Dkt. Leonard Chamuriho atajwa na Rais kuwa ni mtaalam wa kufanya mazungumzo - "Negotiation Expert". Je, hawa watu tunao wangapi?

Dkt. Leonard Chamuriho atajwa na Rais kuwa ni mtaalam wa kufanya mazungumzo - "Negotiation Expert". Je, hawa watu tunao wangapi?

Hiyo mikataba ingewekwa wazi ndio tungejua kama kafanya poa au katutia hasara tuu, zaidi ya hapo sioni cha kumsifia au kumkataa kwa utendaji wake
Kweli binadam tumepewa ujuzi

Yani mwanadam anahulka ya kuhoji teena kuhoji huko si kuunga mkono bali huwa na hulka ya kudadisi kwa kupinga!!!! Ni vigumu sana na ni wanadam wqchache wanaokuwa tayr ku appreciate kitu!!! Kama huamn ww omba itokee mtu agawe pesa utaona wwnadam watasema huyu jamaa siku hizi kawa kichaa kumbe kasaidia wengne hata hawakuwa na senti mfukoni!
 
Raisi John Magufuli alitoa hotuba ya kuzungumzia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa Stiegler Gorge kwenye mto Rufiji.

Kwenye hafla hiyo Misri wamekuja na wajumbe zaidi ya 100 wakiuongozwa na waziri mkuu wao pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Arab Contractors ambao ndo watakaojenga bwawa la Stigler Gorge.

Kwa mujibu wa raisi John Magufuli mwenyewe, mazungumzo kati ya pande mbili za Tanzania na Misri yalikuwa ni mazito na yalochukua muda kuyamalza hadi kufikia makubaliano.

Kwenye mazungumzo hayo Tanzania ilikuwa ikiwakilishwa na ujumbe wa watu wasozidi 15 ambao ni raisi mwenyewe aliwachagua kwa kushirikiana na waziri wa ujenzi.

Mwenyekiti wa timu ya Tanzania ni Dr Leonard Chamuliho ambae ni katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano na uchukuzi.

Ndani ya timu ya Tanzania kuna wajumbe kutoka TANROAD, Tanesco, Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, Hazina, TRA. wizara ya nishati, Ofisi ya raisi (bwana H. Ubwa) na ofisi ya Mazingira.

Hawa ni wataalam wa ujenzi, wataalam wa nishati ya umeme, sheria, usalama, fedha na mazngira.

Lakini mwenyekiti wa timu hii bwana Leonard Chamuliho nde mtaalam wa kufanya mazungumzo yaani Negotiation Expert.

Jambo jingine lilillojenga udadisi ni kusikia kwamba Dr Chamuliho ndie alieshiriki kufanikisha ununuzi na uletwaji wa ndege mpya za ATCL nchini Tanzania.

Pia Dr Chamuliho ameshiriki kwenye mazungumzo ya kujenga reli ya umeme ya Standard Gauge Railways kama mtaalam wa kufanya mazungumzo yaani Negotiation Expert.

NI jambo la kujivunia kuona kwamba nchi yetu inao wataalam ambao wanaweza kufanikisha mambo mengi ya kuleta tija kwa taifa letu.

Ni vizuri nchi yetu inawatunza watu wa aina hii na kuwawezesha kuachia ujuzi wao kwa vizazi vijavyo ili kuiwezesha nchi yetu kufikia kwenye nchi khasa ya asali na maziwa.

Nini maana ya "Negotiation" yaani mazumgumzo baina ya pande mbili?

Hii ni njia ya kufanya nazungumzo maalum ambayo yanalenga kufikia makubaliano ili kuondoa tofauti.

Ni utaratibu ambapo makubaliano au muafaka unafikiwa huku migongano na kutoafikiana vikiondolewa na kisha kusaini makubaliano hayo kisheria mbele ya mashahidi.

Kama hakutakuwa na kukubaliana basi wahusika wa mazungumzo hayo huendelea kufanya vikao kwa malengo ya kufikia muafaka ambao unanufaisha pande zote mbili.

