Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli hajawahi kushindwa, hatashindwa

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli hajawahi kushindwa, hatashindwa

Naunga mkono bandiko lako, hakuna namna wapinzani najiandaa kumuona JPM anaapishwa tuu.

USHINDI kwa CCM October 28 ni Lazima, kwasababu CCM ina mtaji wa watu wengi.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Acha vituko wewe!

Kama Lowasa mlimdekia hadi barabara, mtu ambae Lisu ma chadema nzima walimnanga kwa miaka 8, sembuse Magu?
Magufuli yupi??huyu huyu ambae anateua wapinzani huku Wana CCM wafia chama tupo tuu??akose tuu
 
Naomba nikwambie kuwa magufuli hakuwahi kushinda wala kushindwa kwa kuwa ni muoga kuingia kwenye ushindani ,nasi watanzania tutamwadhibu kwa makosa yafuatayo

1. Kuiba na kula rambirambi
2. Wizi wa 1.5 trillion
3. Ukandamizaji wa haki za binadamu
4. Ubaguzi
5. Uongo na ahadi zisizotekelezeka mfano Noah kwa kila mtanzania na zile 50 mln kwa kila kijiji
6. Utekaji na mauaji
7. Kujificha wakati wa majanga mfano covid19 na Ajali ya MV nyerere
8. Udhalilishaji wa wanawake majukwaani
9. Hajatimiza moja ya masharti ya kugombea urais yanayosema kuwa lazima mgombea ajue "kuongea na kuandika kiswahili na kingereza kwa ufasaha"
10. Ameiba aridh huko karagwe 25000 hekari
Hivi huu uongo wako ni kwa faida ya nani tukutane 28 ndio utajua Magufuli ni nani.
 
Mbona kashindwa kuongeza mishahara kwa wafanyakazi Wa umma , pia kashindwa kulipa fidia za aliowabomolea majumba mbezi ya kimara .

Sasa unasemaje hajawahi kushindwa
 
Tundu hawezi kua rais labda rais wa t.f.f
 
Mbona kashindwa kuongeza mishahara kwa wafanyakazi Wa umma , pia kashindwa kulipa fidia za aliowabomolea majumba mbezi ya kimara .

Sasa unasemaje hajawahi kushindwa
Toshekeni na mishahara yenu, ujenge kwenye hifadhi kwa kiburi afu na fidia ulipwe - jifunzeni kuzingatia sheria
 
Aliyeshiba hamjui Mwenye njaa hata siku moja
No, anajua - Serikali imeendelea kutoa ajira kuchao, imeweka mazingira rafiki kwa wakulima ie pamba, kahawa, chai, korosho nk

Bei za mazao hayo pia zimepanda mara kwa mara
 
Wewe hujui unachoandika. Fatilia historia yake vizuri. Ubunge alikuwa akiangukia za pua mpaka chato ilivyotoka kagera ndyomaana hawapendi watu wa kagera. Na chaguzi zake amekuwa na tabia ya kupita bila kupingwa. Yani mpinzani anamhonga anajitoa kwenye uchaguzi. Hivyo ndivyo aliweza kushinda.
 
No, anajua - Serikali imeendelea kutoa ajira kuchao, imeweka mazingira rafiki kwa wakulima ie pamba, kahawa, chai, korosho nk

Bei za mazao hayo pia zimepanda mara kwa mara
Hiyo nchi gani unayoongelea
 
Naomba nikwambie kuwa magufuli hakuwahi kushinda wala kushindwa kwa kuwa ni muoga kuingia kwenye ushindani ,nasi watanzania tutamwadhibu kwa makosa yafuatayo

1. Kuiba na kula rambirambi
2. Wizi wa 1.5 trillion
3. Ukandamizaji wa haki za binadamu
4. Ubaguzi
5. Uongo na ahadi zisizotekelezeka mfano Noah kwa kila mtanzania na zile 50 mln kwa kila kijiji
6. Utekaji na mauaji
7. Kujificha wakati wa majanga mfano covid19 na Ajali ya MV nyerere
8. Udhalilishaji wa wanawake majukwaani
9. Hajatimiza moja ya masharti ya kugombea urais yanayosema kuwa lazima mgombea ajue "kuongea na kuandika kiswahili na kingereza kwa ufasaha"
10. Ameiba aridh huko karagwe 25000 hekari

kaaaaaah wewe ni muongo adi sio vizuri data zote unazozitoa sio zakweli kabisa.ni mjinga hutumii akili kweli unataka noah 50mln kwa kila mtanzania
 
Kwa niaba ya vijana walio katika ajira ila hawalipwi mshahara mizuri(walimu) na wale vijana ambao hawana ajira ni kwamba hatudanganyiki. Pili, msimamo wetu uko pale pale kwamba tunamchagua Tundu Lisu ili aweze kutujali sisi vijana. Tatu, hata kama hatahahikisha tunapata ajira wote atapitisha sheria nzuri na kuboresha mzingira mazuri ya kujiajiri na kuajiri vijana.
 
