Dkt. Makame: Hakuna haja ya kumsafirisha Mstaafu Mwinyi kwa matibabu kwasasa (Tumuombee)

Rais mstaafu wa awamu ya pili wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi anaendelea kupatiwa matibabu ya kifua akiwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari bingwa

"Anaendelea kupatiwa matibabu na baadhi ya wakati anakuwa na uangalizi wa karibu sana wa madaktari na wamesema kwamba wataendelea kumpa matibabu kwa hapa, hakuna haja kwa sasa ya kumsafirisha labda kama wataona haja ya kufanya hivyo hapo baadaye kwa sababu na umri pia umesogea kidogo lakini mimi chakusema tu ni kwamba tumuombee mzee wetu, tufanye dua, tumuombee aweze kuimarika afya yake na aweze kutoka katika hali hiyo ya maradhi ili aungane na sisi tena tuendelee kupata faida kutoka kwake" -Dkt. Makame

Dkt. Abdallah Makame aliyekuwa Katibu wa Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi amezungumza hayo alipofanya mahojiano maalumu na Azam TV Februari 15.2024
Mwenyezi Mungu amjalie ahuweni na uponyaji kiongozi wetu huyu mahiri wa kiswahili na Rais wetu mpendwa sana wa awamu ya2 ndrugo A. H. Mwinyi

R.I.P Laigwanani comrade ENL
 
Dkt. Abdallah Makame aliyekuwa Katibu wa Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi amezungumza hayo alipofanya mahojiano maalumu na Azam TV Februari 15.2024
Kuna fumbo hapo kwanini aliyekuwa? Kwanini asizungumze aliyepo?
 
Mzee kaacha maelekezo apelekwe mkulanga, Wai wana taka kumpeleka Zanzibar.
👉 I mean no malice to nobody, maandalizi mkulanga.
FB_IMG_17080784396200395.jpg
FB_IMG_17080784442920427.jpg
 
Mzee kaacha maelekezo apelekwe mkulanga, Wai wana taka kumpeleka Zanzibar.
👉 I mean no malice to nobody, maandalizi mkulanga.
View attachment 2905740View attachment 2905742
Bosi, hii ni barabara ya halmashauri (yenye lami iliyokolea)inaunganisha ofisi ya DC na ile ya DED. Barabara hii imeanza kujengwa tangu mwaka jana miezi ya katikati. Aidha, hiyo barabara yenye ranging iliyopauka ni barabara ya Kisiju (imejengwa mwaka juzi).Kwahiyo, ni vyema tukawa tunasupport hoja zetu kwa mifani isiyo na shaka hata punje. Ahsante
 
Rais mstaafu wa awamu ya pili wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi anaendelea kupatiwa matibabu ya kifua akiwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari bingwa

"Anaendelea kupatiwa matibabu na baadhi ya wakati anakuwa na uangalizi wa karibu sana wa madaktari na wamesema kwamba wataendelea kumpa matibabu kwa hapa, hakuna haja kwa sasa ya kumsafirisha labda kama wataona haja ya kufanya hivyo hapo baadaye kwa sababu na umri pia umesogea kidogo lakini mimi chakusema tu ni kwamba tumuombee mzee wetu, tufanye dua, tumuombee aweze kuimarika afya yake na aweze kutoka katika hali hiyo ya maradhi ili aungane na sisi tena tuendelee kupata faida kutoka kwake" -Dkt. Makame

Dkt. Abdallah Makame aliyekuwa Katibu wa Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi amezungumza hayo alipofanya mahojiano maalumu na Azam TV Februari 15.2024
Mwinyi mdogo asikilize wosia wa baba yake asimpangie wapi pa kupumzishwa; muda umekwenda!
 
Ila hii mambo ya kuombea vifo viwapate high ranking ccm official inabidi wajitafakari sana hawa viongozi. Hii sio kawaida.
 
Kama kawaida saikolojia inachukua nafasi yake kuandaa wananchi kupokea taarifa muda ukiwadia
 
Tunasubiri kumaliza msiba wa Edward then tutatangaza!
Acha upuuzi sijui Miafrika mengine yakoje aise. Mnapenda sana taarifa za umbea na uzushi.

Mzee Mwinyi yupo anaendelea na matibabu na yule ni muislamu hawana ujinga wa kuficha msiba kama upande mwingine.
 
Ila hii mambo ya kuombea vifo viwapate high ranking ccm official inabidi wajitafakari sana hawa viongozi. Hii sio kawaida.

Watz wanatatizo Sana na sio ccm mara nyingi Ta huwaombea WATU hata ambao hawana maslahi nao
 
Mwenyezi Mungu ampe unafuu Mzee wetu. Ametutoa mbali toka kupanga foleni na kadi ya kaya kununua sukari ya ugawaji {NMC},chawa,kunguni funza,viroboto kutokana na ukosefu wa sabuni na mafuta,kusikiliza RTD mpaka kuangalia CNN,BBc,DStv Azam kuvaa kaniki na midabwada yenye viraka pamoja na kutembea peku mpaka Sasa kuwa na machaguo ya nguo na viatu.

Watu wanamiliki magari binafsi kuanzia salon mpaka mamia ya magari,maroli,mabasi mpaka ndege yote ni matokeo ya maamuzi magumu ya kubadili mfumo wa nchi
mbooa unatoa wasifu? Muda bado
 
Back
Top Bottom