Cha msingi katika kufanya mazungumzo hayo ni kuwepo kwa usawa yaani fairness, kila mmoja kunufaika, na kuendeleza ushirikiano.

Hivyo Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano baina yao na kuhakikisha ujenzi wa bwawa la Stigler Gorge linamalizwa kwa kuda ulokusudiwa.

Utaratibu wa kufanya mazungumzo yaani Process of negotiation.

1. Maandalizi
2. Majadiliano
3. Kutanabaisha malengo ya majadiliano.
4. Kuafikiana kuelekea kila mtu kushinda kwa upande wake yaani "win-win outcome"
5. Makubaliano yaani agreement
6. Utekelezaji wa hatua za makubaliano.

Kuna wakati majadiliano huwa ni aina mbili yaani formal na informal kwamba pande mbili zinaweza kuamu kuzungumzia mambo yanayojadiliwa nje ya vikao au ndani ya vikao au ikawa ni siri kabisa.

Ila inapotokea kunakuwa na kutokukubaliana (suala la Acacia) basi hatua hizo hapo juu katika utaratibu mzima wa mazungumzo zinaachwa pembeni na kunabakia kwenye namba 2 yaani majadiliano ambayi huwezi kuchukua muda mrefu.

Dr Leonard Chamuliho anao ujuzi wa kufanya mazungumzo yaani kwa kiingereza twasema "he has negotiation skills" ambazo ni adimu sana.

Kitendo cha raisi John Magufuli kumtaja bwana Leonard Chamuliho kwamba aliihusika na mazungumzo iya ununuzi wa ndege na pia ujenzi wa reli ya Standard gauge na sasa kuhusika na mazungumzoi ya ujenzi wa hili bwawa na Stigler Gauge, hilo ni jambo jema kwamba nchi yetu inao wataalam.

Ningependa kufahamu je wataalam kama hawa ambao mara nyingi ni wachache kuwa nao hupatikana wapi?

Je, Tanzania inao wataalam wa kutosha wa kufanya mazungumzo kuhusu miradi mikubwa ya serikali?

Je miaka yote hiyo wataalam hawa walikuwa wapi?

Na kama Dr Chamuliho ni katibu mkuu wa wizara kwanini asiwe na ofisi maalum na akawa ana wigo mpana zaidi ambao utamwezesha kuajiri vijana ambao wana utaalam wa kufanya mazungumzo?
Ondoa huu upuuzi ! Miradi yote Tanzania kulikuwa na majadiliano na bado tukaingia mikataba mavi
 
Weka na mikataba tusome ndugu
Huwa najiuliza mda mwngne asili ya wanajf!!

Hv ushawahi ona wapi mikataba inasiniwa wazi yaani nchi mbili zinazosaini mkataba tena mwananchi nae anapewa wasaa wa kuona kinachisainiwa???? Hivi tunajua maana ya kuwa na viongozi???? Tunajua Rais ni nani na yuko pale kivipi??? Je mawaziri ni kina nani???? Yaani unashndwa kujiuliza swali kwamba hv kwann sheria zinazopitishwa na bunge Letu wananchi huwa hawapewi wasaa wa kuzisoma!????

Kama kuna nchi ushawahi ona inasini mikataba hii kwa uwazi na mwanachi wa kawaidia akashuhudia naomba uzitaje!!!!
 
Ijadilini bungeni ipitiwe basi

Ova
 
Utaalamu wa kuzungumza unakuja pale tu unapokuwa very well conversant na subject matter. Dr. Chamuriho ni jembe na wote waliopita Faculty of Engineering - Civil (FoE) pale UDSM hawatabisha. Sasa peleka vilaza kama Kibajaji, Polepole au Mzee Makamba senior na "utaalamu wao wa kupiga domo" kwenye hizo negotiations uone muziki wake.
 
Npe mfano wa nchi zinzosaini mikataba wazi yaani na wanachi wakihusishwa
Jibu swali!mbn mikataba sahv bunge halishirikishwi .....jumba jeupe wao wanaingia
Wenyewe juu kwa juu au hilo kisheria linaruhusiwa ....

