Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lakini hajawahi kuzungumzia mambo ya siasa usijaribu kumgombanisha na nguvu ya umma yakeDr. Shika mda sio mrefu mtasikia amejiunga na ccm
Shuka la kimasai = 10,000/= sio 1,000/=1000 × 4000 = 4,000,000
WanaJamiiForums habari za mchana,
Yule Daktari bilionea maarufu nchini kwa sasa ameonekana wilayani Kahama akiwa ni mgeni maalumu katika uzinduzi wa chuo hicho ambao unafanyika leo..
Picha zaidi nitatupia .
![]()
![]()
![]()
View attachment 636292 View attachment 636293
Bilionea Dkt. Louis Shika ambaye amejizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania baada ya kuibuka katika mnada wa kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi ametua leo alhamisi Novemba 23, 2017 mjini Kahama kwenda kuhudhuria katika mahafali katika chuo cha Afya cha (Kahama College of Health Science).
View attachment 636684
Dkt. Louis Shika akiwa katika matukio ya upigaji picha na wahitimu chuoni hapo.
Dkt. Shika akitoa hotuba kwenye sherehe za mahafali mbele ya wahitimu amesema anatambua kuwa masomo ya sayansi hususani ya Afya karo yake ni ghali hivyo ameahidi kuwalipia karo wanafunzi wote watakaofanya vizuri kwenye masomo yao chuoni hapo.
“Natambua umuhimu wa masomo ya afya na ughari wa malipo yake kwa Watanzania wenye kipato cha chini, nitawalipia wanafunzi wote wenye uwezo darasani ambao wazazi au walezi wao hawana uwezo wa kugharamia masomo yao.“ amesema Dkt. Shika wakati akitoa hotuba yake kwenye mahafali chuoni hapo.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Chuo hicho, Yona Bakungile ameeleza sababu za kumualika Dkt. Shika katika Chuo chake kuwa ni kutokana na utaalamu wake wa masuala ya tiba ya binadamu na umaarufu wake unaoendelea kuvuma nchini.
“Chuo changu kinatoa mafunzo ya afya ya binadamu; licha ya umaarufu wake nchini kwa sasa, Dk Shika ni miongoni mwa wataalamu katika fani ya utabibu ndiyo maana nimemwalika. Naamini atawashauri na kuwapa hamasa wahitimu na wanafunzi wanaoendelea,” amesema Bakungile kwenye mahojiano yake na gazeti la Mwananchi.
Sharti la mualiko lilikua ni kwamba......Ina maana shati, suruali na tai alivyovaa siku ya mnada pamoja na pozi la picha havibadiliki?
Na hilo ndilo hasa lilikua lengo kuu la kumualika Dr Shika...Wanaopondea Dr shika kualikwa kwenye hiyo mahafali hawana akili?angalia tu hapa hii thread inavyojadiliwa na watu wengi,kwenye social media zote hiko chuo kimepata free publicity kabisa,kimejulikana nchi nzima leo.
Mkuu...kwa mambo kama haya ndipo utapogundua ni jinsi gani itakuwa vigumu kwa Watanzania kumng'oa mkoloni mweusi CCM.
ni nchi iliyosheheni a bunch of jokers.... CCM wanalijua hili na wana-capitalize kisawasawa.
kuing'oa CCM kunahitaji watu wachache wajitoe ufahamu halafu.......bang!
kama Zimbabwe vile. nani alitegemea Mugabe angeondoka madarakani leo kama si kwa watu wachache kujitoa ufahamu??
Mpaka waujuwe ushamba wa Wasukuma! Wao wanapiga hela tu, kilaini, kiakili, kisheria, watake wasitake watashikwa tu..Acha Mungu amrudishie miaka na yote yaliyoliwa na parare, madumadu, na nzige maishani mwake. Dr. Shika, piga hela mjomba. Awamu hii ni ya kanda ya ziwa hakiya nani!!!
Hiyo ndio brand yake mkuuIna maana shati, suruali na tai alivyovaa siku ya mnada pamoja na pozi la picha havibadiliki?
DR. SHIKA FOR PRESDENCY
Yap, bila kusahau kabahasha na tu Sandals...Ina maana shati, suruali na tai alivyovaa siku ya mnada pamoja na pozi la picha havibadiliki?
We jamaa umenichekesha sanaDr. Shika hata kama alikuwa hana hela ila sasa anaanza kupiga hela kwenye age ya 50+ to 60+ kweli hela na utajiri hauna formula maishani.
Life starts at 40s inatimia kwa Dr. Shika.