Ni ngumu sana kujua Magufuli ni Mtu Wa namna gani...anaweza akaamka akawaambia kuwa "maendereo hayana chama" au "Mimi ni raisi Wa Watanzania wote na ninawapenda sana ndugu zangu au nasema uongo jamaniii!!"
sasa siku akiamka na maruhani kichwani utachoka mwenyewe kumsikiliza kwa pumba atakazotoa, yaani hapo CCM ndio chama cha maana vingine takataka, hapo Maendeleo yanakuwa na chama (yanawahusu wavaa nguo za kijani tu) vyama vingine vinakuwa mashetani...hebu angalia hiki kituko, Wazungu wakitupa misaada ya kifedha anawaita "Wahisani wetu wa maendereo hawa!"
At the same time haohao waliompa pesa wakimshauri au wakitoa takwimu zinazogusa maslahi yake anawaita "Mabhebheru hawa". Dah! Ni ngumu sana kujua huyu mtu kichwa chake kipoje.
Wewe mwenyewe umesema kichwa chake kina maruhani halafu unatuuliza kichwa chake kikoje!!
Kwanini hamtaki kusema ukweli nani aliyempa URAIS Jiwe; Vasco Dagama mtu wake alikuwa Membe sasa ili kumkomoa VascoDagama na kulipiza kisasi cha kumsaliti hapo indipo Lowassa alipocheza karata ya kumuangusha Membe walipofika TANO bora!! Walipobakia watatu wafuasi wa Lowassa wakambeba JIWE na ndio akapata kuteuliwa 2015!!! Umewahi kumsikia Jiwe hata siku moja akimdhihaki Lowassa? Anajua fika nani alimpa huo ulaji.