Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

Unauliza kwanini iwe Chato na mimi nakuuliza kwani Chato sio sehemu ya Tanzania?.

Nani kakwambia kuwa chato ya leo ni sawa na jle ya 2035?. Tuwe tunaiangalia Tanzania ya kesho muda wetu hapa duniani ni mfupi.
Ni ngumu sana kubadilisha gia angani ukishakuwa mshabiki wa mtu au kitu fulani hata kama una macho na masikio, ukiacha neema zingine tuliopewa na Mwenyezi Mungu kama vile akili... hii inakuhusu wewe, mimi na wote tuliojaaliwa na hizo baraka... penye baraka kuna uwajibikaji siku zote... kila la kheri..
 
Hoja kama hizi zinawaondolea heshima makamanda wenzangu. Kipindi hiki cha Corona unategemea Atcl wapate faida?
Atcl kwa nini isikaguliwe na CAG wakati ni shirika la umma? Tunajiabisha tuwe makini kujibu hoja
Wewe,hapo umeandika nini?

Hivi kweli unajielewa?

Jaribu kusoma tena ulichoandika wewe Mataga
 
Unadhani hawaelewi hayo mkuu?Wanajua sana ila ndio hivyo lazima watetee tu!Hata usiku watauita mchana!Siku moja watamkana kwenye hili,subiri atoke madarakani ndio utajua rangi halisi za hawa viumbe wanaofikiri kwa kutumia ujazo wa matumbo yao!
Kabisa... utajidanganya mpaka lini, iko siku utachoka tu... ndio inavyokuwa mara nyingi sana... Wapenda haki ya ukweli tuendelee kukosoa inapobidi na Mungu yupo, kuna vitu vinacheleweshwa kwa makusudi na Mwenyezi Mungu ambaye ndio anapanga kila kitu.

Lakini siku mageuzi ya ukweli yakija kwa mipango ya Mungu tu na si vinginevyo, watu waliokuwa wanawaaminisha wengine kwa kuwapumbaza wanakuwa wa kwanza kuaibishwa na kupotezwa... na kwetu Tanzania pia itakuja soon... much sooner than they think kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu pekee....
 
Wamejengewa kwasababu ya Rais ni mzawa wa huko!Ndio maana mpaka leo Rais na marafiki zake ndio wateja pekee wa uwanja wa Chato!
Hebu ingia online ufanye booking ya tiketi kwenda chato!
Kwani umeingia on line ukaona na wiwanja vinginee?

Acheni kubwabwaja hapa, lazima iundo mbinu ijengwa na itaendelea kujengwaaa
 
Kwani umeingia on line ukaona na wiwanja vinginee?

Acheni kubwabwaja hapa, lazima iundo mbinu ijengwa na itaendelea kujengwaaa
Ni kweli itajengwa,ndio maana sasa mpango ni kujenga uwanja wa kimataifa wa mpira wa miguu Chato ili kuvutia watalii!!!
 
Nimekuwa nafuatilia kwa ukaribu kampeni za urais zinazoendelea nchini ambapo Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato Mkoani Geita imekuwa ni moja ya agenda KUU za mgombea urais wa CHADEMA TUNDU LISSU.

Kabla ya Kuanza kujadili kwa kina kuhusu umuhimu wa kiwanja hicho kwa sasa, ni AIBU kwa mgombea wa nafasi ya urais kutumia ujenzi wa kiwanja hicho kuwa miongoni mwa ajenda kuu ya kukuingiza Ikulu kwa hali ya kawaida ilitarajiwa mgombea wa nafasi ya urais wa upinzani kuja na Sera mbadala za kiuchumi, kisiasa na kijamii ili kuvuta hisia za wapiga kura.

Turejee kwenye mjadala wetu mama wa ujenzi wa ujenzi wa kiwanja cha Ndege Chato, nilichobaini katika mijadala mingi inayoendelea kuhusu jambo hilo ni wachangiaji wengi wanaoongozwa na mihemko na itikadi za kisiasa bila kuwa na tafakuri ya kina ili kubaini uhalisia wa jambo hilo.

Ili kupata uelewa mpana wa kwani ujenzi huo ulifanyika Chato ni muhimu sana walau kwa uchache tukafahamu mambo yafuatayo:


** kijiografia mji wa Chato ndio upo karibu zaidi na hifadhi za taifa za Burigi, Ibanda, Kimisi, Rumanyika na Biharamulo ambazo zote zinapatikana mkoa wa Kagera. Vilevile upo karibu sana na hifadhi ya Rubondo yenye wanyama mbalimbali kama Twiga, Tembo, Swala, Viboko, Pongo na Sokwe mtu.

