Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

Nilitumia mfano wa Nyerere kumjibu mwenzako aliyetaka kumfananisha Nyerere na huyu kapuku.
Kiufupi Nyerere hakuwa na roho ya ubinafsi kama huyu mhutu
 
Kwani watu wa geita umewadhalau hawana uhitaji wa usafiri wa ndege??
 
Hata Dictator Mobutu alijenga li uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwake
 
Magufuli hata aseme nini lkn ukweli unabaki pale pale kuwa hana hoja yoyote ya kuutetea huo ufisadi aliyofanya kwa kujenga uwanja wa ndege Chato.

Ndio maana tunataka katiba mpya ili watu kama hawa waweze kuwajibishwa kwa huu utumiaji mbaya wa madaraka. Haiwezekani mtu kama huyu anastaafu halafu tena anaenda kula kodi za wananchi ambao muda wote akiwa madarakani ametumika kuwadhulumu mali zao.

Kihaki hastahili kabisa kupewa tena ridhaa ya kuongoza nchi hii.
 
Huyu ndio Dkt Magufuli mgombea wa Chama cha Mapinduzi na kipenzi cha Watanzania wa rika zote.
2020 ni zamu yake tena bado Watanzania tuna IMANI kubwa na yeye.
Tijitokeze kwa wingi kupiga kura kwa CCM na Dkt Magufuli amefanya mengi makubwa.
 
Hata Dictator Mobutu alijenga li uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwake mbwa we
Ule uwanja alioujenga Mobutu ulikuwa wa uma wawakongomaniii???

Ule uwanja alioujenga Mobutu ulikuwa Mali yakwake binafsi, na ndiomaana ukaitwa uwanja wa Mobutu.

Swali ni kwamba, huo uwanja wa chato ni mali ya mtu??
 
Kila mtu anahitaji usafiri wa Ndege, hata Morogoro wanahitaji, hiyo sio hoja ya kufanya uwekezaji wa Bil 40
Kwahiyo shida yenu kumbe ni wivu tuuu unaowasumbua kwa kuwa uwanja umejengwa mkoani geita.

Kwani morogoro hawana uwanja wa ndege ata mumojaa??
 
Marais wote waliotangulia walikosea kutojenga viwanja vijijini walikozaliwa!Wajao wote waige kwa JPM,wajenge walikozaliwa ilimradi ni Tanzania!Hebu niambie,ni eneo gani nchini kinajengwa kiwanja ambapo kimazingira ni kama chato?Hivyo viwanja vinavyojengwa na kupanuliwa ni mijini kama Dodoma,Mwanza,Mbeya,Tanga nk!
 
Kwani kigezo cha kujenga uwanja wa ndege, nikusajiri kampuni ya usafirishaji Kwanzaa?
Kigezo cha kujenga kiwanja cha ndege kama cha chato Ni kujua mahitaji ya usafiri wa ndege kwanza.
Kufahamu kiasi na aina ya mizigo itakayokuwa inasafirishwa kupitia kiwanja hicho.
Kufahamu idadi ya abiria watakao safiri kupitia uwanjani hapo
Huwezi kukurupuka na kujenga liuwanja la ndege kama la Chato bila kuwa na takwimu hizo kwanza
Ndio maaana tunasema Hilo li white elephant litakuwa kama Lile alilojenga Dictator mwenzake Mobutu huko kijijini kwake
 
Kwahiyo shida yenu kumbe ni wivu tuuu unaowasumbua kwa kuwa uwanja umejengwa mkoani geita.

Kwani morogoro hawana uwanja wa ndege ata mumojaa??
Sema umejengwa kijijini chato alikozaliwa Rais!Nchini hakuna sehemu nyingine unajengwa uwanja penye hadhi kama ya chato!
Mji wa kibiashara kama Kahama,hakuna uwanja!Mpaka watu washukie mwanza halafu wasafiri masaa 5 kwenda kahama!
Huko Chato kunajengwa hospitali kubwa ya rufaa ya kuhudumia kanda,kweli?
Chato Kumejengwa bandari kubwa,sijui kuna mizigo gani wanataka kupakia na kushusha!!!!
Hata mwenye akili anaona huo ni umobutu seseko!
 
Ule uwanja alioujenga Mobutu ulikuwa wa uma wawakongomaniii???

Ule uwanja alioujenga Mobutu ulikuwa Mali yakwake binafsi, na ndiomaana ukaitwa uwanja wa Mobutu.

Swali ni kwamba, huo uwanja wa chato ni mali ya mtu??
Ule uwanja ulikuwa mali ya umma kama huu uliojengwa Chato ndio maaana sasahivi Ni kambi ya jeshi
 
Longo longo kibao.Ujenzi wa uwanja wa Chato ni matumizi mabaya ya madaraka ambayo utayakuta Afrika pekee yake.Mabara mengine huu upuuzi walishasahau tangu karne ya 20.
Tanzania ndipo sehemu pekee Rais anaweza kuchukua pesa Hazina pasipo idhini ya bunge
 
Mrema alipeleka mapipa ya lami Moshi, Nani ulimsikia akilalamika miaka ile?.

Msuya akaweka umeme Mwanga miaka ile, Nani ulimsikia akilalamika?.

Tanzania tukiitazama kisiasa na kibaguzi hatutafika popote.

Kumbuka kuna watoto wanaosoma bure sasa kule Chato wakija kuwa watu wazima wenye elimu watautumia uwanja ule.

Kumbuka kuna wasomi wapo udom muda huu miaka michache ijayo wataimarish utalii wa kanda ya ziwa.
Kuna maisha baada ya sisi wa leo hii kuwa tumeshazikwa, ubinafsi hautusaidii.
 
Hata Dictator Mobutu alijenga li uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwake
Mabotu aliingia madarakani kwa mapinduzi,alijenga jumba la kifahari huko kijijini kwake ,aliamua kujenga uwanja jilani na jumba hilo,baada ya kupinduliwa watu walikwenda kuvunja na kuiba Mali yote na kuacha ghofu, alafu kipindi hicho hiyo nchi ilikuwa haina shirika la ndege na mpaka Leo haina shirika la ndege na na nchi hiyo imetawaliwa na kuvurugwa na wazungu has a wabelgiji na nchi zinazozunguka na INA vibaraka wengi wanaotumiwa na wazungu ili kuiba rasilimali.

Tofauti na magufuri ambaye ameingia madarakani kwa democrasia,amekuwa waziri wa ujenzi 15 years,amejenga viwanja vya ndege songea, mtwara, kigoma, rukwa, kagera, songwe, katavi, tanga na chato na anampango wa kujenga viwanja kila wilaya tanzania na kuviwekea lami kanunua ndege na ataziongeza,barabara unazoringia hizo nyingi zimejengwa kwa usimamizi wa magufuli, na anaendelea kuijenga ukitafuta MTU aliyeijenga Tanzania uwezi kumuacha magufuli yeye ni babalao.
 
Kwani umewapima wakazi wa geita hawawezi kusafiri kwa ndege??

RAIA wote ni sawaa.
 
Jamaa anapenda ndege! Hebu afanye utafiti ni watanzania wangapi Wana uwezo wa kupanda ndege ,anakera.
Ni kama unapata baba yako ni mkulima huko gambushi. Akalima kwa shida. Akapata pesa. Asilimia 90% ya pesa akanunua gari.
Ndo unavomaanisha?
 
Tulikua na fast jet hapa ambayo ilikua very cheap and efficient kuliko hii ATCL .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…