Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Miaka mitano ijayo tutawakatia bima ya Afya Wananchi wote wa Tanzania

Akizidiwa anafyatua ahadi hewa. Uchaguzi uliopita aliahidi kila kijiji elfu 50. Ziko wapi?
Ni Million 50 mkuu sio elfu 50
Alihaidi na Laptop kwa kila mwalimu, na Noah kwa kila Mtanzania ziko wapi sijui..
 
Lissu alisema haya kwenye ufunguzi wa kampeni zake Mataga wakasema haiwezekani maana hata Obama Care ilishindwa Marekani, Leo kimempata nini tena huyu mkurupukaji?
Kimempata kitu!
 
Lissu alisema haya kwenye ufunguzi wa kampeni zake Mataga wakasema haiwezekani maana hata Obama Care ilishindwa Marekani, Leo kimempata nini tena huyu mkurupukaji?
Chadema waliposema elimu bure walicheka na kudhihaki
Slaa aliposema ataleta treni ya umeme walicheka mpaka wakawa hawana mbavu
Lissu aliposema bima ya afya kwa kila mtu wakasema hajui uchumi
Vitambulisho vya machinga ni issue nyingine hati hata bank unakopa kumbe havina hata majina
Majimbo ndio wanapotosha hadi siku mtu wao ata....... basi itakuwa vigelegele. Ni maisha tu.
 
Hiyo sera hawataiweza Kama sera ya elimu bila malipo kwasababu chadema wameficha kwenye ilani yao jinsi watavyoimplement ili atayekopy ashindwe, You can copy ideas but not results ndo wazungu walisema, ndo maana wajanja huwa wanaomba maridhiano ya vyama mbadala ili mashirikiane kujenga nchi.
 
Hatudanganyiki. Ungetimiza baadhi ya mambo yanayowahusu wananchi wako kipindi cha kwanza tungekuwa na imani nawe, ulionesha kutotujari kwa kebehi, dharau na vitisho eti leo watudanganya waziwazi hahaha.
Mdomo wenye ndimi mbilimbili😂😂
 
Pesa inaenda kwa Boeing alete ndege mpya ilihali dunia nzima usafiri wa anga unasuasua na mashirika yanapata hasara

Welcome to Tanzania
 
Kwanza NHIF warudishe huduma zote walizozifuta ambazo awali tulikuwa tunazipata kwa bima za kawaida ndipo tuelekee huko kwenye ahadi mpya
Huyo jamaa hajawahi kutimiza ahadi zake ,mambo anayofanya ni kwenye miradi ni kwa ajili ya upigaji tu...Bima haina Upigaji kwahiyo hatotimiza.
 
Jamaa ana akili sana.Ukisema hamjaongezwa mishahara miaka 5, ana ahidi kuongeza.Kwani mmesahau Lowassa alisema bure Shule za chekechea hadi university, Hutu akasema Primary hadi .... hivyo, bima nchi nzima, sijui tutaumizwa wapi, Elimu bure tunakatwa katika vocha za salio ambazo nyuma hatukuwahi katwa
 
Uziri huu huu uzi utakuwepo hadi 2025
 
Katika hili wote wawili Rais Magufuli na Mh Tundu Lissu ni waongo na wanawatapeli wapumbavu.
Wote wawili hawana uwezo huo
Wanasiasa wetu ni uchwara hasa...pole sana wapiga kura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…