Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli akishinda, Afrika imeshinda

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli akishinda, Afrika imeshinda

Hatuwezi kuweka nchi Rehani kwa kumchagua wakala wa mabeberu, Tunapiga kura kizalendo ili kulinda Uhuru wetu, amani yetu na Rasilimali zetu. Piga kura kizalendo uwaaibishe mabeberu na mawakala wao.
 
Walioshinda ni watawala na familia zao wanaomiliki mabilion ya pesa na Mali zenye thamani ya matrion katika nchi maskini.

Ndio maana kila MTU anajipendekeza ili apate uteuzi.
Pato la taifa linawanufaisha moja kwa moja watawala mifukoni mwao huku wakishika miradi mikubwa kwa fedha keshi ili kuwanufaisha watu wao wa Karibu.

Wao wanakuambia kuwa watanufaika wajukuu zako lakini wao na watoto wao na wake zao na wajomba zao wananufaika Leo.
Tafakari !!
Serikali ya awamu ya tano imekunifaisha we we, familiya yako na ukoo mzima kupitia Elimu bure, huduma bora za afya, mikopo elimu ya juu, usafiri bora, ulinzi, usalama na amani n.k. chagua Magufuli, Chagua Maendeleo
 
Mitano tena tumalizie kazi. Nondo na simenti zitashuka bei, matundu ya choo na madarasa yataongezeka, miradi ya maji wakandarasi wapo kazini.
Piga kura kizalendo, Maisha mazuri yapo kwa JPM, kataa ushoga na ubeberu
 
Unawajua mabeberu lakini. Wakituwekea sanctions ya mwezi mmoja tu inatosha kutuadhibu. Nenda Zimbabwe ukawaangalie wanavyoteseka kwa ajili ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi. ZANU PF wao wapo tu wakitumia dola kubaki madarakani lakini raia wa kawaida awe wa chama gani wanateseka sana. Hii pia ya rais wetu kutokuwana na uhusiano mzuri nao na kuendelea kuwaita mabeberu wanaweza wakatufanyia figsu na uchumi wetu ukaporomoka.

Zimbabwe baada ya kuwekewa vikwazo waliangalia China kama option B. Kumbe China ni zaidi ya mabeberu. Wamepewa migodi ya dhahabu na wanachofanya ni kuondosha mali tu na kuwafunga macho viongozi wakubwa. Hii ndiyo maana anamwambia USA wasiingilie uchaguzi wanajua wanachofanya. Wanajua mambo yakishakuwa magumu tutawageukia wao kuwaomba misaada na hapo ndiyo kuanza kugawana nchi na wao.
 
Piga kura kizalendo kama unayajua hayo, JPM ni alama ya Uhuru, Amani, Uzalendo na Uafrika.
Acha kufananisha Africa na vitu vya kijinga
JPM ni jembe LA Afrika, Ulaya wanatambua Afrika INA Rais mmoja tu, JPM
Unawajua mabeberu lakini. Wakituwekea sanctions ya mwezi mmoja tu inatosha kutuadhibu. Nenda Zimbabwe ukawaangalie wanavyoteseka kwa ajili ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi. ZANU PF wao wapo tu wakitumia dola kubaki madarakani lakini raia wa kawaida awe wa chama gani wanateseka sana. Hii pia ya rais wetu kutokuwana na uhusiano mzuri nao na kuendelea kuwaita mabeberu wanaweza wakatufanyia figsu na uchumi wetu ukaporomoka. Zimbabwe baada ya kuwekewa vikwazo waliangalia China kama option B. Kumbe China ni zaidi ya mabeberu. Wamepewa migodi ya dhahabu na wanachofanya ni kuondosha mali tu na kuwafunga macho viongozi wakubwa. Hii ndiyo maana anamwambia USA wasiingilie uchaguzi wanajua wanachofanya. Wanajua mambo yakishakuwa magumu tutawageukia wao kuwaomba misaada na hapo ndiyo kuanza kugawana nchi na wao.
 
Humu JF kuna team ya wanafiki mmejaa humu kujibu kila Comment.... vijana tuache kuendekeza njaa!

Hivi kama kweli anajiamini kwanini atuzimie mitandao ya kijamii?? Au mnaamini kila mtu ni mpenda siasa?
Kilaaniwe kizazi chenu wote mnaoendeleza haya yote.

Huu upuuzi wenu unaanza kutugusa hadi sisi ambao tumejiweka kando na vichwa panzi nyie
Hiyo laana na ikurudie wewe mwenyewe wala isiguse vizazi vyako, mpaka useme poo ktk jina la Yesu amen🙏!
 
Kwanza kwanini MATAGA wako online??? Inamaana waliamini maneno ya kaka kigogo wakadownload na wao??? Wanafiki sana madogo hawa
Akili yako ndio imeishia hapo tu😂😂😂😂😂😂😂!
Tz na JPM, 5 Tena!
 
Humu JF kuna team ya wanafiki mmejaa humu kujibu kila Comment.... vijana tuache kuendekeza njaa!

Hivi kama kweli anajiamini kwanini atuzimie mitandao ya kijamii?? Au mnaamini kila mtu ni mpenda siasa?
Kilaaniwe kizazi chenu wote mnaoendeleza haya yote.

Huu upuuzi wenu unaanza kutugusa hadi sisi ambao tumejiweka kando na vichwa panzi nyie
Ameen, kilaaniwe kabisa.
 
