Akihutubia jimbo la Kawe, Rais Magufuli amesema yeye ni Binadamu hataweza kwenda lindi na Mtwara hivyo atamtuma Kassim Majaliwa Kassim
Mimi kama mwana CCM naunga mkono kumtumia Mama Salma Kikwete na Jakaya Kikwete mikoa ya lindi na Mtwara na tayari hilo limefanyika.
Kwa uamuzi huu Rais ameona mbali sana na hongera kwake sana sana,
Wale wa maeneo ya Ngende, Nanjilinji na Nkanared na wale wanaotamka mwana Nke badala ya Mwanamke na mnaotamka Ntoto badala ya mtoto wa mikoa ya Lindi na Mtwara tunawategemea sana kupiga kura ya ndio kwa JPM.
Kazi za serikali ni nyingi zinahitaji muda pia.
----
Nilipenda sana kupita maeneo mbalimbali. Nilipenda nifike Mbagala; nitamtuma Mheshimiwa Jakaya Kikwete. Nilipanga niende mpaka Ukonga mwisho, napo nitamtuma Mh. Jakaya Kikwete na viongozi wengine.
Nilipanga kupita kila eneo, lakini mimi ni binadamu. Ningependa hata nifike Katavi na Rukwa lakini ilibidi nimtume Makamu wangu wa Rais, Mama Samia.
Ningependa nifike Mtwara na Lindi lakini nitamtuma kule Waziri Mkuu wangu, Ndugu Kassim Majaliwa.
Ningependa nifike Morogoro; ningependa nifike Pwani; ningependa nifike Pemba na maeneo mengine. Mimi ni binadamu, siwezi kuwa kila mahali na wakati huohuo nifanye kazi za serikali. Kwasababu serikali lazima iendelee kwenda, wafanyakazi wapate mishahara yao. Madawa lazima yapatikane hospitali. Na mengine mengi. Wakulima lazima wapate pembejeo. Hatya yote unayasimamia wakati ukifanya kampeni.
Unaamini ni kazi za kiserikali zimekuwa nyingi? Huyu raisi kuna wakati huwa anakera sana ila ukimsikia Lisu anavyombomoa, unaanza kumwonea huruma.Duu! Kwa hiyo amehodhi kila kitu lazima afanye yeye? Mbona Mkapa na Kikwete walifanya kampeni nchi nzima na serikali iliendelea kufanya kazi kama kawaida.
Kumbuka nchi hii hatupo kwenye hali ya hatari kiasi kwamba Rais anahitajika kila sekunde!
Nimeuliza tu kama mtanzania yeyote, ninayesikiliza sera za 'maendeleo hayana vyama'..Mbona una maneno makali sana?
Bado kuna watu watakupinga hapa. Na hiyo NEC ndo inafumba macho na masikio kabisa hapo.Anafanya makosa makubwa ya kumwingiza Waziri Mkuu kwenye jimbo ambalo sio lake. NEC mpo wapi?
Lakini kapiga magotiAlafu kampeni za. Mwaka huu jamaa ameepwaya sana yani hata zile PUSHAPU hapigi kabisa.
Lakini kapiga magoti
VyoteYeye ni binadamu kwa hiyo atakuwa amechoka au yeye ni binadamu kuna nafsi inamsuta?
Kuzimia tuu au jehanamu kabsaa???Afya imetetereka.
Anajifanya anaenda na mwendo wa Lissu,atazimia!
Jiwe limetepeta, hakuna mkate mgumu mbele ya chai, kakutana na size yakeLeo sio jiwe tena
Ushauri mzuri Sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Huyu kuna kitu anatuficha. Akilazimisha kupita tutarudia uchaguzi bora astaafu
Huo mstari wa mwisho sijaupenda kabsa!Kiukweli
Ukiwa karibu kabisa (physically) na Mhe. Rais unaona amepungua Sana na kuchoka KIMWILI.
Namtakia kila la kheri amalize hizi mbio salama
Mitano ya ny..ok.oTumekuelewa Mh. Rais ,
Mitano tena kwa JPM.
Yote mawili yanamhusu!Yeye ni binadamu kwa hiyo atakuwa amechoka au yeye ni binadamu kuna nafsi inamsuta?
Duuh....!Umeweka kinafiki sana hii kitu..
..anajua kuna mambo mabaya amewatendea.
..hana ujasiri wa kuonana na wananchi wa kusini.