Dkt. Mollel: Utafiti unaonesha Wagonjwa wengi wa Ocean Road wanatokea Kanda ya Kaskazini si Kanda ya Ziwa

Dkt. Mollel: Utafiti unaonesha Wagonjwa wengi wa Ocean Road wanatokea Kanda ya Kaskazini si Kanda ya Ziwa

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge Joseph Michael Mkundi Bungeni leo Aprili 14, 2025 aliyehoji “Takwimu zinaonesha Wagonjwa wengi wa Saratani waliopo katika Taasisi ya Ocean Road wanatokea Kanda ya Ziwa, kwa nini Serikali isiboreshe Hospitali ya Rufaa ya Bugando Kitengo cha Saratani ili kusaidia uwepo mgawanyiko wa taasisi hizo kuhusumia watu?”

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema utafiti unaonesha Wagonjwa wengi waliopo kwenye Taasisi ya Ocean Road wanatokea Kanda ya Kaskazini na sio Kanda ya Ziwa kama ambavyo imekuwa ikiaminika hivyo.

Pia soma:
~
Serikali imekamilisha ujenzi wa jengo la tiba mionzi ya Saratani KCMC kwa bilioni 5
~ Kuchelewa kugundua Saratani huchangia vifo kwa asilimia kubwa
~ Saratani inaua watu elfu 26 kila mwaka nchini
~ MJADALA: Umuhimu wa Chanzo Dhidi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa Wasichana (Miaka 9-14)
 

Attachments

  • 2025-04-14 10-33-57.mp4
    16.5 MB
Nafikiri ni gia ya kupeleka pesa mikoa ya nyumbani kama ilivyofanyika kwa chuo cha Nelson Mandela. Madaktari ambao wamekuwa wakitoa taarifa ya kuwa wengi wa wagonjwa wa saratani wanatokea kanda ya ziwa ina maana wamedanganya taifa kwa miaka yote hiyo?
 
Back
Top Bottom