Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli akishinda, Afrika imeshinda

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli akishinda, Afrika imeshinda

Uchaguzi wa amani upo huru sijasikia mtu akisema haoni jina
 
Magufuli anashinda tena mapema sana.RAIS NI MAGUFULI. huyo mwingine cjui hata kura kapigia wapi
 
Umesahau haya,ameboresha mauaji,utekaji,uharamia na dhuluma pamoja na ukandamizaji wa haki za raia,pamoja na ukandamizaji wa media,na demokrasia,Hali za wananchi kuamua kuongozwa na nani,na kuliondoshea bunge maamuzi yake,kwa kuliteka vile vile,Kama ilivyo tabia yake,kuwagawa watanzania.
 
Nimefurahi mwitikio wa watu kituoni ulikua mzuri sana, amani tele, kwenye foleni wazee, wajawazito, wamama wenye watoto na wanawake kwa ujumla tumepewa kipaumbele👍

Sasa nikiwa natoka kwenye kura nikapita dukani nimekuta vijana 7 wenye afya na makeke ya kutoshaa. Nikaagiza mahitaji yangu wakaniambia dada wewe tayari nikawaambia ndio. Nikauliza nyie mshapiga? Wakatazamana kwa aibu kisha wakaniambia tumepiga mapema kabisaa...ila hakuna mwenye wino kidoleni. Nijua wazi hawa ndio waleee waliogoma kujiandikisha.... Tundu wanamtaka kura hawapigi!

Wakaniuliza wewe umempa nani nikawajibu si anajulikana tunaempa😁😁 wakafurahiii wakaniambia niYeYe😂😂 nikawaambia ni yuleyule😁😁😁 majibu jioni

Nikiwa naondoka nikakutana na wamasai wamekaa kikundi wanasema nataka Tundu Lissu nikawaambia wahi kituoni mmoja akanijibu hamna kitambulisho

Nimejifunza vijana wengi wa upinzani hawajui umuhimu wao kwenye kura ila ni wa kwanza kwenda kwenye mikutano. Vyama vya upinzani hawana connection na watu wao sababu vyama vyao havina dira, hawaijui kesho yao itakuaje kwa hiyo huwa hawana mipango.

Na ndio maana hadi leo hata wale wachache watakaokua wamawapigia hawajui urais wampe membe au Tundu. Pole wapinzani, chama kushika dola inahitaji viongozi kujitoa sana kujijenga
 
AF64D638-DA9E-4F7D-81C6-36BD15D33DFE.jpeg
 
Serikali ya awamu ya tano imekunifaisha we we, familiya yako na ukoo mzima kupitia Elimu bure, huduma bora za afya, mikopo elimu ya juu, usafiri bora, ulinzi, usalama na amani n.k. chagua Magufuli, Chagua Maendeleo
Faida zipo kama kwa matajiri na watu wenye uchumi wa kati zaidi :-

Watoto Wa Maskini :
Ada shule ya Msingi = 0
Ada Sekondari = 0
Ada Ngazi ya Cheti = 1200,000/-
Ada ngazi ya Diploma = 180,0000/
Ada ngazi ya digrii - Mkopo 40% ajira hakuna.
 
Nakubaliana 100%. Tayari katika familia yangu na ukoo wetu ameshashinda kwani mapema asubuhi tumeenda kumshindisha.

Tunasubiri waTanzania wazalendo tuungane.
 
Sawa amefanya mazuri lakini watanzania wote hawamtaki, si apumzike tu, Nyerere walimtaka lakini alikataa. yeye hawamtaki lakini anataka jamani!!!
 
Naunga mkono hoja Africa ina wazalendo wachache sana moja ya hao wazalendo ni Magufuli.

Congratulations in advance President Magufuli

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Magufuli akifanikiwa kupora ushindi wa Lissu

Basi majambazi, wanyanyasaji, wakandamizaji na madikteta wa Dunia wameshinda
 
Back
Top Bottom