Dkt. Manguruwe matatani, asomewa mashtaka 28 ya utapeli, uhujumu Uchumi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mr. Manguruwe yamemkuta huko.

Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd, Simon Mkondya (40) maarufu kwa jina la Dkt. Manguruwe na mwenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiballiwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 28.

Katika kesi hiyo, Mkondya na Mwenzake Rweyemamu John ambaye ni Mkaguzi wa kiwanda hicho wanakabiliwa na mashtaka 19 ya upatu na mashtaka tisa ya kutakatisha viwanja vilivyopo huko Njombe eneo la Idunda.
1730817774303.png
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Job Mrema mbele ya Hakimu Mkazi Aaron Lyamuya inadai washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya January Mosi 2020 na Desemba 2023 jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika kipindi hicho Mkondya akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla pamoja na mkaguzi wake huyo walifanya biashara ya upatu kwa kuwaahidi watu kuwa ukitoa kiasi chochote cha pesa utapata faida mara tatu ya kiasi ulichotoa.
1730817809968.png
Inadaiwa washitakiwa walijipatia jumla ya Sh Milioni 92.2 kutoka kwa watu kumi na tisa tofauti ikiwa kila mmoja alimpatia kiasi chake cha fedha akimuahidi kuwa fedha hizo zingezaa mara tatu ya zile alizotoa.

Katika mashtaka tisa ya utakatishaji mshtakiwa Mkondya peke yake anadaiwa katika kipindi hicho hicho, akiwa ndani ya Mkoa wa Dar es salaam alijipatia jumla ya viwanja tisa vitalu namba Ab vilivyopo eneo la Idunda Mkoani Njombe huku akijua kuwa viwanja hivyo ni mazalia ya kosa tangulizi la upatu.
1730817866650.png
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19,2024 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Mshtakiwa amerudishwa rumande.
Soma, Pia: Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake
 
Attachments

  • 1730811743852.png
    1730811743852.png
    1.6 MB · Views: 12
Mr. Manguruwe yamemkuta huko.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla International Limited, Saimon Mnkondya, akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo kusomewa mashtaka 28 ya kuendesha Biashara ya Upatu, utakatishaji fedha, Uhujumu Uchumi pamoja na kujipatia Viwanja mbalimbali ambapo alikuwa akipokea pesa kutoka kwa watu na kudai atawapa faida ya pesa zaidi.
Soma, Pia: Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake
Kawa motivate Masheikh na Maustaadhi wakimbilie kufuga nguruwe, kumbe yeye mwenyewe kilichomtoa na kumfanya asikike mjini siyo nguruwe
 
Huyu alikuwa amevumiliwa Sana maana alikuwa anatapeli wazi wazi sijui watu wamekuwa na hela Sana au ujinga umeongezeka .

So sad watu wanaumizwa kwa mambo ambayo wangeyakwepa.

Mfano kuhusu UPATU . hii sio mara ya kwanza watu wanatapeliwa.
 
Na atachomoka atarudi kuwapiga wajinga tena
Hizi media zinatumiwa sana kuwakuza

Ova
 
Huyu Tapeli amejitahidi sana kula na Vipofu, lakini kujipendekeza kwa viongozi kulikozidi kiwango kulinifanya nielewe kwamba kuna analolificha

View attachment 3144430View attachment 3144431
Mimi nasema usimtilie mashaka bali kuwa na uhakika kuwa huyo siyo mtu mzuri. Narudia tena: mtaani ukiona mtu anajipendekeza sana kwa CCM na viongozi wake basi moja kwa moja huyo mtu ana makandokando mengi. NB: Waliotapeliwa na huyu jamaa nao ni wajinga kweli kweli.
 
Mr. Manguruwe yamemkuta huko.

Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd, Simon Mkondya (40) maarufu kwa jina la Dkt. Manguruwe na mwenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiballiwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 28.

Katika kesi hiyo, Mkondya na Mwenzake Rweyemamu John ambaye ni Mkaguzi wa kiwanda hicho wanakabiliwa na mashtaka 19 ya upatu na mashtaka tisa ya kutakatisha viwanja vilivyopo huko Njombe eneo la Idunda.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Job Mrema mbele ya Hakimu Mkazi Aaron Lyamuya inadai washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya January Mosi 2020 na Desemba 2023 jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika kipindi hicho Mkondya akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla pamoja na mkaguzi wake huyo walifanya biashara ya upatu kwa kuwaahidi watu kuwa ukitoa kiasi chochote cha pesa utapata faida mara tatu ya kiasi ulichotoa.
Inadaiwa washitakiwa walijipatia jumla ya Sh Milioni 92.2 kutoka kwa watu kumi na tisa tofauti ikiwa kila mmoja alimpatia kiasi chake cha fedha akimuahidi kuwa fedha hizo zingezaa mara tatu ya zile alizotoa.

Katika mashtaka tisa ya utakatishaji mshtakiwa Mkondya peke yake anadaiwa katika kipindi hicho hicho, akiwa ndani ya Mkoa wa Dar es salaam alijipatia jumla ya viwanja tisa vitalu namba Ab vilivyopo eneo la Idunda Mkoani Njombe huku akijua kuwa viwanja hivyo ni mazalia ya kosa tangulizi la upatu.
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19,2024 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Mshtakiwa amerudishwa rumande.
Soma, Pia: Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake

Debe tupu, haliachi kutika. Mshana Jr alitahadharisha hapa..hakuna mtu mwenye hela halafu ana kelele. Hela zinajieleza zenyewe.

Ukiona mtu anatamba mji mzima ana hela, muogope kama ukoma. hana hizo hela anazosema. Kuna mengi nyuma ya pazia.

Kuna yule mmoja anasumbua sana. Usiku mmoja nikaona msafara unatembea huku uswekeni magari yote yana jina lake. Nikamkumbuka Mshana
 
Back
Top Bottom