Dkt. Magufuli, Rais Bora Afrika kwa mwaka 2019

Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza, Tuzo ya Mo Ibrahimu hutolewa kwa marais wastaafu sio waliopo madarakani
Shukurani kwa kukumbusha,Na siyo kutojua.Ila hata akistaafu hata 3 bora hapati. Rekodi chafu!
 
Kama ubora unapimwa kwa mambo hayo basi hatukuwa na sababu ya kuwafukuza wakoloni Kwani ndio walioleta reli na Elimu Afrika
 
Ushahidi ni kuwa hakuna popote zoezi limeendeshwa la kumpata rais bora ndani ya hili bara, au popote kuhusu kiongozi bora wa Afrika.
Unapaswa kujiongeza sio kila kitu usubirie kuanzishiwa, Tumia Elimu yako kupima na kufikiri. Rais wako kwa maendeleo
 
Shukurani kwa kukumbusha,Na siyo kutojua.Ila hata akistaafu hata 3 bora hapati. Rekodi chafu!
Mabeberu hawawezi kumpa Tuzo lakini wazalendo tutampatia tuzo
 
VAPS,
Awamu ya kwanza (2015-2020) ilikuwa kujenga miundo mbinu, Yaani nyenzo za maendeleo au maendeleo ya vitu, awamu ya pili (2020-2025) ni maendeleo ya watu. Hizi changamoto ndogo zitatatuliwa zote, tumuunge mkono akamalizie kazi.
Usije kuwa uko ndotoni mkuu, tunamuungaje mkono?
 
Bajeti anatekeleza kwa asilimia ngapi?hapo ndipo ubora wa rais ulipolala
 
Usije kuwa uko ndotoni mkuu, tunamuungaje mkono?
Unga mkono kwa 1. Kulipa kodi, 2. Kuchapa kazi, 3. Kuwa mzalendo kwa kuitangaza nchi na serikali vizuri na 4. Kumchagua tena akakamilishe kazi
 
Mabeberu hawawezi kumpa Tuzo lakini wazalendo tutampatia tuzo

Nyie sio wazalendo bali ni wafaidika binafsi wa madaraka yake. So mnachikifanya ni kuhalalisha ugali wenu.
 
Sasa unafail, kama unasema umoja wa kitaifa umeimarika!!!. Unaonyesha mahaba ya dhairi kabisa na nyekundu unaiita nyeusi
 
VAPS,
Awamu ya kwanza (2015-2020) ilikuwa kujenga miundo mbinu, Yaani nyenzo za maendeleo au maendeleo ya vitu, awamu ya pili (2020-2025) ni maendeleo ya watu. Hizi changamoto ndogo zitatatuliwa zote, tumuunge mkono akamalizie kazi.

Miradi yake mikubwa ni SGR & SG, yote hadi sasa haijafika robo ya malengo, sasa hiyo 2020-2025 iwapo atachezea uchaguzi ili aendelee kukaa madarakani atafanya nini?
 
Vipi kuhusu Rais Ahmed wa Ethiopia aliyeshinda tuzo ya amani ya Nobel
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…