamini kwani yeye anatuwakilisha.
 
Ni kweli kwa kabudi tunasubiri kishika uchumba stigler tunaolewa kabisa

Matatizo yalianzaia kwa akina chifu Mangungo wa Msovero ambao hawakuwa wnafahamu kusoma na kuandika.

Sidhani kama serikali ya sasa inakubali mambo hayo ya kizamani ya kusaini mambo usoyafahamu.
 
huo mkataba wewe umeuona? au kwa vile magu kasifia basi unaamini ni kweli?

Raisi amemsifia mtaalam wa kufanya mazungumzo.

Hatukuwahi kusikia kuwa Tanzania inaweza kuwa na watu ambao wanaweza kukaa meza moja na wazungu na wakazungumza na kikaeleweka.

Au ndugu umewahi kusikia huko nyuma, hebu tupatie ushuhuda.
 
HATA PROF KABUDI TULIAMINISHWA HIVYO NA MPAKA LEO HAKUNA HELA, SENTI WALA PESA
 
Tumia akili japo hata kwa siku moja badala ya kukurupuka na majibu ya Lumumba!!! Umekuwaje siku hizi weye? 😳😳😳

Zamani ulikuwa ukiandika posts zilizoenda shule sana siku hizi umeunga tela kwa mamburula!!!!

Kama zipo sababu za msingi za kujitoa kwanini haziwekwi hadharani!? Unajitoa vipi katika mpango ambao Wananchi wako walio wengi wanauunga mkono!? Si ndiyo UDIKTETA wenyewe huo?

Kama mpango huo unahusu UN basi kuna sababu za kujitoa.
 
tuione mikataba hio aliyoingia

Sasa akionyeshwa kila mtu si itachukua mwaka.

Pili unapaswa kuiamini serikalki yako inayokuwakilisha kwenye masuala mazito yanayohusu nchi kama haya ya miradi mikubwa.
 
Tumia akili japo hata kwa siku moja badala ya kukurupuka na majibu ya Lumumba!!! Umekuwaje siku hizi weye? 😳😳😳

Zamani ulikuwa ukiandika posts zilizoenda shule sana siku hizi umeunga tela kwa mamburula!!!!

Kama zipo sababu za msingi za kujitoa kwanini haziwekwi hadharani!? Unajitoa vipi katika mpango ambao Wananchi wako walio wengi wanauunga mkono!? Si ndiyo UDIKTETA wenyewe huo?

🙂

Dah! mkuu, haya ngoja niangalie wapi nakosea.

Ila taarifa hiyo ni kwamba kila kiongozi anaengia akikuta mambo fulanifulani huwa wana uwezo wa kukubali mambo hayo yaendelee au kuamua vingine.

Huyu wa sasa amepangua mambo mengi tu,

Nafikiri ndivyo ilivyokuwa.
 
Mkuu nakupongeza sana kwa kuiyona hii angle..!
1. Mh Rais hana unafiki, ukifanya vizuri atakutaja na kukupongeza mbele ya kadamnasi! Huyu Dr Chamuliho katika ununuzi wa ndege kamupni ya Airbus ilitaka imuondoe, ilifikia muda baada ya Airbus kukosa Tender ya ndege kubwa basi walimshtaki kwa Mh Rais kuwa alihongwa na Boeing na ndiyo maana aliwapata ile Tender lakini Mh Rais aliunda jopo likaenda kumfanya uchunguzi mwisho wa siku Dr alionekana yuko Sahihi kwani Airbus ilihitaji fedha nyingi na walihitaji muda mwingi kutuletea ndege, kama ingekuwa ni Aibus basi leo hii tungekuwa bado hatuna ndege kubwa tunasubiri mpaka mwakani ndipo ije lakini Boeing walitoa muda mfupi na hela ikiwa nafuu na hapa ndipo Mh Rais alianza kumuamini huyu Dr.

