Dkt. Manguruwe matatani, asomewa mashtaka 28 ya utapeli, uhujumu Uchumi

Mr. Manguruwe yamemkuta huko.

Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd, Simon Mkondya (40) maarufu kwa jina la Dkt. Manguruwe na mwenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiballiwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 28.

Katika kesi hiyo, Mkondya na Mwenzake Rweyemamu John ambaye ni Mkaguzi wa kiwanda hicho wanakabiliwa na mashtaka 19 ya upatu na mashtaka tisa ya kutakatisha viwanja vilivyopo huko Njombe eneo la Idunda.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Job Mrema mbele ya Hakimu Mkazi Aaron Lyamuya inadai washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya January Mosi 2020 na Desemba 2023 jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika kipindi hicho Mkondya akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla pamoja na mkaguzi wake huyo walifanya biashara ya upatu kwa kuwaahidi watu kuwa ukitoa kiasi chochote cha pesa utapata faida mara tatu ya kiasi ulichotoa.
Inadaiwa washitakiwa walijipatia jumla ya Sh Milioni 92.2 kutoka kwa watu kumi na tisa tofauti ikiwa kila mmoja alimpatia kiasi chake cha fedha akimuahidi kuwa fedha hizo zingezaa mara tatu ya zile alizotoa.

Katika mashtaka tisa ya utakatishaji mshtakiwa Mkondya peke yake anadaiwa katika kipindi hicho hicho, akiwa ndani ya Mkoa wa Dar es salaam alijipatia jumla ya viwanja tisa vitalu namba Ab vilivyopo eneo la Idunda Mkoani Njombe huku akijua kuwa viwanja hivyo ni mazalia ya kosa tangulizi la upatu.
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19,2024 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Mshtakiwa amerudishwa rumande.
Soma, Pia: Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake
Hivi watu kama hawa wakibainika na makosa ya jinai hawawezi kunyongwa.....sheria ya nchi inasemaje juu yao?
 
Mfanyabiashara Simon Mkondya maarufu kama Dk Manguruwe (40) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 28 ikiwemo utakatishaji wa fedha wa Shilingi Milioni 90.

Manguruwe ambaye pia ni Mmiliki wa Kampuni ya Vanilla International Ltd amefikishwa mahakamani na mwenzake Rweymamu Joh (59) ambaye ni Mkaguzi wa Kampuni hiyo.

Hata hivyo, wawili hao wamekosa dhamana kutokana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokuwa na mamlaka ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19, huku washtakiwa wakipelekwa mahabusu.

Wawili hao wamesomewa mashtka yao na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya ambapo wanadaiwa walitenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Januari mosi mwaka 2020 na Disemba mosi mwaka 2023 ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo ilidaiwa kwamba mashitaka 19 ni ya kufanya biashara ya upatu ,ambapo katika kipindi hicho Mkondya akiwa kama Mkurugenzi na John akiwa kama mfanyakazi wa kampuni hiyo walifanya biashara ya upatu kwa kuwaahidi watu kupata faida mara mbili hadi tatu kulingana ya kiasi cha fedha watakazotoa.

Ilidaiwa kwamba, washitakiwa hao walijipatia kiasi cha jumla ya sh milioni 92.2 kutoka kwa watu 19 tofauti ambapo watu hao walitoa kiato tofauti cha fedha ambapo aliwaahidi watapata faida mara mbili hadi tatu ya fedha walizotoa.

Iliendelea kudaiwa kwamba, mashitaka tisa ni ya utakatishaji yanayomkabili mshitakiwa Mkondya pekee ambapo kati ya Januari mosi mwaka 2020 na Desemba mosi 2023, akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni hiyo alijipatia jumla ya viwanja 9 kitalu namba AB eneo la Idunda mkoani Njombe huku akijua viwanja hivyo ni mazalia ya makosa tangulizi ya upatu.

