Uchaguzi 2020 Dkt. Lwaitama atabiri mshindi Uchaguzi Mkuu 2020

Uchaguzi 2020 Dkt. Lwaitama atabiri mshindi Uchaguzi Mkuu 2020

Bernard Membe atapunguza kura za CCM Mpya na Siyo zile za CHADEMA.- Mwalimu A. Lwaitama.
Huu ni ukweli usio na mashaka. Hakuna mpinzani wa kumpa kura BM lakini wale maccm aliotoka nao kule wapo watakaompa hadharani na hata mafichoni.
 
25 Agosti 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Live : Ofisi ya Mkurugenzi kurudisha fomu, wafuasi wa CHADEMA na CCM watambiana

Wafuasi wa vyama hivyo viwili wakutana wakati wa kurudisha fomu na hali imechangamka kwa tambo zao
 
Huyu mzee hana lolote ana tabia ya kujitekenya mwenyewe na anacheka
 
Haka kazeee ni kanafiki kweli,
Atueleze kwanza hapo alipofikia amefanya kitu gani cha kuishangaza dunia au nchi yake kama siyo unafiki wa kujipendekeza kwa wazungu
Amekuwa mpigania haki wa kweli ambae amejitolea kwa kila kitu pamoja na maisha yake.
 
Tutafakari mfano wa Afrika Kusini na Chama cha ANC.
Je kilikuwa na pesa za kusimamia uchaguzi?
Je Makaburu hawakuiendeleza Afrika Kusini kuliko Tulivyoiendeleza Tanzania ndani ya miaka 5?
Je kila siku kumweleza Mwanainchi kuwa nimekufanyia jambo moja , mbili, tatu na kuendelea si Kumsimanga. Mila na Desturi za Mwafrika haziruhusu kutangaza jambo ulilomsaidia mwenzako,
Yeye aliyesaidiwa ndiye anatakiwa kulitangaza.
Yesu Kristo alipokuwa anawaponya watu, aliwaambia baada ya kuwaponya, enendeni zenu msimwambie mtu. Alijua vipofu ni wengi na yeye hawezi kufanya miujiza kila siku. Alifanya hivyo ili watu wamwamini.
Yesu Kristo hakutaka kutangaza alichowafanyia watu na hata hakuwaruhusu wale waliowaponya kutangaza. Lakini aliyoyafanya Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita, yote tunayajua hadi leo.
Hata Hayati Mwalimu Nyerere hakuwa anahubiri aliyowafanyia Wanainchi kwa sababu alikuwa anajua ni wajibu wake na wanainchi walikuwa wanajua alichowafanyia. Pia walikuwa bado na matatizo mengine mengi.
Si vyema sana kutangaza kila kitu unachofanya kwa watu kwa sababu si wote unaweza kuwatendea hivyo.
Unawapa uchungu wale ambao hujawafanyia na pengine ndiyo walio wengi.
Mwalimu Nyerere alikuwa anaongea maendeleo ya Inchi kulingana na aina ya watu anaongea nao.
Akifika kwa wakulima ataongea mambo ya Kilimo. Mambo ya Railway line ya Standard gage, Umeme wa Stirgers Gauge, au Ndege wanakuwa hawaelewi kabisa. Ni sawa na kumfundisha Mtoto wa shule ya Msingi elimu ya chuo Kikuu.
Unaweza kumpa mtu keki ukafikiri umemsaidia sana kumbe yeye alikuwa anataka ugali na mchuzi wa samaki na Nazi.
Unaweza kumpa mtu pilau lakini kumbe yeye alikuwa anatamani Bia.
Mwisho.
Ukiwa na Mtoto mdogo jifafanye na wewe ni Mtoto.
Ukiwa na Mkulima, Jifanye na wewe ni mkulima.
Ukiwa na mfanya Biashara, jifanyanye na wewe ni mfanya biashara.
Ukiwa na kiongozi wa Dini nawe jifanye ni muumini mzuri.
Siku zote tujifanye wadogo kuliko wale tunaowaongoza.
AMEN
 
