Dkt. Magufuli, Rais Bora Afrika kwa mwaka 2019

Dkt. Magufuli, Rais Bora Afrika kwa mwaka 2019

Mabeberu hawawezi kumpa Tuzo lakini wazalendo tutampatia tuzo
ILI MABEBERU WAWEPO SI LAZIMA WAWEPO MAJIKE, AU MAJIKE YANAWEZA ISHI / HAYAHITAJI MABEBERU?
Msitari unaotofautisha "ubeberu"na "ubia" wa maendeleo upo wapi? Maana hamchelewi kubadilika kama vinyonga.
 
Unga mkono kwa 1. Kulipa kodi, 2. Kuchapa kazi, 3. Kuwa mzalendo kwa kuitangaza nchi na serikali vizuri na 4. Kumchagua tena akakamilishe kazi
1. Mnakata PAYE 600K plus kodi kwa kila bidhaa na huduma ninayonunua 2. Ningekuwa sifanyi kazi ningekula mawe 3. Uzalendo ni zaidi ya kuisema nchi kwa mazuri 4. Umeingiza siasa na kuanza kampeni mapema sana, sikujua kama kuna umuhimu wa kumchagua tena kwani watangaza matokeo ni wa kwake.
 
Nyie sio wazalendo bali ni wafaidika binafsi wa madaraka yake. So mnachikifanya ni kuhalalisha ugali wenu.
Mimi ni mfaidika nawewe pia ktk yafuatayo
1. Huduma za afya
2. Miundo mbinu
3. Elimu bure
4. Ulinzi na usalama
5. Riba nafuu ya mikopo ktk mabenki
N.k
 
1. Mnakata PAYE 600K plus kodi kwa kila bidhaa na huduma ninayonunua 2. Ningekuwa sifanyi kazi ningekula mawe 3. Uzalendo ni zaidi ya kuisema nchi kwa mazuri 4. Umeingiza siasa na kuanza kampeni mapema sana, sikujua kama kuna umuhimu wa kumchagua tena kwani watangaza matokeo ni wa kwake.
Unamaanisha atapita bila kupingwa?
 
Vipi kuhusu Rais Ahmed wa Ethiopia aliyeshinda tuzo ya amani ya Nobel
Huo ni ujinga, unashinda tuzo ya amani lakini kila siku RAIA wako wanakamatwa wakikimbia nchi kwa maisha magumu?
Beberu akikupa Tuzo, jiulize ulipokosea, akikunyima endeleza unapopatia.
Maisha ya Ethiopia magumu sana, hiyo tuzo INA umuhimu gani?. Sisi tunajenga nchi, Tuzo yetu maendeleo ya Taifa.
 
ILI MABEBERU WAWEPO SI LAZIMA WAWEPO MAJIKE, AU MAJIKE YANAWEZA ISHI / HAYAHITAJI MABEBERU?
Msitari unaotofautisha "ubeberu"na "ubia" wa maendeleo upo wapi? Maana hamchelewi kubadilika kama vinyonga.
Tunajenga miundo mbinu ya kiuchumi ili Taifa lijitegemee, Tuchape kazi Taifa lisonge mbele.
 
Huenda mimi ndio sijui maana ya ubora. Kama hivyo ulivyotaja ndio vinatoa rais bora, basi mbona marais wengi wa Afrika watakuwa bora? Maana ukiangalia hiyo list yako marais wengi wametekeleza kama sehemu ya majukumu yao. Ni vyema ungesema vitu Magufuli alivyotekeleza, ila suala la ubora ndani ya Afrika achana nalo. Ubora ni zaidi ya hivyo vitu vilivyo kwenye list yako. Ukumbuke na kuweka deni la taifa kwenye kipindi chake, ili tupime vizuri.

we jamaa kwa kwel kama ni upinzani dam dam mwaka 2019 ulistahili kupewa tuzo, kila mada ya ccm ama magu sidhan kama sjaona umechangia, na hakuna sehem ata moja umempa hongera magufuli kila sehem upinzani, daaah uko vizuri baba lao
 
Mimi ni mfaidika nawewe pia ktk yafuatayo
1. Huduma za afya
2. Miundo mbinu
3. Elimu bure
4. Ulinzi na usalama
5. Riba nafuu ya mikopo ktk mabenki
N.k

  1. Natibiwa hospitali binafsi
  2. Miundombinu iko toka yeye hajawahi rais
  3. Hakuna mtoto wangu anasoma shule ya bure.
  4. Ulinzi na usalama upo hata kabla yeye hajaingia madarakani, na hata akitoka ni huduma zitakazoendelea kuwepo.
  5. Hakuna riba nafuu huko kwenye mabenki, acha maneno ya kitapeli
Narudia tena, sio rais bora fullstop.
 
we jamaa kwa kwel kama ni upinzani dam dam mwaka 2019 ulistahili kupewa tuzo, kila mada ya ccm ama magu sidhan kama sjaona umechangia, na hakuna sehem ata moja umempa hongera magufuli kila sehem upinzani, daaah uko vizuri baba lao

Sitoagi hongera kwa watu wa sampuli hiyo.
 
Sitoagi hongera kwa watu wa sampuli hiyo.

kila mtu ana upande wake mmbaya, dont take everything emotionally, just be legite to life: no hate just challenges, at the end life has to move on with all the negatives, hata upinzani wana negative side zao including the ones in public na zingine hatujui, same to ccm, life cant be perfect but kwenye kupewa hongera unatoa tu kiroho safi na penye kukosoa same same
 
Kwani JPM siyo rais wa jamhuri ya Tanzania?

