TANZIA Dkt. Masumbuko Lamwai afariki dunia

TANZIA Dkt. Masumbuko Lamwai afariki dunia

Mwanasheria nguli, Msomi Kindakindaki aliyeichachafya CCM Hadi ikatia NIDHAMU.
Rest in eternal peace
Ni kweli ila aliharibu kuingia siasa .Alikuwa Ni meanasheria mahiri ambaye alikuwa na wateja wenginkuliko wakili yeyote Tanzania kabla ya kujiunga na siasa .Kuingia ofisii yake tu ulikuwa unalipia pesa siio kidogo. Sio za kumuona Bali za kueleza shida yako mapokezi ili ishugulikiwe

Umati uliokuwa ofisini nje utafikiri mkutano wa hadhara wote wakisubiri Kuingia ofisini kwake wampelekee pesa alipojiunga na siasa ndio ikawa kifo Cha uwakili wake

Nadhani iko haja kujifunza kuwa Mara ingine ni viziri kubakia eneo lako lenye nyota inakowaka Sana
Amefariki akiwa kapoteza vyote umaarufu wa uwakili na umaarufu wa kisiasa

Siasa ziliua vyote
 
Timu ya NCCR ilikuwa kiboko baadae ikahujumiwa tukawapoteza tuliowaamini. Upinzani na WATU wenye mioyo ya kuamini haki na utengamano ktk jamii.

Tuka fubaa ndiyo maana mpk sasa hivi NCCR haina maana tena. Ni chama kilicho jaa wanasiasa wanafiki na waongo RIP Dr. Ila ushujaa wako uliishia kuwavunja moyo wapenda haki. Lala Kwa amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ezekieli 18:20 Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu pema peponi. Amina
 
Pole sana Roman kwa kupotelewa na mzee...

Mungu awape faraja
 
Death bed ya wanasiasa wengi wa upinzani ni ccm. Huyu bwana sawa na wengine wote wanaotoka upinzani na kuhamia ccm wanapofika huko ndio inakuwa mwisho wao kisiasa.

Huyu bwana alipokuwa upinzani alikuwa ni moto wa kuotea mbali sawa tu na alivyo Lissu leo hii lkn nyota yake ilizimika tu pale alipohamia ccm kiasi kuwa wengine tulifikiri aliishakufa kitambo, kumbe alikuwa bado angali hai..!!

Anyway, ccm ndio kaburi la wanasiasa wa upinzani na bado wakienda huko watazidi kufa tu kisiasa. RIP, hata hivyo.
 
Nakumbuka Mzee wetu Mkapa aliwahi mlaumu baada ya wabunge wengi wa CCM kushindwa kwenye kesi za uchaguzi ambapo Masumbuko alikuwa wakili upande wa upinzani.

Mkapa alisema" ukiona mtu ambaye kazi yake ni kuwavua wenzake ubunge hafai" akimaanisha Masumbuko Lamwai. Nakumbuka asilimia 99% ya kesi zoote alizosimamia Lamwai alishinda. R.I.P JEMBE
 
Selasini pole sana lakini jifunze utu. We siyo was kumkashifu Mbowe kwa ahadi ya kupewa vijisenti na ccm, sasa toka bungeni nenda msibani ukitafakali matendo ya.
 
Back
Top Bottom