Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

Kwahyo hiyo wakazi wa geita hawawezi kulipia usafiri wa ndege ili shirika la ndege liende kufanya biashara hukoo??

Au huo uwanja wa ndege hauna viwango vya ndege kutua paleee??
kwanza uwanja upo wilayani Chato na sio Geita Mjini
Uwanja huo unahadhi ya kimataifa Kama aliojenga dictator Mobutu ambao Hadi Concord ilikuwa inaweza tua
Halafu Kama wangekuwa na uwezo huo lazima mashirika ya ndege yangeanzisha route za huko.
biashara ya ndege sio Kama daladala unapeleka gari unalipigia debe kuita abiria
 
Aiseee you guys need to think kwa kweli!Hivi umesoma ulichokiandika?Najua deep down mnajua si sahihi ila kwakuwa mnaendeshwa na mihemko ya kisiasa basi mnalazimika kuandika msichokiamini!
Ninachoukiza na naomba uwe muwazi kukijibu,je,Rais angekuwa hatokei Chato,uwanja ule ungejengwa huko?Je,hospitali kubwa ya rufaa ya kuhudumia kanda ingefikiriwa kujengwa Chato?Bandari je?
Kama marais wote wangefanya kama JPM,nchi hii miaka kadhaa ijayo ingekuwa inaongoza kuwa na viwanja vya kimataifa vijijini!
Rais akifa leo hivyo vitu vyote anakwenda navyo kaburini?.

Hao watakaobaki wakivitumia sio walipa kodi wa Tanzania?.

Ni fikra za kibaguzi tu kuamini kwamba watu wa Chato na Geita hawana hadhi ya kuwa na maendeleo.
 
Mara mia hospitali inaeleweka kabisa kwa sababu ni kwa faida mapana ya watu, na hapo tusibague kikanda, tutakua tumekosea...kwa hospitali mtu akiniambia watu wa pale sio watanzania inaleta mantiki kabisa... lakini uwanja wa ndege hapana kabisa... na kwa hilo tu mkuu wa nchi akiambiwa awaombe msamaha taifa kwa unyenyekevu anaouhubiri kwake na kwa wateule wake kila kukicha, utaona cha mtema kuni haijawahi kutokea...

Si tunaaminishwa ni msema kweli, mnyenyekevu, alizaliwa kimakosa kama binadamu alitakiwa awe na mamalaika... kwani hayo maneno yote nimeota au tumeambiwa na yeye mwenyewe hadharani???
Mkuu hospitali kwa mujibu wa makaratasi yao ni kupunguza mzigo kwa Bugando!Yaani wakazi wote wa Kigoma,Rukwa,Shinyanga na Kagera waende kutibiwa Chato kama hospitali ya Rufaa badala ya kwenda Bugando!
Jamani!!!!!
 
Rais akifa leo hivyo vitu vyote anakwenda navyo kaburini?.

Hao watakaobaki wakivitumia sio walipa kodi wa Tanzania?.

Ni fikra za kibaguzi tu kuamini kwamba watu wa Chato na Geita hawana hadhi ya kuwa na maendeleo.
Mobutu seseko kwani alienda navyo kaburini?Acheni majibu ya rejareja kwa mambo serious!Tokea mmemsikia akisema hataenda nao uwanja kaburini basi na nyinyi mmebeba hivyo hivyo kama lilivyo na kuufanya utetezi wenu!
Jibuni maswahi kwa hoja zenye mantiki,sio porojo za hapa na pale!!!
Je,JPM angekuwa mzawa wa shinyanga,uwanja ungejengwa Chato?
Msingi wa swali hilo ni ili kujua kama uwanja ni wa kimkakati wa kiuchumi uliopangwa na serikali na si mpango kutokana na Rais kazaliwa wapi!
 
1.Kuna uhusiano wowote wa uwanja ule kujengwa Chato na Rais wa nchi kuwa mzawa wa huko Chato?Au ni mipango tu hata JPM angekuwa amezaliwa Shinyanga basi uwanja ungejengwa Chato!!!
2.Ni sehemu gani nyingine nchini ambapo uwanja umepelekwa wilayani na mkoani hakuna uwanja?Ukishindwa hilo,nitajie tu wilaya zenye viwanja vya vyenye hadhi kama ya Chato!
Mpaka leo bado mikoa mingi nchini haina viwanja vya ndege!Iweje Chato?
Tanzania ni nzima imejaa viwanja vya ndege na umuhimu wake unajulikana.