Bernard Membe atapunguza kura za CCM Mpya na Siyo zile za CHADEMA.- Mwl. A. Lwaitama.

ukiskiliza hii video utajua mshindi ni nan na atashinda kwa asilimia ngap


lakini pia ukiongeza na hizi video utajua asilimia ztachezea ngap


ongeza na hizi


lalafu fuatilia coments kwenye live talks za magufuli na lissu, then mwisho kabisa nenda mtaani fanya research apo sasa utajua mshindi nan,
 
25 Agosti 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Live : Ofisi ya Mkurugenzi kurudisha fomu, wafuasi wa CHADEMA na CCM watambiana

Wafuasi wa vyama hivyo viwili wakutana wakati wa kurudisha fomu na hali imechangamka kwa tambo zao

Hapo hakuna vyombo dola wala maelekezo hali ni shwari.
 
24 Agosti 2020

Katika mahojiano maalum Mwanzuoni wa masuala ya binadamu, mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha UDSM mwalimu Dr. Azavery Lwaitama amesema anaufuatilia michakato uchaguzi wa Oktoba 2020 kwa ukaribu



Tukio la uchaguzi wa 2020 ni kuthibitisha wananchi ndiyo watawala halisi wa nchi hii Tanzania na siyo Bunge, wala taasisi ya uRais, udiwani. Hilo ni muhimu waTanzania wapiga kura kutambua ni watu-huru na wasisahau kuwa tukio la Oktoba watambue wasiuze uhuru wao kwa wagombea wanaopenda kutawala badala ya kuongoza.

Hivyo wapiga kura wawe makini kuchagua wagombea ambayo hawatajitwalia madaraka ya kuwaswaga wananchi kwa kigezo cha kuchaguliwa kwa kura.

Tukio la kupiga kura kisigeuzwe kuwa ni maridhiano ya kuuza uhuru na utu wao ili watawaliwe kwa miaka mitano bila uhuru au sauti ya kuwakosoa au kushirikishwa ktk maamuzi na wanasiasa watakaokuwa wameingia madarakani ktk serikali, bungeni au ktk mabaraza ya madiwani.

Tofauti za Mvuto wa wagombea katika uchaguzi wa Oktoba 2020 kutafuta wadhamini, hivyo wapiga kura Watanzania wanahisia gani kwa wagombea wanaotafuta udhamini na wale wa kimya kimya waliopitishwa na vyama wanavyovipenda na kuviamini vyama vyao.

Chama cha ANC cha Afrika ya Kusini kilipigwa marufuku na makaburu kwa muda mrefu lakini ANC walikuja kuibuka washindi huku Mandela mbali ya kuweko nje ya siasa kwa miaka 27 alichaguliwa kuwa Rais na pia ANC chama kilichopigwa marufuku ya siasa kilipata wabunge wengi. Uchaguzi huo wa kihistoria wa mwaka 1994 baada ya ubaguzi kuondolewa ulihusisha vyama 19 vya siasa nchi Afrika ya Kusini ANC, PAC, NP na :



Historia katika Sayansi ya Siasa ( Political Science) inaonesha vyama vinavyofungiwa kufanya siasa vina uwezekano wa kuibuka washindi kushika dola kupitia uchaguzi huru na wa haki.

Chama kilichopo madarakani kina fursa kutumia walichofanya kwa wananchi kushinda uchaguzi.

Lakini katika siasa chochote kinaweza kutokea bila kujali chama kilikuwa madarakani au katika katazo la kufanya siasa kushinda.

Ngazi ya ki-urais katika kuwania nafasi ya urais hata wakijitokeza watu 100 historia huonesha ni watu wawili tu ndiyo watakuwa wanachuana vikali.

Na mpaka sasa inaonesha uchaguzi wa mwaka huu utakuwa ngumu na matokeo ya kustaajabisha sana anamalizi mwanazuoni huyu mahiri aliye mtu-huru katika uchambuzi wake wa eneo lake la taalumu ya uchambuzi wa tabia za binadamu na leo ameangazia eneo la siasa na chaguzi.

