Dkt. Manguruwe matatani, asomewa mashtaka 28 ya utapeli, uhujumu Uchumi

Huyu alikuwa amevumiliwa Sana maana alikuwa anatapeli wazi wazi sijui watu wamekuwa na hela Sana au ujinga umeongezeka .

So sad watu wanaumizwa kwa mambo ambayo wangeyakwepa.

Mfano kuhusu UPATU . hii sio mara ya kwanza watu wanatapeliwa.
Makonda juzi juzi alikuwa anamjoki sana eti wawekezaji kama hawa tusiwa-disturb maana wameajiri watu wengi sana ,halafu kuna watu wawili walipelekwa kama chambo tu ili aingizwe kwenye 18.
 
tunarudi kulekule ukiona tajiri anakuwa chawa jua kuna dhambi anafunika

huyu jamaa alikuwa analazimisha umaarufu
 
Mr. Manguruwe yamemkuta huko.

Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd, Simon Mkondya (40) maarufu kwa jina la Dkt. Manguruwe na mwenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiballiwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 28.

Katika kesi hiyo, Mkondya na Mwenzake Rweyemamu John ambaye ni Mkaguzi wa kiwanda hicho wanakabiliwa na mashtaka 19 ya upatu na mashtaka tisa ya kutakatisha viwanja vilivyopo huko Njombe eneo la Idunda.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Job Mrema mbele ya Hakimu Mkazi Aaron Lyamuya inadai washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya January Mosi 2020 na Desemba 2023 jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika kipindi hicho Mkondya akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla pamoja na mkaguzi wake huyo walifanya biashara ya upatu kwa kuwaahidi watu kuwa ukitoa kiasi chochote cha pesa utapata faida mara tatu ya kiasi ulichotoa.
Inadaiwa washitakiwa walijipatia jumla ya Sh Milioni 92.2 kutoka kwa watu kumi na tisa tofauti ikiwa kila mmoja alimpatia kiasi chake cha fedha akimuahidi kuwa fedha hizo zingezaa mara tatu ya zile alizotoa.

Katika mashtaka tisa ya utakatishaji mshtakiwa Mkondya peke yake anadaiwa katika kipindi hicho hicho, akiwa ndani ya Mkoa wa Dar es salaam alijipatia jumla ya viwanja tisa vitalu namba Ab vilivyopo eneo la Idunda Mkoani Njombe huku akijua kuwa viwanja hivyo ni mazalia ya kosa tangulizi la upatu.
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19,2024 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Mshtakiwa amerudishwa rumande.
Soma, Pia: Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake
Plea bargain itamuokoa...
 
Huyu alikuwa amevumiliwa Sana maana alikuwa anatapeli wazi wazi sijui watu wamekuwa na hela Sana au ujinga umeongezeka .

So sad watu wanaumizwa kwa mambo ambayo wangeyakwepa.

Mfano kuhusu UPATU . hii sio mara ya kwanza watu wanatapeliwa.
Daa! Kweli wajinga ndio waliwao. Ni kama DESI. Halafu anajitangaza hadi kwenye redio za dini, kama WAPO Radio.
 
Ajapata dhamana,na pia kesi ya uhujumu uchumi ina dhamana,ila mara nyingi unalipa robo tatu ya kiaisi cha ghalama ya iyo case, Ila hao jamaa wana kesi pia ya money laundaring
Huyo jamaa ili atoke kwenye plea bargain awalipe watu wote aliowatapeli.
 
Unapotafuta pesa kuna njia nyingi binadamu unaweza kupitia kama kutapeliwa, kuibiwa na kukutana na kadhia mbalimabali. Hao jamaa hawakupenda kutapeliwa ila Kuna muda huyu jamaa kama alikua verified hivi.. kwani kipindi mambo hayo anayafanya hadharani mamlaka zilikuwa wapi. Tena jamaa alipewa airtime na vyombo vikubwa vya habari. Kwa muktadha huo ilikua raisi watu kuingizwa mkenge
 
Hakuna hela rahisi duniani, kupenda urahisi na tamaa ndio watu hugeuzwa futsa.

Ngoja nianze kuwaletea utajiri wa majini ya bermuda na mimi niwapige hela.
 
Jamaa una chuki na uislam mbwa wewe,wapi kawatapeli masheikh hapo?
Ndiyo unavyojidanganya kuwa nina chuki? Unajikasirisha mpaka akili zinakutoka na kushindwa kuelewa kilichoandikwa. Mimi na Waislam ni damdam , one love, hata ndani ya familia tuna waislam wa kutosha, ila siyo waliojitwika imani kipuuzi kama wewe, lazima mnichukie, uwe Muislam, uwe Myahudi, uwe Mkristo , uwwe msomi au haujasoma ili mradi ukiwa mpuuzi tu lazima unichukie sababu lazima nikupe knucles za kutosha.
 
Mr. Manguruwe yamemkuta huko.

Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd, Simon Mkondya (40) maarufu kwa jina la Dkt. Manguruwe na mwenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiballiwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 28.

Katika kesi hiyo, Mkondya na Mwenzake Rweyemamu John ambaye ni Mkaguzi wa kiwanda hicho wanakabiliwa na mashtaka 19 ya upatu na mashtaka tisa ya kutakatisha viwanja vilivyopo huko Njombe eneo la Idunda.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Job Mrema mbele ya Hakimu Mkazi Aaron Lyamuya inadai washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya January Mosi 2020 na Desemba 2023 jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika kipindi hicho Mkondya akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla pamoja na mkaguzi wake huyo walifanya biashara ya upatu kwa kuwaahidi watu kuwa ukitoa kiasi chochote cha pesa utapata faida mara tatu ya kiasi ulichotoa.
Inadaiwa washitakiwa walijipatia jumla ya Sh Milioni 92.2 kutoka kwa watu kumi na tisa tofauti ikiwa kila mmoja alimpatia kiasi chake cha fedha akimuahidi kuwa fedha hizo zingezaa mara tatu ya zile alizotoa.

Katika mashtaka tisa ya utakatishaji mshtakiwa Mkondya peke yake anadaiwa katika kipindi hicho hicho, akiwa ndani ya Mkoa wa Dar es salaam alijipatia jumla ya viwanja tisa vitalu namba Ab vilivyopo eneo la Idunda Mkoani Njombe huku akijua kuwa viwanja hivyo ni mazalia ya kosa tangulizi la upatu.
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19,2024 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Mshtakiwa amerudishwa rumande.
Soma, Pia: Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake
Scandal ya vanilla imeibuka.
 
Back
Top Bottom