tweenty4seven
JF-Expert Member
- Sep 21, 2013
- 15,863
- 19,626
Angekua na akili chato ingekua na maendeleo kawa mbunge miaka 25 alichoweza ni kuweka traffic light kuvushia ngombe na punda
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna Tofauti kati ya akili ya magufuli na ya Nabii Tito. Kama Nabii Tito ana akili basi kweli Magufuli ana akili sana!Habari za wasaa huu watanzania wenzangu ndugu na marafiki kwaajumla.
Natumai mu wazima wa afya njema kabisa na mnaendelea vizuri na kujituma katika kazi zenu za kila siku.
Sasa leo nitaenda kumzungumzia huyu mwamba Magufuli kwa mapana na marefu zaidi ili sote tupate kumwelewa.
Bila kumumunya maneno, ukianza kuzungumzia na kutafakari kwa kina juu ya mwamba Magufuli na Tanzania ya sasa utakuja kugundua na kuhitimisha kwamba huyu mwamba ni kiongozi mwenye akili nyingi haijawai kutokea katika taifa hili.
1. Mwamba Magufuli ana shahada ya elimu ya sayansi yaani Bachelor katika somo la namba na kemia kwa kizungu tunasema Bachelor of Science of Education in Mathematics and chemistry. Kwa hiyo unapozungumzia swala la namba hapo ndio zimelala yaani, kemia hii ya kuchanganya makemikali ndio huwezi kumdanganya kitu.
2. Ana shahada ya uzamili katika fani ya kemia kwa kizungu wanaita masters of science in chemistry. Kwa hiyo unapozungumzia wakemia duniani basi lazima umzungumzie na huyu mwamba. Pia ana shahada ya uzamivu katika fani ya kemia tena. Kwa kizungu wanaita PhD in Chemistry. Basi unapo zungumzia kuhusiana na sayansi ya chemistry yoyote hapo ndio imelala kwa huyu mwamba.
3. Sasa huyu mwamba ukimwangalia vizuri na kutafakari kwa kina unakuja kugundua kwamba ana akili nyingi mno za kuzaliwa nazo, utakuja kugundua ana kipaji cha uongozi yaani karama ya uongozi. Anakipaji cha kusimamia. Anakipaji cha kuyaelewa mambo kwa uharaka kwa speed ya 5G na kuyachukulia hatua stahiki. Ana hekima. Hekima ndio inabeba mazagazaga yote, Ndani ya hekima kuna kila kitu. Ndani ya hekima kuna akili za kupambanua na kutafakari mambo, ndani ya hekima kuna akili za kutatua matatizo mbalimbali, ndani ya hekima ndio kuna akili ya kumucha Mungu aliyeziumba Mbingu na nchi na vyote vilivyomo ndani yake, ndani ya hekima ndio kuna kuna akili ya kutambua kwamba kahuna jambo linaloshindikana tukimwomba Mungu, ndani ya hekima kuna ujuzi na Maarifa ya kila namna (historia, sheria, geographia, math, science, economics, judging, problem solving n.k), ndani ya hekima kuna busara. Ndani ya hekima kuna akili za kuyaelewa mambo ambayo hujayasomea darasani au popote.
4. Nasema hivyo kwasababu huyu mwamba hajasomea masomo ya sanaa, Lakini anajua vitu vingi mnoo, hauwezi kumdanganya. Anajua na kuielewa historia, anajua na kuielewa sheria na ipo kichwani, mambo ya utalii ndio usiseme anayajua vilivyo, anajua kuongoza, anaijua geographia ya dunia nzima, anajua kusimamia majukumu, anajua na kuuelewa uchumi, anajua na kuilewa vilivyo elimu ya fedha, anajua na kuyaelewa mambo ya kodi, anajua na kuzielewa vizuri mbinu zote na janja janja za mafirisi, anajua na Kuzielewa vilivyo mbinu zote za mebeberu laghai na makwepa kodi, anajua na Kuelewa vizuri janjajanja zote za mafisadi, watakatishaji wa fedha, majizi, anajua na kuyaelewa mambo ya mapato na matumizi. Mambo ya kubajeti hapo ndio kabisa Magufuli yupo makini mnooooo.