2. Nilimuona pia Eng; Mfugale kwenye timu ya mazungumzo:- Hili si la kupuuzwa nalo na sitoshangaa awamu ijayo Mfugale akawa Katibu mkuu wa wizara kwani nae kaaminika sana kwa Mh Rais, Mh Rais siku anafungua Flyover pale Tazara alisema Mfugale alitimuliwa na watu fulani kipindi yeye alipopelekwa wizara ya uvuvi lakini aliporudi alimteua tena kuwa mkurugenzi wa Tanrods, ki ukweli Tanzania ilifikia hatua ukiwa mfanyakazi mzuri na mpinga rushwa unadhoofishwa sana lakini leo tunaona Mh rais anavyo watumia hawa watu kutuletea maendeleo.

Niliwahi kuleta thread hapa JF juu Mfugale https://www.google.com/url?sa=t&rct=j&q=&esrc=s&source=web&cd=1&cad=rja&uact=8&ved=2ahUKEwiOlYzl_qDfAhXNXRUIHRgSAp4QFjAAegQIChAB&url=https://www.jamiiforums.com/threads/mawaziri-jifunzeni-kwa-eng-mfugale-kufanya-kazi-na-rais.1510743/&usg=AOvVaw3FykRGvEZQld8jCt_fLZ2m ni kweli watumishi hasa hawa wakubwa wakiangalia kwa jicho la tatu basi wanakila sababu ya kujifunza kitu kwa Eng Mfugale na Dr Chamuliho.

Nakushukuru mkuu kwa kuliona hilo.

Ila nasikitika hadi sasa sijapata post yoyote inayoongelea kwamba hawa wataalaam wa kufanya haya mazungumzo nchi yetu inao wangapi.

Kama nilivyoleza kuhusu Negotiation ni kazi na ni kipaji na pia kinalipa pesa sana.

Halafu kuna mtu amesema huyu Dr Chamuriho pia ni mshauri elekezi yaani ni consultant.

Ni vigumu sana kuamini kwamba tunao watu kama hawa.
 
Sekunde 60 (Sixty Seconds) za Dkt. Leonard M. Chamuriho ktk video clip:

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt .Leornard Chamuriho imetoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya Fidia kwa wakazi wa maeneo yanayopitiwa na mradi wa reli ya kisasa (SGR), ambapo amesema Chuo cha Ardhi kinaendelea na uthamini

Zinaonesha Dkt. huyu wa structural engineering hana ubobezi ktk masuala ya mazito aliyotaja mwanzisha uzi kuhusu Dkt. Chamuriho

Dkt. Chamuriho akielezea ushoroba :

Source : BMG online
 
Sekunde 60 (Sixty Seconds) za Dkt. Leonard M. Chamuriho ktk video clip:

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt .Leornard Chamuriho imetoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya Fidia kwa wakazi wa maeneo yanayopitiwa na mradi wa reli ya kisasa (SGR), ambapo amesema Chuo cha Ardhi kinaendelea na uthamini

That's him, the expert.

Thanks.
 
That's him, the expert.

Thanks.

Hii tabia ya viongozi wetu kugeuka kuwa wakalimani kila wanapotembelewa na wageni wanaoongea lugha ya kigeni kama ktk video clip ya pili huwa inakera.

Huu siyo utaalamu wa negotiation skills bali ni kitu kingine kabisa (ukalimani), viongozi wetu wakitoka kwenye vikao na wageni watumie muda mwingi kuelezea msimamo sahihi wa serikali baada ya mazungumzo.

Maana mara nyingi utasikia wageni wetu wakitoa ufafanuzi baada ya viongozi wetu kupotosha umma!

Hivyo naungana na wachangiaji wengine makini JamiiForums kuwa na wasiwasi na sifa hizo za ziada anazobebeshwa Daktari huyu wa masuala ya ujenzi.
 
Raisi amemsifia mtaalam wa kufanya mazungumzo.

Hatukuwahi kusikia kuwa Tanzania inaweza kuwa na watu ambao wanaweza kukaa meza moja na wazungu na wakazungumza na kikaeleweka.