Dodoma alituahidi. 2017-20.

1. Ujenzi wa uwanja mkubwa wa kisasa wa michezo kushirikiana na mfalme wa Moroco ameshindwa.

2. Ujenzi wa Barabara ya Mzunguko kuzunguka Dodoma jiji. Ring road Ameshindwa.

3Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato ameshindwa.

4. Ujenzi wa Hospital ya Uhuru baada ya kukata fedha za sherehe maazimisho ya uhuru day.

5.Kiingereza kimemshinda.

Hii ni Dodoma sijui huko mikoani?
Duuh ,hivi Kinge kinamsumbua sana.
Kama kinge kinamsumbua hawezi kwenda Ughaibuni kabisa . Na sio kwamba hapendi sifa za huko majuu lakini atakua anaogopa kuhojiwa na CNN kwa Kinge mana anaweza asielewe hata swali linahusu nini mana wale jamaa wana Kinge cha kusukutua meno kabisa.
Ndio maana anatuma watu. Angekua anapunguza matumizi angepunguza Msafara wake na pia asibgetuma MTU huko ughaibuni . Mana kumtuma MTU halafu ni gharama pia.
 
Acha vituko wewe!

Kama Lowasa mlimdekia hadi barabara, mtu ambae Lisu ma chadema nzima walimnanga kwa miaka 8, sembuse Magu?
Lengo la wapinzani ni kuiondosha CCM bara na visiwani ili nchi iwe na watu wenye usawa kupitia katiba mpya itakayoweza kumwajibisha MTU yeyote anayefanya uhalifu. Kwa sasa nchi hii ina MTU mmoja chini ya CCM ambaye ni mkuu kuliko Mungu aliyemuumba. MTU mmoja mkuu kuliko watu wote waliompa maraka, mkuu kuliko wanaolipa kodi ili alipwe mshahara.
Mkuu kuliko dini zote. Yeye ni Alfa na Omega badala ya Mungu.

Hiyo hatuitaki. CCM ikifa ndio itakua mwanzo mpya wa kuwapata viongozi bora wenye kuheshimu utaifa wetu badala ya vyama.
Mbona Uhuru Kenyata chama cha baba yake kimekufa na sasa ni Rais.

Moi na Kenyatta waliua watu kwa makumi elfu kulinda Neno KANU badala ya kulinda utaifa wa wakenya. Kumbe wakenya wote ni sawa na ni ndugu moja leo KANU haipo na watu wale wale wanatawala bila kutisha watu na kuua watu kutetea vyama.

Ndio ujinga ambao CCM hii ya awamu ya tano tunaukataa mana Kikwete alishatutoa huko kwenye siasa za kuchinjana kwa sababu ya kulinda Vyama hasa CCM . Tulifikia kuzuri kwa kuweka midahalo na kuchambua Sera bila kuumizana lakini Leo kuanzia Mkuu wa nchi mpaka chini wanahubiri uadui na visasi tuu .

Eti musiponicchagua hamtapata maji wala dawa, kwa maana kwamba wataachwa wafe kwa kiu na kukosa tiba. Sasa hiyo ni nchi gani ina kiongozi wa namna hiyo na bado aendelee kukalia kiti kwa kodi za watu kupitia katiba mbovu inayolinda ukatili na visasi kama hivyo .

Tumweke Pembeni aletewe Katiba yenye misingi yavutawala bora na yeye atagombea tena tu kwa haki na atapewa kama watashindwa lakini atawale kwa kufuata misingi ya uwajibikaji kisheria.
 
Kila kitu nchi hii ni SGR na ndege
Wao wanalipwa mamilioni na wana Mali za kutosha kila sehemu na ardhi ekari 25000. Na Mashule ya private wamejenga wao na familia zao. Mahoteli na majumba ya kupangisha. Halafu wanasema mfanyakazi anayelipwa laki NNE avumilie tu mana wanajenga nchi watakaonufaika ni wajukuu zao . Huku wao wakiwawekea wajukuu zao akiba za fedha na Mali zisizo na kifani. Kuwadanganya watu kuwa tunafunga mikanda huku wao wakiwa wananeemeka ni Dhambi kubwa mbele za Mungu. Ndio maana Mungu anabadili mioyo ya watu kumuelekea Lisu ili wao nao wasilale kwa raha kama walivyojiona kuwa wangepata raha kutokana na Mali walizo Nazo na vyeo vyao . Sasa wanapiga magoti kuomba uhalali wa kuiba kura. Waombe msamaha kwanza na wasafishe mioyo yao inayowaza kuiba na kuharibu uchaguzi ili waendelee kukalia viti vya umma.

Mungu pekee ndiye atakayewashughulikia madhalimu wanaopanga uovu kupitia madaraka.
 
Back
Top Bottom