Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli hajawahi kushindwa, hatashindwa

Wakuu, salaam!

Nawakumbusha tu kwamba John Pombe Magufuli hajawahi kushindwa na haitatokea ashindwe - mara zote akiwa mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki na baadae Chato iwe ndani ya CCM au uchaguzi mkuu hakuwahi kushindwa na haitatokea ashindwe.

Katika uchaguzi tunaoenda kuufanya tarehe 28 Oktoba, 2020 bado anapambana lkn usitegemee atashindwa - sababu za kutoshindwa ziko nyingi:-

(i). Uwezo binafsi na Ubunifu:-
Haikuwa kazi nyepesi kusimamia ongezeko la mapato ya Serikali kutoka takriban 800B - 1.3T kwa mwezi (ni fedha hizi zimewezesha utekelezaji wa miradi mikubwa kwa midogo i.e viwanja vya ndege, ndege, meli, vivuko, maji, hospital na vituo vya afya, elimu bure nk nk);

(ii). Ziara za ndani:-
Wakati wote ametumia muda mwingi kufanya ziara za kikazi ndani ya mikoa tofauti na utamaduni wa viongozi wengi ambao leo wakinywa chai Ufaransa mchana hula UK - hii imemjengea sifa kubwa kwa wananchi na kuwa ktk orodha wa viongozi wanaoaminiwa;

(iii). Usimamizi wa matumizi ya fedha za umma:-
Hapa kila mmoja ni shahidi kwamba hata zile kelele za ufisadi zilizokuwa zinapigwa zimepungua sana - ingawa anapaswa kuendelea kumulika zaidi kwa watendaji wake ili wasiingize masuala binafsi kwenye utendaji wa kila siku;

(iv). Ajali za barabani - zimepungua sana tofauti na miaka kadhaa ya nyuma;

Kwa ujumla sifa za kiungozi anazo nyingi, kama kuna kasoro sehemu basi ni zile za kibinadamu ambazo kila mmoja anazo.

Rai yangu:-
Kwa kuwa amehiari kutuongoza kwa miaka mingine mitano (2020/2021 - 2024/2025) basi tukubali kwa wingi wetu kumchagua na kulinda kura zake ili zisihujumiwe na mahasimu wake wa kisiasa.

Nawasilisha kwa hatua zenu hapo 28/10
Safari hii anaangukia Pua bila huruma yoyote
 
Umri wangu huujui
Hatuna watoto jamii forum, hatuna vichaa jamii forum na wala hatuna vikongwe/wazee jamii forum

Tutumie lugha za staha kufikisha ujumbe tutaelewana - kwa kuwa hata angeshinda mgombea mwingine zaidi ya JPM bado watanzania wanapaswa kuwa wamoja
 
Naomba nikwambie kuwa magufuli hakuwahi kushinda wala kushindwa kwa kuwa ni muoga kuingia kwenye ushindani ,nasi watanzania tutamwadhibu kwa makosa yafuatayo

1. Kuiba na kula rambirambi
2. Wizi wa 1.5 trillion
3. Ukandamizaji wa haki za binadamu
4. Ubaguzi
5. Uongo na ahadi zisizotekelezeka mfano Noah kwa kila mtanzania na zile 50 mln kwa kila kijiji
6. Utekaji na mauaji
7. Kujificha wakati wa majanga mfano covid19 na Ajali ya MV nyerere
8. Udhalilishaji wa wanawake majukwaani
9. Hajatimiza moja ya masharti ya kugombea urais yanayosema kuwa lazima mgombea ajue "kuongea na kuandika kiswahili na kingereza kwa ufasaha"
10. Ameiba aridh huko karagwe 25000 hekari
Atashinda sasa
 
Sifa zingine zinatolewa na wasiojua kufikiri. Hebu fikiri... kuanzia aanze shule ufaulu wake ulikuwaje? Hajawahi kushindwa? Mialiko yote hajawahi kushindwa kufika? Matatizo yote anayoletewa kutatua, je hajawahi kushindwa? Hata kutongoza, hajawahi kataliwa na na mwanamke? Sio kushindwa? Hata alipoanza kugombea ubunge, alishindwa mara ngapi?

ACHA KUMKUFURU MUNGU....
Siku zinahesabika:-
- andaeni orodha ya wasimamizi/mawakala wenu siku saba kabla ya tarehe ya uchaguzi na kiyawasilisha kwa DG NEC

- pigeni kula mpigavyo,
- lindeni kura,
Mwisho wa siku JPM lzm ashinde
 
Si alishindwa mara mbili 1985 na 1990 kura za maoni ndani ya CCM jimbo la Biharumulo.au kushindwa kupi unakokuzungumzia.
 