Au ndugu umewahi kusikia huko nyuma, hebu tupatie ushuhuda.
hatujawahi kusikia kwa sababu hatujawahi kusaini mikataba ya akili...

hata magufuli nae mwongo, anamsifia huyo kwavile katii maagizo yake, aweke mkataba tuuone km kweli una maslahi na sisi........

labda ni maslahi ya magu na watu wake
 
Sasa akionyeshwa kila mtu si itachukua mwaka.

Pili unapaswa kuiamini serikalki yako inayokuwakilisha kwenye masuala mazito yanayohusu nchi kama haya ya miradi mikubwa.
ubongo wako una shida..... bye
 
hatujawahi kusikia kwa sababu hatujawahi kusaini mikataba ya akili...

hata magufuli nae mwongo, anamsifia huyo kwavile katii maagizo yake, aweke mkataba tuuone km kweli una maslahi na sisi........

labda ni maslahi ya magu na watu wake

Nchi gani umeona wanaweka mikataba wazi kwa wananchi wake iwe Ulaya, Marekani au kwingine?

Ukinijibu hili suali utakuwa umewasaidia wengi.
 
Raisi John Magufuli alitoa hotuba ya kuzungumzia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa Stiegler Gorge kwenye mto Rufiji.

Kwenye hafla hiyo Misri wamekuja na wajumbe zaidi ya 100 wakiongozwa na waziri mkuu wao pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Arab Contractors ambao ndo watakaojenga bwawa la Stigler Gorge.

Kwa mujibu wa raisi John Magufuli mwenyewe, mazungumzo kati ya pande mbili za Tanzania na Misri yalikuwa ni mazito na yalochukua muda kuyamalza hadi kufikia makubaliano.

Kwenye mazungumzo hayo Tanzania ilikuwa ikiwakilishwa na ujumbe wa watu wasozidi 15 ambao ni raisi mwenyewe aliwachagua kwa kushirikiana na waziri wa ujenzi.

Mwenyekiti wa timu ya Tanzania ni Dr Leonard Chamuriho ambae ni katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano na uchukuzi.

Ndani ya timu ya Tanzania kuna wajumbe kutoka TANROAD, Tanesco, Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, Hazina, TRA. wizara ya nishati, Ofisi ya raisi (bwana H. Ubwa) na ofisi ya Mazingira.

Hawa ni wataalam wa ujenzi, wataalam wa nishati ya umeme, sheria, usalama, fedha na mazngira.

Lakini mwenyekiti wa timu hii bwana Leonard Chamuriho nde mtaalam wa kufanya mazungumzo yaani Negotiation Expert.

Jambo jingine lilillojenga udadisi ni kusikia kwamba Dr Chamuriho ndie alieshiriki kufanikisha ununuzi na uletwaji wa ndege mpya za ATCL nchini Tanzania.

Pia Dr Chamuriho ameshiriki kwenye mazungumzo ya kujenga reli ya umeme ya Standard Gauge Railways kama mtaalam wa kufanya mazungumzo yaani Negotiation Expert.

NI jambo la kujivunia kuona kwamba nchi yetu inao wataalam ambao wanaweza kufanikisha mambo mengi ya kuleta tija kwa taifa letu.

Ni vizuri nchi yetu inawatunza watu wa aina hii na kuwawezesha kuachia ujuzi wao kwa vizazi vijavyo ili kuiwezesha nchi yetu kufikia kwenye nchi khasa ya asali na maziwa.

Nini maana ya "Negotiation" yaani mazumgumzo baina ya pande mbili?

Hii ni njia ya kufanya nazungumzo maalum ambayo yanalenga kufikia makubaliano ili kuondoa tofauti.

Ni utaratibu ambapo makubaliano au muafaka unafikiwa huku migongano na kutoafikiana vikiondolewa na kisha kusaini makubaliano hayo kisheria mbele ya mashahidi.

Kama hakutakuwa na kukubaliana basi wahusika wa mazungumzo hayo huendelea kufanya vikao kwa malengo ya kufikia muafaka ambao unanufaisha pande zote mbili.

Cha msingi katika kufanya mazungumzo hayo ni kuwepo kwa usawa yaani fairness, kila mmoja kunufaika, na kuendeleza ushirikiano.