Kwanini mnasema ni rais bora Afrika wakati hatukufanya uchaguzi ama sijui nini ili kutafuta rais bora wa Afrika?

Penye ukweli ni lazima usemwe, kwani siku hizi takwimu zote hutolewa na serkali, wewe za kwako umezipikia wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kila mtu ana upande wake mmbaya, dont take everything emotionally, just be legite to life: no hate just challenges, at the end life has to move on with all the negatives, hata upinzani wana negative side zao including the ones in public na zingine hatujui, same to ccm, life cant be perfect but kwenye kupewa hongera unatoa tu kiroho safi na penye kukosoa same same

Huwa natoa hongera sana tu, labda hujafuatilia mada zangu zote. Ila mpaka nimsifie kazi ipo. Hata hivyo wasifiaji ni wengi, hivyo mimi nisipomsifia sioni kama kuna shida yoyote, ili mradi simtukani.
 
we jamaa kwa kwel kama ni upinzani dam dam mwaka 2019 ulistahili kupewa tuzo, kila mada ya ccm ama magu sidhan kama sjaona umechangia, na hakuna sehem ata moja umempa hongera magufuli kila sehem upinzani, daaah uko vizuri baba lao
Hata mie sioni cha kusifia. Nisifie alhali anazidi kutufanya wadeni sugu????!!!!
 
Kwa vigezo vinavyoonekana na kupimika, Mheshimiwa Magufuli ndiye RAIS BORA barani Afrika kwa mwaka 2019. Nina sababu 20 ambao ni Ushahidi wa ubora wa Magufuli ukimlinganisha na maraisi wengine wote wa Afrika:

1. Amefufua shirika la ndege lililokufa kwa kununua ndege mpya 8 kwa pesa taslimu
2. Amekarabati shule kongwe, vyuo vya ualimu na kupeleka ruzuku ya elimu bure mashuleni.
3. Ameboresha ulinzi wa rasilimali kwa kukomesha ujangili
4. Amedhibiti biashara ya madawa ya kulevya
5. Ameboresha sheria na mikataba ya madini hivyo kuongeza pato la Taifa
6. Ameboresha uzalishaji na utendaji wa mashirika ya umma hivyo kwa sasa yanatoa gawio serikalini badala ya kuomba ruzuku
7. Amedumisha ulinzi na usalama nchini hivyo kukomesha ujambazi na mipaka IPO salama hakuna chokochoko za majirani
8. Amejenga hospitali mpya za wilaya na mikoa na kuboresha vituo vya afya, zahanati na huduma za afya hivyo idadi ya wagonjwa kupelekwa India imepungua
9. Ameboresha mfumo wa ajira serikalini kwa kudhibiti rushwa katika sekretarieti ya ajira, sasa vijana kutoka kaya maskini wanapata ajira bila upendeleo
10. Amefungua milango ya uhamisho kwa wahadhili vyuo vikuu hivyo kuondoa upendeleo, ubabe wa maprofesa vyuoni
11. Amedhibiti asasi za kihuni nchini zilizokuwa zinaeneza uharibifu na mmomonyoko katika jamii
12. Amerudisha nidhamu serikalini na heshima katika jamii hivyo hakuna urasimu wala umangimeza
13. Amedhibiti utoroshaji wa madini kwa kujenga ukuta mererani na kuimarisha ulinzi
14. Ameboresha huduma za bandari na sasa ni kimbilio kwa wafanyabiashara wa ndani na nje
15. Ameimarisha usafiri uliokufa mfano Reli ya Tanga, Tazara na reli ya kati, sasa ujenzi wa standard gauge
16. Amerejesha mahusiano ya kimataifa yaliyopotea mfano Israel na Morocco
17. Amedhibiti safari za nje kwa viongozi hivyo kuokoa fedha za kigeni.
18. Ameongeza makusanyo ya kodi hivyo kuimarisha uwezo wa Taifa kujitegemea.
19. Amepunguza kiwango cha umaskini na kukuza uchumi kama takwimu za benki ya dunia zinavyoonesha.
20. Amerejesha heshima ya nchi kimataifa, sasa watanzania tunatembea kifua mbele ndani na nje ya nchi.

TUNAKUTAKIA AFYA NjEMA KATIKA MWAKA 2020, HATA KAMA WAPIGA DILI HAWATA KUPONGEZA, SISI WAZALENDO TUPO PAMOJA NAWE, KUKUUNGA MKONO NA KUKUOMBEA
we kweli timu JPM/Kichaa. yani amemzidi hata KENYATA?
yeye anazungumzia kujenga SGR mwenzake ilishajengwa na inatumika.
JPM anaua wapinzani wake (lisu) mwenzake anapatana nao (raila odinga)
Fikiria kama raila ndo angekuwa mpinzani wa JPM afu akajiapisha kuwa raisi leo angekuwepo duniani? (rejea maneno yake JPM ya kifedhuli alipoizuru Zanzibar)
 
Jibu hoja-'Wakati gani wanakuwa mabeberu na lini wanakuwa wabia?"
Wanapotuibia, kupora rasilimali zetu na kitukopesha kwa masharti magumu wanakuwa mabeberu, wanapounga mkono juhudi za maendeleo bila hila wala masharti, hapo ni wabia
 
Huo ni ujinga, unashinda tuzo ya amani lakini kila siku RAIA wako wanakamatwa wakikimbia nchi kwa maisha magumu?
Beberu akikupa Tuzo, jiulize ulipokosea, akikunyima endeleza unapopatia.
Maisha ya Ethiopia magumu sana, hiyo tuzo INA umuhimu gani?. Sisi tunajenga nchi, Tuzo yetu maendeleo ya Taifa.
Duh....cha njombe
 
Back
Top Bottom