** Wilaya ya Chato inapatikana katika mkoa wa Geita ambao una Mgodi mkubwa wa Geita Gold Mine uliochini ya wawekezaji na umekuwa ukitajwa kama miongoni mwa migodi ambayo inzauzalishaji mkubwa wa dhahabu barani Afrika. Kadhalika ndani ya chato kuna shughuli za uchimbaji madini zinazofanywa na wachimbaji wadogo katika maeneo ya Msasa, Matabe, Imwelu, Makurugusi, Bwanga, Iparamasa, Buseresere na Nyarutembo

** Wilaya ya Chato inapatikana karibu na Ziwa Victoria lenye samaki wa aina mbalimbali ikiwemo Sato, Sangara, Mumi, Dagaa, Gogogo, Kamongo n.k likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 100 na mialo 34.


Baada ya kupata wasifu ya Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita kwa ujumla na maeneo jirani, kwa mtazamo wa jicho la kiuchumi hasa uuchumi wa kati tulioufikia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato umejengwa kwa kimkakati na utakuwa na manufaa yafuatatyo;-


i) Kuongeza idadi ya watalii katika hifadhi ya taifa ya Lubondo mkoani Geita na hifadhi zilizopo mkoani Kagera kwa kuwa kiungo muhimu kati ya Tanzania na Nchi jirani za DRC Congo, Burundi, Rwanda na Uganda ambazo ni jirani kabisa na vivutio hivyo. Hivyo kuiongezea Serikali mapato.

ii) Utasaidia kuongeza na kuimarisha usafirishaji wa abiria kwenda nchi jirani, mizigo, mazao na bidhaa mbalimbali kama vile asali, minofu ya samaki kutoka Tanzania kwenda nje ya Nchi.

iii) Utachangia katika kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania, kukuza biashara katika wilaya ya Chato na Mkoa wa Geita kwa ujumla hivyo kuondokana na umasikini.

iv) Utasaidia kuongeza ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Tanzania na mataifa jirani ya Uganda, DRC Congo, Rwanda, Burundi n.k

Kwa ujumla kiwanja hicho kitakuwa na tija katika maeneo ya Utalii, biashara na katika sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji. Pia utasaidia kuibua vivutio vingi mbalimbali vitavyovuta watalii wengi zaidi kuja kuitembelea Tanzania.

Licha ya sababu na manufaa lukuki ambayo yanatarajiwa kupatikan Chato, Geita na Tanzania kwa ujumla bado unakutana na mtu anajenga hoja dhaifu kama anapendelea Chato kwa kuwa ndio nyumbani, nimekuwa najiuliza hivi kumbe kata, wilaya, Mkoa au kanda ikitoa kiongozi wananchi wa eneo hilo HAWANA HAKI ya kuletewa maendeleo hadi kiongozi huyo atoke madarakani?? hebu tubadilike kwa kuachana na fikira hizo mgando, wakazi wa Geita kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wana haki ya kuletewa maendeleo kama wananchi wa maeneo mengine Kama Kilimanjaro, Arusha, Dar n.K
 
Serekali siku zote ikijiingiza katika biashara tegemea majanga makubwa.Binafsi ningependa ATCL ishirikiane na sekta binafsi katika uendeshaji wake na hasa bodi wawepo watu binafsi.
I agree with you on the issue of accountability. Shida kubwa ni kuwa kuna wakati hata kama mashirika hayaendeshwi kibiashara, bado kuna confidence kwamba hela ya kuyaendesha itapatikana tu.
Haya mashirika sasa hivi yapewe mzigo sawa na makampuni binafsi kwenye suala zima la kujiendesha
 
Nimekuwa nafuatilia kwa ukaribu kampeni za urais zinazoendelea nchini ambapo Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato Mkoani Geita imekuwa ni moja ya agenda KUU za mgombea urais wa CHADEMA TUNDU LISSU...
Sasa baada ya nadharia leta uhalisia.
 
Kaka uwanja ndio ushajengwa na utatumiwa na vizazi vingi vya kesho.

Walioujenga uwanja wa KIA wangekuwa na mawazo kama ya kwako miaka ya nyuma wasingeujenga...
Hoja zako si kweli kabisa na hazina mashiko. Eti economic benefits hazionekani ndani ya mwaka au miaka miwili? Na unafurahi kutumbukiza hela zako kwenye mradi wa namna hii ukitegemea uanze kuona economic benefits baada ya miaka 4 hivi?

Kama ni hela yako ya mfukoni waweza kufanya hivyo? Mradi wowote lazima economic benefits zianze kuonekana mara baada ya kumalizika labda useme return on investment yaweza kuchukua miaka mingi au hata miongo..
 
HUNA HISTORIA YA
HUNAHISTORIA YA RAIS MOBUTU WEWE KAA KIMYAAAA.
MOBUTU ALITUMIA FEDHA YA UMA KWAKUJENGA MIRADI NA MALI ZAKE BINAFSI.
JEE UMESIKIA UWANJA WA CHATO NI MALI YA MAGUFULI??

UPINZANI MUMEVURUGWAA
Acha ubishi...ndege za Magufuli,Chato ya Magufuli,Tanzania ya Magufuli
 
Back
Top Bottom