5.Magufuli ni kiongozi anayeweza kuongoza (lead), kufuatilia (monitoring) na kusimamia (manage) viongozi wa kila wizara kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu na kwa kujituma bila kuchoka.
6.Wizara ya afya yumo, wizara ya ujenzi yumo, wizara ya elimu yumo, wizara ya kilimo yumo, wizara ya ulinzi yumo, Kwenye Maliasiri yumo, TRA yumo, Bandarini yumo, TAZARA yumo, Michezo yumo, wizara ya fedha yumo, kwenye miradi yumo, kwenye dini yumo, kwenye hekima yumo, kwenye umeme yumo, kwenye sheria yumo, kwenye lugha yumo, kwenye chemistry yumo, kwenye mathematics yumo, kwenye madawa yumo. Kuishinda corona yumo.
7.Kuyazidi kete mabeberu yumo, kugundua mbinu wanazotumia watu wanaokwepa kodi yumo, kuweka mbinu bora za kuzuia wakwepa kodi yumo, kuyashinda mabeberu kupambana na corona yumo. Kuzungumza lugha za kila aina yumo.
8.Kukusanya kodi za kuendeshea serikali kwa ufanisi yumo, kutafuta fedha za kuendeshea serikali bila kutegemea mabeberu yumo. Kusimamia miradi kwa ufanisi na kuzuia ubadhilifu na ufisadi wa pesa za miradi yumo.
9. Kuboresha viwanja vyetu vya ndege kama ulaya yumo, kuwaza jinsi ya kufanya watanzania wote watibiwe hapahapa Tanzania yumo. Kuyazidi mabeberu kete yumo. Kupiga stori za maendeleo na wananchi yumo.
10. Kugundua janja janja za mabeberu na mafilisi katika kuiba rasilimali za nchi yumo. Kuyapa displine mabeberu ambayo yanakwepa kodi na kufanya unyonyaji wa rasilimali zetu yumo.
11. Kutokuyaogopa mabeberu yumo. Kugundua matakatishaji ya fedha za miradi za serikali yumo, kugundua majitu yanayotaka kupata au kutoa rushwa yumo, kutoa elimu bure yumo, kujenga hosteli vyuoni yumo, kujenga babara za juu na za rami yumo.
12. Kugundua mbinu wanazotumia majizi kutuibia mapato bandarini yumo. Kuyazuia majizi yasituibie mapato bandarini yumo, Kugundua mbinu wanazotumia majizi kutuibia madini yumo, kuyazuia majizi yasituibie madini yetu yumo.
Nitaendelea bado sijamaliza nataka kujaza page kama 100 hivi.
Na mtanzania mwaminifu.
Bila kuondoa chuki utaishia kutazama tu ila hutaona.Mleta mada umeandika upuuzi mtupu.
Chief kumbe umekapata kaujumbe vilivyoHakuna Tofauti kati ya akili ya magufuli na ya Nabii Tito. Kama Nabii Tito ana akili basi kweli Magufuli ana akili sana!
Haaaaaa kumbe umekapata kaujumbe chiefSema ana akili nyingi zaidi yako na baba yako 😝
Thank you EllySkyWillyMama D zawadi yangu leo kwako ni hii moja.
Wooooowwwwwww
Kama makao mkuu ya chama chao chenye umri wa zaidi ya miaka 28 ni haya uwaelewe tuu kwamba wao ni wa hivyo.Hua situmii lugha za matusi kwenye nyuzi zangu chief. Naomba tujibizane kwa hoja tu inatosha. Tuachane na matusi.
Imedhihirika kumbe anaposema hivyo anakuwa anadanganya na hivyo kuonyesha kuwa yeye ni mpenzi wa shetaniNimeanika ukweli hadharani. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu
Tumia akili tu kuwafanya wenye nguvu watende kwa ajili yako.Nguvu na akili vinakwenda pamoja sasa wewe kaaa tu ndani bila kutumia nguvu kutafuta pesa utegemee zitakuja zenyewe thubutu, lazima utumie nguvu.
Kwani ameandika kuhusu nini mkuu. Maana ameandika maandishi mengiMleta mada umeandika upuuzi mtupu.
Kwanini chiefKwenye kilimo hapana!
Wala sijapata ugumu kuandika yaaniHakika usemayo asilimia 100%