Uwanja wa Chato upo kimkakati. Unapokuwa na uwanja wa hadhi ya Mwanza ambao utakuwa ni hub maana yake unahitaji uwanja mwingine ambao ni alternative airport, Chato airport inafanya kazi hiyo.

Uwanja wa KIA unayo alternative ambao ni uwanja wa Arusha.

Uwanja wa Dar alternative ni Zanzibar.
 
Zote ni investments zenye faida zinazoishi kwa miaka mingi mbeleni.
Faida za Investments hazifanani... barabara na umeme ni ndio uwekezaji unaogusa watu maskini na kwa haraka...leo hii tunaona barabara strategic ziko hoi, kwanini hizo bil 40 hazikwenda huko?

Ukarabati kichekesho Rusahunga - Rusumo

Hili jambo lilikosewa, hata mkijaribu kulipaka rangi gani. Ndio maana inakuwa ngumu kulitetea
 
Mobutu seseko kwani alienda navyo kaburini?Acheni majibu ya rejareja kwa mambo serious!Tokea mmemsikia akisema hataenda nao uwanja kaburini basi na nyinyi mmebeba hivyo hivyo kama lilivyo na kuufanya utetezi wenu!
Jibuni maswahi kwa hoja zenye mantiki,sio porojo za hapa na pale!!!
Je,JPM angekuwa mzawa wa shinyanga,uwanja ungejengwa Chato?
Msingi wa swali hilo ni ili kujua kama uwanja ni wa kimkakati wa kiuchumi uliopangwa na serikali na si mpango kutokana na Rais kazaliwa wapi!

Kwani Chato sio Tanzania, mbona kuna uwanja Kilimanjaro na upo mwingine Arusha?.

Ndio maana nimekwambia wewe ni mbaguzi tu kama wengineo wengi.

Unaitazama Chato ya leo umeshajiuliza miaka mitano ijayo au kumi lile eneo litakuwa na mabadiliko gani kiuchumi na kijamii?.
 
Tanzania ni nzima imejaa viwanja vya ndege na umuhimu wake unajulikana.

Uwanja wa Chato upo kimkakati. Unapokuwa na uwanja wa hadhi ya Mwanza ambao utakuwa ni hub maana yake unahitaji uwanja mwingine ambao ni alternative airport, Chato airport inafanya kazi hiyo.

Uwanja wa KIA unayo alternative ambao ni uwanja wa Arusha.

Uwanja wa Dar alternative ni Zanzibar.
Kwani uwanja wa Mwanza umejengwa juzi?Upo miaka na miaka!Kwanini uwanja haujajengwa shinyanga badala yake ukajengwa Chato?Msitufanye wajinga!Uwanja wa Mbeya alternative yake ni upi?
 
kwanza uwanja upo wilayani Chato na sio Geita Mjini
Uwanja huo unahadhi ya kimataifa Kama aliojenga dictator Mobutu ambao Hadi Concord ilikuwa inaweza tua
Halafu Kama wangekuwa na uwezo huo lazima mashirika ya ndege yangeanzisha route za huko.
biashara ya ndege sio Kama daladala unapeleka gari unalipigia debe kuita abiria
Haaaaa haaaaa. Umezidiwa hoja mnakimbilia matusi.
Tutaendelea kuwafundisha tuuu. Ngoja nikuripot TCRA wakunyoooshe kwanzaaaa
 
Kwani Chato sio Tanzania, mbona kuna uwanja Kilimanjaro na upo mwingine Arusha?.

Ndio maana nimekwambia wewe ni mbaguzi tu kama wengineo wengi.

Unaitazama Chato ya leo umeshajiuliza miaka mitano ijayo au kumi lile eneo litakuwa na mabadiliko gani kiuchumi na kijamii?.
Hiyo yote ni mikoa,kama uwanja ulivyo Mbeya,Tanga,Dsm,Kigoma nk!
Lakini chato ambako hata magari ni ya kuhesabu!Abiria gani watapanda hizo ndege?Rais akitoka madarakani na uwanja ndio hivyo kazi imekwisha!
Miaka 5 au iwe 20,chato haitakuwa na uhitaji kama ilivyo kahama na miji mingine yenye uhitaji sasa!
 
