Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
Mi nadhani angepewa muda tuone atafanyaje kwa hao 13, ila angezuiwa kuongeza watuAlisema anakufanyia shughuli zote mnagawana faida tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi nadhani angepewa muda tuone atafanyaje kwa hao 13, ila angezuiwa kuongeza watuAlisema anakufanyia shughuli zote mnagawana faida tu.
Huwa iko hivo mbona.Ukiona mtu ni tajiri nyuma yake kuna Madudu mengi,uchawi,kafara,utapeli,madawa ya kulevya,misukule nk
Wapi amedhaminiwa????Kesi za uhujumu uchumi zina dhamana siku hizi?
Wajinga ndio tuliwaoUtajiri una Siri nyingi
Kaficha alafu kaachia,upuuzi gani huuHivi kwanini watuhumiwa hupenda kuficha sura zao pindi wanapokuwa mahakamani?
Mwenye kujua hii anisaidie plz
Hiyo sio kesi ya nguruwe ni ya Vanilla kwani pia alikuwa na Vanilla Village huyo. Aliwapiga sana wajinga huko.Mr pork watu walikuwa wanamtumia hela ili awafugie mifugo ambayo wameinunua ikae hapo hapo, hela kumbe anabunya
Mr. Manguruwe yamemkuta huko.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd, Simon Mkondya (40) maarufu kwa jina la Dkt. Manguruwe na mwenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiballiwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 28.
Katika kesi hiyo, Mkondya na Mwenzake Rweyemamu John ambaye ni Mkaguzi wa kiwanda hicho wanakabiliwa na mashtaka 19 ya upatu na mashtaka tisa ya kutakatisha viwanja vilivyopo huko Njombe eneo la Idunda.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Job Mrema mbele ya Hakimu Mkazi Aaron Lyamuya inadai washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya January Mosi 2020 na Desemba 2023 jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa katika kipindi hicho Mkondya akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla pamoja na mkaguzi wake huyo walifanya biashara ya upatu kwa kuwaahidi watu kuwa ukitoa kiasi chochote cha pesa utapata faida mara tatu ya kiasi ulichotoa.
Inadaiwa washitakiwa walijipatia jumla ya Sh Milioni 92.2 kutoka kwa watu kumi na tisa tofauti ikiwa kila mmoja alimpatia kiasi chake cha fedha akimuahidi kuwa fedha hizo zingezaa mara tatu ya zile alizotoa.
Katika mashtaka tisa ya utakatishaji mshtakiwa Mkondya peke yake anadaiwa katika kipindi hicho hicho, akiwa ndani ya Mkoa wa Dar es salaam alijipatia jumla ya viwanja tisa vitalu namba Ab vilivyopo eneo la Idunda Mkoani Njombe huku akijua kuwa viwanja hivyo ni mazalia ya kosa tangulizi la upatu.
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka DPP.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19,2024 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Mshtakiwa amerudishwa rumande.
Soma, Pia: Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake
Hiyo sio kesi ya nguruwe ni ya Vanilla kwani pia alikuwa na Vanilla Village huyo. Aliwapiga sana wajinga huko.
Na akitoka atawapiga tena na hao wote waliyopigwa hawastahili kulipwa na hawatolipwa..maana mazuzu tuWatu wamepigwa kiboya sana
Ule ni utapeli wa wazi kabisa.Vanilla almanusura nijichangnye aseee😄
Wakusanyaje pesa kwenye sandarusi halafu wanakwambia nimeziona tu kwenye accountDaa! Kweli wakinga ndio waliwao. Ni kama DESI. Halafu anajitangaza hadi kwenye redio za dini, kama WAPO Radio.
Haya haina shida kuwa na kazi njema tajiri.Ali piga sana, 92m ? Hela gani hiyo
ATI kilo Moja inanunuliwa tsh 1,000,000/=akiulizwa soko liko wapi!kimya,nikuuzia zangu!kimya,eti lete hela nikulimie,haya shamba liko wapi!kimya,ama anasema ni la mfano Afrika yote,Vanilla almanusura nijichangnye aseee😄
Mtoa post ya awali kabla haijafanyiwa editing alisema DR manguruwe akitoka mahakamani.Wapi amedhaminiwa????