Wakuu, salaam!
Nawakumbusha tu kwamba John Pombe Magufuli hajawahi kushindwa na haitatokea ashindwe - mara zote akiwa mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki na baadae Chato iwe ndani ya CCM au uchaguzi mkuu hakuwahi kushindwa na haitatokea ashindwe.
Katika uchaguzi tunaoenda kuufanya tarehe 28 Oktoba, 2020 bado anapambana lkn usitegemee atashindwa - sababu za kutoshindwa ziko nyingi:-
(i). Uwezo binafsi na Ubunifu:-
Haikuwa kazi nyepesi kusimamia ongezeko la mapato ya Serikali kutoka takriban 800B - 1.3T kwa mwezi (ni fedha hizi zimewezesha utekelezaji wa miradi mikubwa kwa midogo i.e viwanja vya ndege, ndege, meli, vivuko, maji, hospital na vituo vya afya, elimu bure nk nk);
(ii). Ziara za ndani:-
Wakati wote ametumia muda mwingi kufanya ziara za kikazi ndani ya mikoa tofauti na utamaduni wa viongozi wengi ambao leo wakinywa chai Ufaransa mchana hula UK - hii imemjengea sifa kubwa kwa wananchi na kuwa ktk orodha wa viongozi wanaoaminiwa;
(iii). Usimamizi wa matumizi ya fedha za umma:-
Hapa kila mmoja ni shahidi kwamba hata zile kelele za ufisadi zilizokuwa zinapigwa zimepungua sana - ingawa anapaswa kuendelea kumulika zaidi kwa watendaji wake ili wasiingize masuala binafsi kwenye utendaji wa kila siku;
(iv). Ajali za barabani - zimepungua sana tofauti na miaka kadhaa ya nyuma;
Kwa ujumla sifa za kiungozi anazo nyingi, kama kuna kasoro sehemu basi ni zile za kibinadamu ambazo kila mmoja anazo.
Rai yangu:-
Kwa kuwa amehiari kutuongoza kwa miaka mingine mitano (2020/2021 - 2024/2025) basi tukubali kwa wingi wetu kumchagua na kulinda kura zake ili zisihujumiwe na mahasimu wake wa kisiasa.
Nawasilisha kwa hatua zenu hapo 28/10