Dkt. Mollel: CHADEMA walipanga njama za kumpiga risasi Lissu

Yaani watolewa walinzi wote halafu wauaji wahakikishiwe kinga na aliyewatuma then wawe labda askari cha ajabu watumie 30+ bullets kwa umbali mdogo hivyo et mtu aishie kupigwa miguu!!! Hakuna miujiza ya hivyo au unadhani yule mhuni wa New Zealand aloowaua mosque hawamjui Mungu?
 
Ujinga huu wa Mollel aliutoa Feb 2019 mbele ya Bunge, ni jambo la ajabu kuwa hadi Leo hii June 23 bado hajaitwa popote kutakiwa asaidie maelezo yatakayo ifikisha Chadema au viongozi wake kortini.
Maana halisi Mbunge Mollel amepuuzwa kuwa ni mjinga au mpumbavu.
Hii inaleta maana kuwa hawa watu walionunuliwa ni wajinga kiasi kwamba hata huko CCM wanapaswa kukaa nao kwa machale kwani wana unafiki kuzidi wa shetani mwenyewe
 
When was the case opened?!
 
Badala ya kujibu hoja wewe unajikita kurusha vijembe?
 
Napenda kuwashauri wana JF kuacha tabia ya kuwasingizia watu maneno magumu haiwezekani mtu kama mollel atamke maneno kama hayo tunajua ni msomi na ni mtunga sheria wa nchi lakini kama ni yeye kweli na aliosema alidhamiria ninaamini sasa atakuwa amelisaidia jeshi letu pendwa namna ya kuanza uchunguzi wao maana waliotenda mollel anawajua na atakuwa tayari kuweka kila kitu wazi huko polisi lakini akiweka wazi hadharani atakuwa anawasaidi wauaji namna ya kujipanga kujibu na ninaamini tena kwa maelezo haya polisi.

Wataanza haraka sana lakini tukiona jeshi letu limepuuza na haliwahoji waliotajwa na wala mollel hajaitwa kutoa ushirikiano tunaweza amini mollel kafilisika ubongo na itakuwa ni ishara tosha ya kuonyesha hana uwezo wa kuongoza na itakuwa ni aibu kwa waliomchagua mimi ninavyowajua polisi huwa hawadharau tuhuma kama huamini sema kwa fulani kuna dawa za kulevya uone muziki wake.
 
kwani kigogo2014 na yule mwenzake Ex-Spy wanasemaje kuhusu shambulio la T.L ?
 
Mtoa mada, subiri Tundu Lissu arudi pamoja na dereva wake ili watowe ushirikiano kwa vyombo vya dola, kisha ndipo utajua kwamba, mpango wa kushambuliwa Tundu Lissu ulipangwa ndani ya chadema au hapana.

Aidha katika ushirikiano huo pia utajua kwa nini Tundu Lissu alipigwa risasi mguu wa kulia alikokuwa dereva wake na si mguu wa kushoto ilikodaiwa washambuliaji walikuwa. Pia utajua kwa nini Dereva wa Tundu Lissu alishuka kwenye gari na kwenda kujificha ndipo boss wake akashambuliwa.

Na kama washambuliaji walitoka nje ya chadema, kwa nini walisubiri dereva ashuke? Je, washambuliaji hao walikuwa na makubaliano yoyote ya kutomdhuru dereva isipokuwa Tundu Lissu pekee?

Na mwisho utajua, kwa nini risasi zilizodaiwa kumpiga Tundu Lissu zilitoka 54 tulizoelezwa awali, na sasa tunaambiwa ni 19 tu? Sambamba na yote hayo utajua kwa nini mara baada ya shambulio, chadema haikutaka kumtoa dereva kusaidia vyombo vya uchunguzi kwa kisingizio cha kuathirika kisaikolojia. Je, saikolojia inatibiwa Kenya na baada ya Kenya alipewa rufaa ya kutibiwa Ubelgiji?

Akili za kuambiwa, changanya na za kwako.
 
Njaa ni mbaya sana aisee!! Bora nife rofa kuliko kutumika kwa aibu namna hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…