Naomba nikwambie kuwa magufuli hakuwahi kushinda wala kushindwa kwa kuwa ni muoga kuingia kwenye ushindani ,nasi watanzania tutamwadhibu kwa makosa yafuatayo

1. Kuiba na kula rambirambi
2. Wizi wa 1.5 trillion
3. Ukandamizaji wa haki za binadamu
4. Ubaguzi
5. Uongo na ahadi zisizotekelezeka mfano Noah kwa kila mtanzania na zile 50 mln kwa kila kijiji
6. Utekaji na mauaji
7. Kujificha wakati wa majanga mfano covid19 na Ajali ya MV nyerere
8. Udhalilishaji wa wanawake majukwaani
9. Hajatimiza moja ya masharti ya kugombea urais yanayosema kuwa lazima mgombea ajue "kuongea na kuandika kiswahili na kingereza kwa ufasaha"
10. Ameiba aridh huko karagwe 25000 hekari
Hizo porojo zako hazigusi hata 2% ya wapiga kura. Andaa propaganda nyingine muda sio rafiki
 
Muda ni rafiki, tarehe ya kuapishwa rais wetu iko wazi - hata kama mmemuibua Sheikh ponda lkn lzm ashinde JPM
 
kuna jamaa alisema PHD ya MA.... ikaguliwe mbn hatumuoni huyo jaman yuko wap
 
Muda ni rafiki, tarehe ya kuapishwa rais wetu iko wazi - hata kama mmemuibua Sheikh ponda lkn lzm ashinde JPM
Ukitaka kuchangia kwenye maoni ya mtu, jitahidi kusoma original post na maoni mengine utaelewa zaidi na kuweza kuongezea maoni juu ya maoni ya mwingine. Ushauri wangu ni huo.
 
Sawa ndugu Buberwa - let us start counting days remaining to face such general election - JPM kishashinda
 
Wakuu, salaam!

Nawakumbusha tu kwamba John Pombe Magufuli hajawahi kushindwa na haitatokea ashindwe - mara zote akiwa mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki na baadae Chato iwe ndani ya CCM au uchaguzi mkuu hakuwahi kushindwa na haitatokea ashindwe.

Katika uchaguzi tunaoenda kuufanya tarehe 28 Oktoba, 2020 bado anapambana lkn usitegemee atashindwa - sababu za kutoshindwa ziko nyingi:-

(i). Uwezo binafsi na Ubunifu:-

Haikuwa kazi nyepesi kusimamia ongezeko la mapato ya Serikali kutoka takriban 800B - 1.3T kwa mwezi (ni fedha hizi zimewezesha utekelezaji wa miradi mikubwa kwa midogo i.e viwanja vya ndege, ndege, meli, vivuko, maji, hospital na vituo vya afya, elimu bure nk nk);

(ii). Ziara za ndani:-

Wakati wote ametumia muda mwingi kufanya ziara za kikazi ndani ya mikoa tofauti na utamaduni wa viongozi wengi ambao leo wakinywa chai Ufaransa mchana hula UK - hii imemjengea sifa kubwa kwa wananchi na kuwa ktk orodha wa viongozi wanaoaminiwa;

(iii). Usimamizi wa matumizi ya fedha za umma:-

Hapa kila mmoja ni shahidi kwamba hata zile kelele za ufisadi zilizokuwa zinapigwa zimepungua sana - ingawa anapaswa kuendelea kumulika zaidi kwa watendaji wake ili wasiingize masuala binafsi kwenye utendaji wa kila siku;

(iv). Ajali za barabani
- zimepungua sana tofauti na miaka kadhaa ya nyuma;

Kwa ujumla sifa za kiungozi anazo nyingi, kama kuna kasoro sehemu basi ni zile za kibinadamu ambazo kila mmoja anazo.

Rai yangu:-

Kwa kuwa amehiari kutuongoza kwa miaka mingine mitano (2020/2021 - 2024/2025) basi tukubali kwa wingi wetu kumchagua na kulinda kura zake ili zisihujumiwe na mahasimu wake wa kisiasa.

Nawasilisha kwa hatua zenu hapo 28/10
Kama Mungu muumba wa mbingu na nchi aishivyo Magufuli atashindwa. Mungu hadhihakiwi
 
Back
Top Bottom