Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Miaka mitano ijayo tutawakatia bima ya Afya Wananchi wote wa Tanzania

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Miaka mitano ijayo tutawakatia bima ya Afya Wananchi wote wa Tanzania

Akizidiwa anafyatua ahadi hewa. Uchaguzi uliopita aliahidi kila kijiji elfu 50. Ziko wapi?
Ni Million 50 mkuu sio elfu 50
Alihaidi na Laptop kwa kila mwalimu, na Noah kwa kila Mtanzania ziko wapi sijui..
 
Lissu alisema haya kwenye ufunguzi wa kampeni zake Mataga wakasema haiwezekani maana hata Obama Care ilishindwa Marekani, Leo kimempata nini tena huyu mkurupukaji?
Kimempata kitu!
 
Lissu alisema haya kwenye ufunguzi wa kampeni zake Mataga wakasema haiwezekani maana hata Obama Care ilishindwa Marekani, Leo kimempata nini tena huyu mkurupukaji?
Chadema waliposema elimu bure walicheka na kudhihaki
Slaa aliposema ataleta treni ya umeme walicheka mpaka wakawa hawana mbavu
Lissu aliposema bima ya afya kwa kila mtu wakasema hajui uchumi
Vitambulisho vya machinga ni issue nyingine hati hata bank unakopa kumbe havina hata majina
Majimbo ndio wanapotosha hadi siku mtu wao ata....... basi itakuwa vigelegele. Ni maisha tu.
 
Hiyo sera hawataiweza Kama sera ya elimu bila malipo kwasababu chadema wameficha kwenye ilani yao jinsi watavyoimplement ili atayekopy ashindwe, You can copy ideas but not results ndo wazungu walisema, ndo maana wajanja huwa wanaomba maridhiano ya vyama mbadala ili mashirikiane kujenga nchi.
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amesema kwa miaka mitano ijayo wakipata ridhaa kutoka kwa wananchi watakata bima ya afya kwa kila Mwananchi.

Amesema kwanza walikuwa wanaboresha miundombinu na kwa miaka mitano anayoimaliza tayari wameshajenga hospitali na vituo vya afya vya kutosha zoezi linalofuata ni kuwakatia bima watu wote milino 60 waliopo Tanzania.

Amesema jambo la kumpa bima kila mwananchi linawezekana kwa kuwa wanafahamu hela za kutimiza hilo watakapozitoa.

Amesema hadi sasa wameshaajiri madaktari zaidi ya 1,000 na watumishi wa afya zaidi ya 14,000. Anasema wamepanga kwa kuwa wanajua watakavyotekeleza.
Hatudanganyiki. Ungetimiza baadhi ya mambo yanayowahusu wananchi wako kipindi cha kwanza tungekuwa na imani nawe, ulionesha kutotujari kwa kebehi, dharau na vitisho eti leo watudanganya waziwazi hahaha.
Mdomo wenye ndimi mbilimbili😂😂
 
1. Ahadi ya 50,000,000/- kila Kijiji na Mtaa:
50000000x17582 = trilioni 8.79/-

2. Ahadi ya Bima ya Afya (tuchukue yenye gharama ndogo (30,000/-) ambayo ni "Improved Community Health Fund" (iCHF)
30000x60000000 = trilioni 18/-

Je, ahadi namba 1 hapo juu imetekelezwa? Na kama haijatekelezwa kwanini?

Kama ahadi namba 1 hapo juu ambayo gharama yake ni ndogo kuliko ahadi namba 2, je, anaweza kutekeleza ahadi namba 2 kweli? Au ndio msemo usemao "Wajinga ndio waliwao"?

Ndugu watanzania, jaribuni kutumia japo kidogo kufikirisha ubongo wenu juu ya ahadi za aina hii.
Pesa inaenda kwa Boeing alete ndege mpya ilihali dunia nzima usafiri wa anga unasuasua na mashirika yanapata hasara

Welcome to Tanzania
 
Kwanza NHIF warudishe huduma zote walizozifuta ambazo awali tulikuwa tunazipata kwa bima za kawaida ndipo tuelekee huko kwenye ahadi mpya
Huyo jamaa hajawahi kutimiza ahadi zake ,mambo anayofanya ni kwenye miradi ni kwa ajili ya upigaji tu...Bima haina Upigaji kwahiyo hatotimiza.
 
Jamaa ana akili sana.Ukisema hamjaongezwa mishahara miaka 5, ana ahidi kuongeza.Kwani mmesahau Lowassa alisema bure Shule za chekechea hadi university, Hutu akasema Primary hadi .... hivyo, bima nchi nzima, sijui tutaumizwa wapi, Elimu bure tunakatwa katika vocha za salio ambazo nyuma hatukuwahi katwa
 
Uziri huu huu uzi utakuwepo hadi 2025
 
View attachment 1607817

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amesema kwa miaka mitano ijayo wakipata ridhaa kutoka kwa wananchi watakata bima ya afya kwa kila Mwananchi.

View attachment 1607816
Amesema kwanza walikuwa wanaboresha miundombinu na kwa miaka mitano anayoimaliza tayari wameshajenga hospitali na vituo vya afya vya kutosha zoezi linalofuata ni kuwakatia bima watu wote mili60 waliopo Tanzania.

View attachment 1607815
Amesema jambo la kumpa bima kila mwananchi linawezekana kwa kuwa wanafahamu hela za kutimiza hilo watakapozitoa.

Amesema hadi sasa wameshaajiri madaktari zaidi ya 1,000 na watumishi wa afya zaidi ya 14,000. Anasema wamepanga kwa kuwa wanajua watakavyotekeleza.
View attachment 1607814
Katika hili wote wawili Rais Magufuli na Mh Tundu Lissu ni waongo na wanawatapeli wapumbavu.
Wote wawili hawana uwezo huo
Wanasiasa wetu ni uchwara hasa...pole sana wapiga kura
 
Back
Top Bottom