Mnamo mwaka 2015 JPM alijipigia chapuo sana kuwa ni Rais wa wanyonge. Sikuelewa sana, nikasema ngoja nijipe muda nione.

Baada ya mwaka mmoja tu nikaona dalili za wanyonge kuumizwa sana, huku akidai ananyoosha nchi. Sikuelewa!

Hapa chini nakudadavulia mambo ambayo yanaonesha JPM alivyowafukarisha hoi bin taaban hata wale waliokuwa nacho kidogo.

1. Aliongeza makato ya bodi ya mikopo (HESLB) kutoka 8% hadi 15% kila mwezi
Mshahara hajaongeza hata tone, anadai anajenga reli, na kununua ndege. Hivi jamani, Rais hujaongeza mshahara wa mtumishi, unaongeza vipi makato? Naombeni mnisaidie kushangaa! Mshahara hutaki kuongeza, bado unawaongezea makato kweli?

Chini ya JPM, aliyekuwa anapokea laki 3, kwa makato haya amefanywa kupokea laki 1 na pointi.

(maskini amekuwa fukara, hoi bin taaban).

2. Alipandisha kilo ya sukari kutoka 1,800/- ya jk hadi sh. 2,500/- au zaidi
Wananchi wakiwa wanyonge vile vile kaingia kazuia kuingizwa sukari, bila hesabu wala maarifa. Matokeo yake sukari ikapungua, bei ikashuti. Kaanza kukimbizana na watu ma-godown huko. Ovyo kabisa!

Mwisho wa siku anatangaza eti bei elekezi eti sh. 2,500/- Nisaidieni kushangaa!

Hivi umekuta bei 1,800/- kwa kg, yeye jpm miaka miwili tu ikawa mara mbili sh. 3,000/-

Yani iko hivi hela ambayo maskini alikuwa ananunua kg 2, leo ananunua kg 1 tu imeisha.

(waliokuwa maskini amewafanya mafukara, hoi bin taaban)

3. Alizuia minada ya mazao kama mbaazi, korosho, ufuta n.k.
Akawapekekea jeshi watu wa kusini kuchukua korosho zao. Matokeo yake, bei ya mbaazi ikashuka kutoka sh 1500/- kwa kg hadi sh. 200/- kwa kg zikakosa wanunuzi, hasara kwa maskini.

Korosho zilivyobebwa hakuna ajuaye. Jeshi kwenye mambo ya kiraia, huwezi kuhoji. Wengine wakaishia kuambiwa korosho zao zilikuwa eti mbovu. Mpaka leo hawana kitu. Hawana hela na uendelezaji wa mashamba msimu mpya umekuwa mgumu.

(maskini mkulima amefanywa fukara, hoi bin taaban)

4. Bomoa bomoa ya nyumba DSM (Kimara), na huko Moro bila fidia kwa sheria ya mwaka 1938/50.
Huyu JPM aliacha sheria za miaka ya 80, za road reserve kuwa mita 60. Akachukua sheria ya kikoloni road reserve mita 120.

Kabomoa mpaka ambako barabara haitapita. Waliokuwa na nyumba, wakabaki nje na maskini hatari. Kwa maisha yale yale

(maskini akafanywa, fukara hoi bin taaban)

5. Hatoi ajira
Toka ameingia madarakani ni madaktari elfu 3 na ushee na walimu baadhi wa sayansi ndio waliajiriwa.

Yani mzazi kasomesha mtoto, kwa kujikamua, enzi za jk walimu walikuwa hawaombi ajira, ilikuwa ukimaliza ualimu degree, au cheti/diploma, unasubiri kupangiwa kituo. Ukatae mwenyewe kazi. Ila leo soma, maliza ng'ombe za wazazi, na kazi JPM hatoi.

(maskini amekuwa fukara zaidi, hoi bin taaban)

6. Hakuwajengea walioharibikiwa nyumba na tetemeko la Kagera pamoja na kukusanya michango kila pembe ya dunia.
Maskini wa Kagera, akaambiwa hajaletewa tetemeko.

(maskini akawa fukara, hoi bin taaban)

7. Kikokotoo cha pensheni ya wastaafu.
Akaleta kikotoo eti ukistaafu zile hela ulizohifadhi, upewe kiduchu. Yani ufanye kazi miaka 60, uzeeke. Wkt unataka hela yako, jpm anasema chukua kiduchu. Huko nyuma wastaafu walikuwa wanapewa mara moja 75% ya hela , yeye akasema wapewe 25% tu.

(hapa maskini mstaafu anapunguziwa hata jasho lake la kwenda kupumzikia). Fukara, hoi bin taaban.

8. Kahawa huko kagera alikuta wanauza kilo 2500/-, kazuia wa Uganda wasije kuinunua. Ikashuka bei hadi sh 1000/-

Maskini akawa fukara zaidi, hoi bin taaban chini ya JPM.

Kwa ufupi:
Wakulima hoi bin taaban
Wafanyakazi hoi bin taaban
Wastaafu hoi bin taaban
Waliomaliza vyuo hoi bin taaban
Wafanyabiashara hoi bin taaban
Wavuvi hoi bin taaban

Eti huyu anataka mi5 tena!! Afanye nini?

Huyu ni rais wa wanyonge gani?

Ongezea wengine walio hoi bin taaban

TUNDU LISSU FOR PRESIDENT
 
Back
Top Bottom