SOURCE: MwanaHalisi TV

Hivi mlezi wa Chama ulitaka atoe tathmini gani? Mbona mnajidanganya namna hii?
 
ukiskiliza hii video utajua mshindi ni nan na atashinda kwa asilimia ngap


lakini pia ukiongeza na hizi video utajua asilimia ztachezea ngap


ongeza na hizi


lalafu fuatilia coments kwenye live talks za magufuli na lissu, then mwisho kabisa nenda mtaani fanya research apo sasa utajua mshindi nan,

Staki kukuharibia jioni yako. Lissu hawezi kuwa rais kwa NEC hii mbona hamtaki kuelewa?
 
Hivi mlezi wa Chama ulitaka atoe tathmini gani? Mbona mnajidanganya namna hii?

Hapa alikuwa anatoa maoni kama mwanazuoni , hivyo ulezi aliuweka pembeni ni kawaida ya wasomi kutoa tathmini kwa kujitoa ktk ushabiki.
 
Hapa alikuwa anatoa maoni kama mwanazuoni , hivyo ulezi aliuweka pembeni ni kawaida ya wasomi kutoa tathmini kwa kujitoa ktk ushabiki.
Acha kuwa na akili kama ya mtoto. Hizi siasa za partisanship za Tanzania wanazuoni wamegeuka kama mizoga. Huyu jamaa kawa partisan muda mrefu kama wenzake kina Kabudi. Danganya wenzio wa CDM ama CCM wenye mawazo kama ya kina Lwaitama na Kabudi siyo sisi tunaojielewa na hatukufunikwa na u chama
 
Historia katika Sayansi ya Siasa ( Political Science) inaonesha vyama vinavyofungiwa kufanya siasa vina uwezekano wa kuibuka washindi kushika dola kupitia uchaguzi huru na wa haki.
 
Acha kuwa na akili kama ya mtoto. Hizi siasa za partisanship za Tanzania wanazuoni wamegeuka kama mizoga. Huyu jamaa kawa partisan muda mrefu kama wenzake kina Kabudi. Danganya wenzio wa CDM ama CCM wenye mawazo kama ya kina Lwaitama na Kabudi siyo sisi tunaojielewa na hatukufunikwa na u chama

Huyu ame declare kabisa kuwa anachambua facts na historia, siyo mawazo ya kikamanda au kikada.

Kubali kusikiliza facts, data na historia weka uchama pembeni utamuelewa anachoongea.
 
Twende LISSU, twende baba, vijana tupo na wewe.

Naona kila Mtanzania taratiiibu wameanza kuonyesha nyuso za furaha kwa kukukubali.
Wadau mpaka sasa nasikia| mpaka sasa CCM imeshachukua majimbo nane, namaanisha wamepita bila kupingwa. Yaani kabla ya hata ya kitufe kubonyezwa majimbo yafuatayo wapinzani wamenyanyua mikono na CCM wanayachukua labda wagombea waage dunia.

1.Misungwi,
2.Ruangwa,
3.Ushetu,
4.Morogoro Mjini,
5.Mvomero,
6.Kilosa,
7.Mtama,
8. Gairo

Karibuni tuweke kumbukumbu za clean sheets hapa.
 
Mbio za kuwania urais 2020 utakuwa baina ya farasi wawili, wengine watakuwa wasindikizaji.
 
25 Agosti 2020
Dodoma, Tanzania

RAIS MAGUFULI ARUDISHA FOMU NEC, APITISHWA KUGOMBEA 2020



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, amerudisha fomu ya kugombea Urais katika Ofisi NEC Jijini Dodoma, Ambapo baada ya kukabidhi fomu hizo Tume ya Uchaguzi NEC imeelezwa kuridhishwa na Nae yeye pamoja na Mgombea Mwenzake ambaye ni Mama Samia Suluhu.
 
Back
Top Bottom