Kesho Oktoba 28, 2020 ni siku ya uchaguzi mkuu wa Tanzania. Nianze kwa kuwatakia Uchaguzi mwema wa Kizalendo kwa watanzania wote, ukiwa uchaguzi wa amani, huru na haki kwa watanzania wa vyama vyote, jinsi zote, dini zote, rika zote na kada zote.
Uchaguzi huu ni muhimu kwa watanzania na Afrika kwa ujumla, Magufuli akishinda, Tanzania imeshinda na huo ni ushindi wa Afrika nzima kwa sababu zifuatazo:
1. Watanzania na waafrika wote kwa ujumla pasipo kujali itikadi zao wanakubaliana nami kwamba Hatua ya serikali ya JPM kupitia upya mikataba ya madini na kuongeza pato LA madini kwa taifa ni jambo Jema LA kishujaa na kizalendo hivyo anafaa kuchaguliwa tena katika awamu ya pili. Hivyo JPM akishinda ni ushindi wa Tanzania na Afrika kupitia madini.
2. Watanzania na waafrika wote wataungana nami kwamba usafiri wa anga kwa Taifa ni muhimu sana na nchi kumiliki ndege zake kuna manufaa kiuchumi, kisiasa na kijamii hivyo JPM kufufua ATCL na kununua ndege mpya ni jambo jema na lenye manufaa kwa nchi hivyo anapaswa kupigiwa kura nyingi kesho na ushindi wake ni ushindi wa Taifa na Afrika nzima
3. Watanzania na waafrika wote watakubaliana nami kwamba ujenzi wa miundo mbinu kama reli, Barabara, madaraja, vivuko na fly over ni kuchochea maendeleo kwa Taifa kwa kuimarisha usafiri na biashara. Hivyo kitendo cha JPM kufanya uwekezaji mkubwa katika miundo mbinu ni jambo zuri lenye kumfanya achaguliwe tena. Ushindi wa JPM ni ushindi wa Taifa na Afrika kupitia miundo mbinu
4. Kupitia uwekezaji mkubwa katika Elimu kupitia elimu bure, mikopo na ukarabati wa shule kongwe, vyuo na uboreshaji wa mifumo ya uthibiti ubora kupitia NACTE, TCU, SQA, NECTA na Wizara ya Elimu. Usimamizi thabiti wa Elimu unamfanya JPM kama Rais wa mfano kwa Afrika nzima hivyo JPM akishinda Afrika imeshinda kupitia Elimu.
5. Uthibiti wa maliasili na utalii ambapo serikali ya JPM imethibiti mauaji ya Tembo, utoroshaji wanyama hai na ujangili. Ushindi wa JPM ni ushindi wa Tanzania na Afrika kupitia wanyama pori
6. Hatua ya JPM kuhimiza uwajibikaji na kukomesha rushwa na uhujumu, mishahara hewa na vyeti feki kumeleta heshima kwa serikali na Taifa hivyo akishinda, Afrika imeshinda.
7. Msisitizo wa JPM katika ujenzi wa viwanda ili kuongeza ajira, kuongeza thamani ya bidhaa na kupanua soko LA ndani na nje ni jambo jema kwa uchumi wa familiya, Taifa na Afrika nzima.
8. Katika vita dhidi ya Korona, JPM amekuwa mfano na kielelezo cha kiongozi shupavu, jasiri na mbobezi kwa kuzuia lockdown na kuliongoza Taifa ktk ushindi dhidi ya Korona na nchi IPO salama na maisha yanaendelea. JPM akishinda, Tanzania imeshinda na Afrika imeshinda
9. Katika uthibiti wa madawa ya kulevya, biashara haramu inayonyong'onyeza nguvu kazi, JPM kaonesha ushupavu hivyo ushindi wake ni ushindi wa Taifa na Afrika dhidi ya madawa ya kulevya.
10. Katika Uhuru, amani na ulinzi na usalama wa Nchi na rasilimali zake, JPM amedhihirisha weledi. Ameimarisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama kupitia mafunzo, vifaa na maslahi. Ameimarisha ulinzi wa madini kwa kujenga ukuta wa mererani, kufunga vifaa vya usalama migodini na n.k. Mipaka IPO salama na nchi inatawalika na maisha yanaenda vizuri hivyo ushindi wake ni ushindi kwa Taifa na Afrika nzima.
Mwisho, JPM amerejesha hadhi ya utumishi wa umma, ameboresha maslahi kwa kupunguza kodi, amelipa malimbikizo na kupandisha madaraja, ameboresha vitendea kazi na kuondoa uonevu maofisini.
Kwa sababu hizo na nyinginezo, Mpigie Kura ya ndio JPM, maana JPM akishinda, Tanzania Imeshinda, ni Ushindi wa Afrika