Haaaa haaaa, chadema bwaanaaa, mkizidiwa hojaaaa mnakimbilia matusiii.

HIVI MATUSI NDO IRANI YENU YA UCHAGUZI MWAKA HUUUU???

Kwani chato wilaya iliyopo mkoa wa geita hawana hadhi ya kujengewa uwanja wa ndegeee?
Wamejengewa kwasababu ya Rais ni mzawa wa huko!Ndio maana mpaka leo Rais na marafiki zake ndio wateja pekee wa uwanja wa Chato!
Hebu ingia online ufanye booking ya tiketi kwenda chato!
 
Wamejengewa kwasababu ya Rais ni mzawa wa huko!Ndio maana mpaka leo Rais na marafiki zake ndio wateja pekee wa uwanja wa Chato!
Hebu ingia online ufanye booking ya tiketi kwenda chato!
Tuko busy kugombana kuhusu magufuli. Wakati adui yetu tunaetakiwa kupambana nae yuko nyuma ya pazia akiplay kama " ukoloni mambo leo"
 
Mkuu hospitali kwa mujibu wa makaratasi yao ni kupunguza mzigo kwa Bugando!Yaani wakazi wote wa Kigoma,Rukwa,Shinyanga na Kagera waende kutibiwa Chato kama hospitali ya Rufaa badala ya kwenda Bugando!
Jamani!!!!!
Kaka nimekuelewa... nachosema, kama wanatetea kwamba popote pale maendeleo yakifikishwa ni haki ya watu wa pale kwani ni watanzania pia, hapo mimi binafsi siwezi kubishana kwa nguvu kubwa kwani msema kweli hawezi kuimba wimbo huu na wakati wa majaribio nikawa mwongo wakati roho na mantiki yangu inakubali kwamba wao pia ni watanzania...na hospitali ikiendeshwa ipasavyo inatija sana kwa watu wa eneo husika na ni haki ya msingi kwa raia wa nchi yoyote ile wanaokusanyishwa kodi.. natarajia umenielewa...

Kwa sababu topic hii inajadili hasa uwanja wa ndege na jinsi mkulu alipangua hoja; nasema hakuna uhalali kivyovyote vile. Iwe mantiki, iwe haki yao kama watanzania (kwani haki pia inapimwa kwa uhitaji wa wakati ule), n.k
Kuna viwanja vya ndege zinaingiza mapato nyingi mno na kupitia viwanja hivyo tunapata mapato ya kila aina kupitia watalii, mfano mzuri ni uwanja wa Arusha... kama kiwanja kile lingegeuzwa kuwa kama KIA faida tungeiona mara mmoja tu, sio hii mantiki ya kuona faida eti baadae... Nasema vipaumbele ni muhimu sana, na sio matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia mabilioni ya pesa ya walipa kodi na kuleta utetezi usio na miguu wala kichwa...
 
Kwani uwanja wa Mwanza umejengwa juzi?Upo miaka na miaka!Kwanini uwanja haujajengwa shinyanga badala yake ukajengwa Chato?Msitufanye wajinga!Uwanja wa Mbeya alternative yake ni upi?
Uwanja wa Mwanza umepanuliwa kimkakati katika awamu hii ili uwe ni Kituo kikubwa cha ndege cha ukanda huu (hub), unapokuwa na hub unahitaji kuwa na uwanja wa msaada ulio karibu kwa ajili ya dharura itakayotokea.
Ni masuala ya kimkakati na sio kisiasa kama inavyoandikwa humu jukwaani.

Uwanja wa Mbeya alternative ni Iringa.
 
Hiyo yote ni mikoa,kama uwanja ulivyo Mbeya,Tanga,Dsm,Kigoma nk!
Lakini chato ambako hata magari ni ya kuhesabu!Abiria gani watapanda hizo ndege?Rais akitoka madarakani na uwanja ndio hivyo kazi imekwisha!
Miaka 5 au iwe 20,chato haitakuwa na uhitaji kama ilivyo kahama na miji mingine yenye uhitaji sasa!
Wewe unaiongelea Chato ya leo, kumbuka kuwa yapo maisha baada ya mimi na wewe kuwa tumeshazikwa.
 
Back
Top Bottom