Baada ya kusomwa mashitaka hayo, Wakili Mrema alidai kutokana na mashitaka yanayowakabili, Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza hivyo washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote.

#KitengeUpdates
 
Attachments

  • 1730826477322.jpg
    1730826477322.jpg
    297.7 KB · Views: 4
Watanzania wa Vichwa vigumu sijawah ona...juzi tu Mr Kuku aliwapiga watu ila hawakuelewa.

Serikali iache wajinga waendelee kupigwa ili wapate akili
 
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu
Sasa kama walijua mahakama yenyewe haina mamlaka ya kusikiliza hiyo kesi kwanini waliipeleka kesi hapo?
 
Debe tupu, haliachi kutika. Mshana Jr alitahadharisha hapa..hakuna mtu mwenye hela halafu ana kelele. Hela zinajieleza zenyewe.

Ukiona mtu anatamba mji mzima ana hela, muogope kama ukoma. hana hizo hela anazosema. Kuna mengi nyuma ya pazia.

Kuna yule mmoja anasumbua sana. Usiku mmoja nikaona msafara unatembea huku uswekeni magari yote yana jina lake. Nikamkumbuka Mshana
Yule ana hela
 
Mr. Manguruwe yamemkuta huko.

Mkurugenzi Mwanzilishi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd, Simon Mkondya (40) maarufu kwa jina la Dkt. Manguruwe na mwenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiballiwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 28.

Katika kesi hiyo, Mkondya na Mwenzake Rweyemamu John ambaye ni Mkaguzi wa kiwanda hicho wanakabiliwa na mashtaka 19 ya upatu na mashtaka tisa ya kutakatisha viwanja vilivyopo huko Njombe eneo la Idunda.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Job Mrema mbele ya Hakimu Mkazi Aaron Lyamuya inadai washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya January Mosi 2020 na Desemba 2023 jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika kipindi hicho Mkondya akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla pamoja na mkaguzi wake huyo walifanya biashara ya upatu kwa kuwaahidi watu kuwa ukitoa kiasi chochote cha pesa utapata faida mara tatu ya kiasi ulichotoa.
Inadaiwa washitakiwa walijipatia jumla ya Sh Milioni 92.2 kutoka kwa watu kumi na tisa tofauti ikiwa kila mmoja alimpatia kiasi chake cha fedha akimuahidi kuwa fedha hizo zingezaa mara tatu ya zile alizotoa.

Katika mashtaka tisa ya utakatishaji mshtakiwa Mkondya peke yake anadaiwa katika kipindi hicho hicho, akiwa ndani ya Mkoa wa Dar es salaam alijipatia jumla ya viwanja tisa vitalu namba Ab vilivyopo eneo la Idunda Mkoani Njombe huku akijua kuwa viwanja hivyo ni mazalia ya kosa tangulizi la upatu.
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19,2024 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Mshtakiwa amerudishwa rumande.
Soma, Pia: Dkt. Manguruwe anyooshewa kidole akidaiwa kufanya utapeli kwa baadhi ya wateja walioitikia kuwekeza kwenye kampuni yake
Hawa matapeli ndio wanaotuharibia vijana kwa kujifanya wajuwaji kumbe wahuni na WEZI tu!
 
Debe tupu, haliachi kutika. Mshana Jr alitahadharisha hapa..hakuna mtu mwenye hela halafu ana kelele. Hela zinajieleza zenyewe.

Ukiona mtu anatamba mji mzima ana hela, muogope kama ukoma. hana hizo hela anazosema. Kuna mengi nyuma ya pazia.

Kuna yule mmoja anasumbua sana. Usiku mmoja nikaona msafara unatembea huku uswekeni magari yote yana jina lake. Nikamkumbuka Mshana
Ukiona mtu anatamba mji mzima ana hela, muogope kama ukoma. hana hizo hela anazosema. Kuna mengi nyuma ya pazia.🥍
 
Back
Top Bottom