Hivyo Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano baina yao na kuhakikisha ujenzi wa bwawa la Stigler Gorge linamalizwa kwa kuda ulokusudiwa.

Utaratibu wa kufanya mazungumzo yaani Process of negotiation.

1. Maandalizi
2. Majadiliano
3. Kutanabaisha malengo ya majadiliano.
4. Kuafikiana kuelekea kila mtu kushinda kwa upande wake yaani "win-win outcome"
5. Makubaliano yaani agreement
6. Utekelezaji wa hatua za makubaliano.

Kuna wakati majadiliano huwa ni aina mbili yaani formal na informal kwamba pande mbili zinaweza kuamu kuzungumzia mambo yanayojadiliwa nje ya vikao au ndani ya vikao au ikawa ni siri kabisa.

Ila inapotokea kunakuwa na kutokukubaliana (suala la Acacia) basi hatua hizo hapo juu katika utaratibu mzima wa mazungumzo zinaachwa pembeni na kunabakia kwenye namba 2 yaani majadiliano ambayi huwezi kuchukua muda mrefu.

Dr Leonard Chamuriho anao ujuzi wa kufanya mazungumzo yaani kwa kiingereza twasema "he has negotiation skills" ambazo ni adimu sana.

Kitendo cha raisi John Magufuli kumtaja bwana Leonard Chamuriho kwamba aliihusika na mazungumzo iya ununuzi wa ndege na pia ujenzi wa reli ya Standard gauge na sasa kuhusika na mazungumzoi ya ujenzi wa hili bwawa na Stigler Gauge, hilo ni jambo jema kwamba nchi yetu inao wataalam.

Ningependa kufahamu je wataalam kama hawa ambao mara nyingi ni wachache kuwa nao hupatikana wapi?

Je, Tanzania inao wataalam wa kutosha wa kufanya mazungumzo kuhusu miradi mikubwa ya serikali?

Je miaka yote hiyo wataalam hawa walikuwa wapi?

Na kama Dr Chamuriho ni katibu mkuu wa wizara kwanini asiwe na ofisi maalum na akawa ana wigo mpana zaidi ambao utamwezesha kuajiri vijana ambao wana utaalam wa kufanya mazungumzo?
Jamaa he is the Best Alikua lecturer kilaka kila course alikua anafundisha pale coet civil Engineering wakati lectures wenzie walikua wanashindwa
 
Hii tabia ya viongozi wetu kugeuka kuwa wakalimani kila wanapotembelewa na wageni wanaoongea lugha ya kigeni kama ktk video clip ya pili huwa inakera.

Huu siyo utaalamu wa negotiation skills bali ni kitu kingine kabisa (ukalimani), viongozi wetu wakitoka kwenye vikao na wageni watumie muda mwingi kuelezea msimamo sahihi wa serikali baada ya mazungumzo.

Maana mara nyingi utasikia wageni wetu wakitoa ufafanuzi baada ya viongozi wetu kupotosha umma!

Hivyo naungana na wachangiaji wengine makini JamiiForums kuwa na wasiwasi na sifa hizo za ziada anazobebeshwa Daktari huyu wa masuala ya ujenzi.

Yaani unabisha kwamba Dr Chamuriho si mtaalam wa kufanya mazungumzo kwa niaba ya serikali, yaani hana negotiation skills?

Hufahamu kwamba negotiation skills zaenda sambamba na communication skills yaani umakini kwenye kutumia lugha khasa ya kiingereza na kujenga hoja na ikakubalika?

Pia unabisha na unasema kwamba hata kwenye ununuzi wa ndege yeye alikuwa ni mkalimani?

Ni kweli kwamba hufahamu wapo wakalimani wa serikali ambapo ukalimani nayo ni taaluma?
 
Hizi sifa za ziada yaani kuwa nguli / uzoefu kazini ktk kushawishi / kuendesha mazungumzo kwa hoja kuhusu mikataba ya kikanda au kimataifa inayoambatana makubaliano ya kimataifa, treaties, sheria kibao n.k hana.

Ila la eneo lake la kufundisha course /degree za structural / civil engineering sifa / uzoefu anazo.
 
Back
Top Bottom