GE2025 Dkt. Marcus Alban: Kuzuia Uchaguzi ni Kosa Kubwa katika Taifa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hawa ndio wasomi vilaza ukisikia.anadhani uchaguzi ni kwenda kupiga kura tu. Hizi shule walienda kusomea ujinga.
 
Mpumbavu huyo
 

..lakini Ccm nao kwa kushirikiana na polisi, msajili, mahakama, na watumishi wa serikali, wanatumia njia mbalimbali za haramu kupoka haki za wengine wakati wa uchaguzi.

..kwa mfano, kuna Wazanzibari wanaotaka kutumia haki yao ya kushiriki katika uchaguzi, lakini wamenyimwa haki hiyo, kwa kuzuiliwa isivyo halali, kupata kitambulisho cha Mzanzibari.

..Kwa maoni yangu, Ccm ndio wanaozuia uchaguzi, wana historia hiyo, na wanazo nyenzo za kufanya hivyo. Hali hiyo ni tofauti na wengine wanaotishia kuzuia uchaguzi, lakini hawana uwezo.
 
Ukiandamana siku ya "uchaguzi" ambao kiukweli si uchaguzi ni kama unautambua na kuu validate huo uchaguzi kuwa upo.

Wapinzani walitakiwa kuwahamasisha wananchi wakae nyumbani siku hiyo wasitoke kwenye uchaguzi, voter participation ishuke mpaka kuwa chini ya 5%.

Hapo dunia ingeona watu wamesusia uchaguzi.

Upinzani umeshindwa katika hilo.
 
Naam.

Sasa kwa nini wapinzani wakiulizwa strategy yenu ni ipi wanashindwa kuelezea?
Kuna kitu umeshindwa kukielewa. NRNE campaigns zimekuwa halted na watawala approximately four months ago. Kimsingi, CHADEMA (a duly registered political party) imeshazuiliwa kufanya shughuli za kisiasa. Wapinzani wataufikia umma kueleza strategies zao kwa kutumia jukwaa lipi?
 
Kama CHADEMA imeshindwa kuwa mobilize watu kuwakabili watawala kwenye NRNE, kuwezesha NRNE irudi, hapo maana yake ineshindwa uongozi.

CHADEMA imeshindwa hata ku mobilize wananchi kuisusia CRDB iliyoharibu imani ya watu kwa kuwapotezea fedha zao, this was a golden opportunity.

Unategemea vipi wataweza mambo ya kuleta mabadiliko katika nchi?
 
It’s none of our business; we leave that to CHADEMA. No need to stand in their way!
 
It’s none of our business; we leave that to CHADEMA. No need to stand in their way!
It's none of your business wakati wewe ndiye umeanza kuwataja CHADEMA hapa?

Sasa kama CHADEMA is none of your business umewataja wa nini?

Si ungewaacha tu utuambie what your business is.

You are contradicting yourself.
 
It's none of your business wakati wewe ndiye umeanza kuwataja CHADEMA hapa?

Sasa kama CHADEMA is none of your business umewataja wa nini?

Si ungewaacha tu utuambie what your business is.

You are contradicting yourself.
Ukiacha Mtanzania mmoja mmoja mpenda haki, CHADEMA ndiye amekuwa political victim number moja. This isn’t debatable. Kwa kutambua ukweli huu, I cannot (in good conscience) stand in their way!

CHADEMA na wapenda haki wengine wanayo haki ya kufanya uasi dhidi ya sheria kandamizi kwa namna wanayoona inafaa.
 
Sawa.

Lakini nani anaamua ipi ni sheria kandamizi na ipi si sheria kandamizi?

Nani anaamua hii ni sheria kandamizi lakini tutaikabili mahakamani au vinginevyo kisheria au/na kwa amani, na hii ni sheria kandamizi tutaikabili kwa kufanya fujo?

Kwa kipimo gani?

Peter Madeleka alikuwa CHADEMA, CHADEMA wakagomea uchaguzi, yeye akaona atapoteza haki yake ya kikatiba ya kuchaguliwa, akaenda ACT Wazalendo anagombea ubunge.

Ana haki ya kikatiba ya kuchaguliwa.

In principle anaweza kushinda uchaguzi na kuwa mbunge. Akaendeleza ndoto zake na kufichua anachotaka Bungeni. Akasaidia mabadiliko bungeni.

Peter Madeleka si CCM.

Sasa huoni ukilazimisha uchaguzi usifanyike, kwa nguvu, bila kujali haki za wengine waliotofautiana na wewe kifalsafa tu, ambao hata si CCM, unawanyima Peter Madeleka na wenzake haki zao za kugombea ubunge, hili jambo haliiathiri CCM tu?
 
Vitu vingine ni common sense except pale mtu anapoamua kujizima data. Ni mtu gani wa kawaida, kwa mfano, atakayekubaliana na sheria inayosema referee wa match ya Yanga v Simba atateuliwa na Yanga? Au atateuliwa na Simba?

Kuna baadhi ya watu wanadhani huu ni mchezo wa bahati na nasibu. Wamehama CHADEMA kujaribu bahati yao. They’ll learn it the hard way and quickly come to their senses. Soon watakuja kulialia humu!
 
Sawa.

Hata kama mtu kakubali kwenda kwenye mechi ya Simba na Yanga ambayo timu moja imemchagua refree, wewe hutakiwi kufanya fujo.

Unatakiwa ujenge hoja tu kwamba hii mechi si halali kwa sababu refree kachaguliwa na timu moja.

Watu waelewe, wasusie hiyo mechi.

Ukifanya fujo utakuwa huna tofauti na hao wanaopanga refree katika mechi.

Wote mtakuwa mnafanya vurugumechi tu.

Sasa utakuwa na uhalali gani wa kusema huyu anapanga refa katika mechi, mtoeni, niwekeni mimi ninayefanya fujo?

Kwa nini mnapinga CCM kuwa na udikteta wakati nyie pia mnataka kuweka udikteta kila mtu akubaliane nanyi kwenye kupinga uchaguzi?

Kwa nini hamtaki kukubali kuwa kuna watu wamependa kushiriki uchaguzi huu na haki zao za kikatiba zinatakiwa kuheshimiwa?
 
Shida ni moja kwenye hii debate—unajizima data! Hiyo hoja waijenge na kuiwasilisha kupitia jukwaa gani? Ndiyo kusema hujui kwamba CHADEMA wamezuiliwa kufanya shughuli za kisiasa?
 
Kuna wakati........
 
Shida ni moja kwenye hii debate—unajizima data! Hiyo hoja waijenge na kuiwasilisha kupitia jukwaa gani? Ndiyo kusema hujui kwamba CHADEMA wamezuiliwa kufanya shughuli za kisiasa?
Wewe hata hueleweki unazungumzia CHADEMA au unazungumzia wananchi kupinga CCM.

CHADEMA kama kweli ni chama cha wananchi kinazuiliwaje kufanya shughuli za kisiasa?

Hiyo ni excuse ya chama kilichoshindwa ku mobilize watu.

Hiyo ni failure ya CHADEMA. Nakwambia CHADEMA imeshindwa hata kuanzisha campaign ya ku boycott CRDB, benki ya ovyo kabisa iliyowapotezea watu access ya pesa zao, achilia mbali ku boycott uchaguzi.

Huelewi wapi?
 
Kuna madokta wengine ni wapumbavu tu kama huyo dokta wa hapa na pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…