Ova
 
Jibu swali!mbn mikataba sahv bunge halishirikishwi .....jumba jeupe wao wanaingia
Wenyewe juu kwa juu au hilo kisheria linaruhusiwa ....

Ova
Hujielewi ww!?? Yaani niulize swali awali ujibu kwa kuniuliza swali halafu ww ukose haki ya kunijb mie ndo nkujibu

Ona haya basi
 
Kweli binadam tumepewa ujuzi

Yani mwanadam anahulka ya kuhoji teena kuhoji huko si kuunga mkono bali huwa na hulka ya kudadisi kwa kupinga!!!! Ni vigumu sana na ni wanadam wqchache wanaokuwa tayr ku appreciate kitu!!! Kama huamn ww omba itokee mtu agawe pesa utaona wwnadam watasema huyu jamaa siku hizi kawa kichaa kumbe kasaidia wengne hata hawakuwa na senti mfukoni!
Sijaona Logic ya ulichoandika Mkuu au sijakuelewa, mada inataka kumsifia mtu kuhusiana na utendaji wake katika sehemu fulani lakini tunachohoji ni kuona weledi kazi aliyofanya maana historia inawahukumu sana viongozi wetu miaka yote tunasikia hawa mabepari wametuibia sana lakini tulikuwa nao kwenye meza ya majadiliano kabla ya kuwaruhusu kuanza kufanya kazi au uwekezaji katika taifa letu. Lengo sio kupinga ni kutaka kuona mambo yakienda sawa kwa uwazi mwisho wa siku hili ni taifa letu sote wote tunataka matokeo chanya.
 
Sasa umeona wapi serikali mbili zinasaini mkataba na wewe mwananchi wa kawaida unapewa nakala usome?

Nambie ni nchi gani hiyo tukaitembelee tujifunze kitu?
Hatuwezi kuwa wa kwanza?
 
Huwa najiuliza mda mwngne asili ya wanajf!!

Hv ushawahi ona wapi mikataba inasiniwa wazi yaani nchi mbili zinazosaini mkataba tena mwananchi nae anapewa wasaa wa kuona kinachisainiwa???? Hivi tunajua maana ya kuwa na viongozi???? Tunajua Rais ni nani na yuko pale kivipi??? Je mawaziri ni kina nani???? Yaani unashndwa kujiuliza swali kwamba hv kwann sheria zinazopitishwa na bunge Letu wananchi huwa hawapewi wasaa wa kuzisoma!????

Kama kuna nchi ushawahi ona inasini mikataba hii kwa uwazi na mwanachi wa kawaidia akashuhudia naomba uzitaje!!!!
Ndugu sio ugomvi upo kwenye kuelimisha na hili ni jukwaa huru weka basi haya bei ya ndege tulionunua kwa kupunguziwa kwa sababu tuna MTU mwenye kujua kuongea vizuri na hayo makampuni
 
Hakuwa anafundisha pekee!
Alikua BICO, wanafanya ushauri elekezi.
Pia alikua NCC.....
BTW: Sijasema lolote kuhusu uwezo wake, natoa facts nazozijua kumhusu.

amebobea wapi sasa huyo ni sawa tu na wale maphd wengine kufundisha udsm sio uexpert ni narudio ya tu unalichosomea kila siku kwa wanafunzi ndo maana mohd wengi wamechemka
 
Kama kawaida yetu kipindi cha makinikia tuliambiwa sisi tupo wachache wao wapo wengi na sisi tumeshinda na wanatulipa [emoji23][emoji23][emoji23] ila mpk leo sijui wameanza kulipwa wakazi wa dsm Noah zao sisi huku mikoani tusubirie kidogo
 
Kwani mikataba mingine ya hovyo ambayo taifa ilikua inaingia nani alikua kwenye nafasi kama ya jamaa huyu unayomzungumzia kwa sababu kama tunafanya appreciation kwa Nazi nzuri tuone pia na majina ya wapumbavu
 
Back
Top Bottom