Dkt Mpango: Kuna manung’uniko mengi ya Wananchi kuhusu mifumo yetu ya haki jinai

Dkt Mpango: Kuna manung’uniko mengi ya Wananchi kuhusu mifumo yetu ya haki jinai

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango amesema manung’uniko hayo ya Wananchi yanaonesha changamoto nyingi zilizopo kuanzia ukamataji wa wahusika kujua hata haki zao pamoja na ucheleweshaji wa upelelezi.

Amesema “Nitoe mfano kuna kijana alikamatwa mwezi mmoja na nusu uliopita #Mwanza, wazazi wake wakamtafuta sana hawakumpata hata walipoomba msaada Polisi ikawa kimya, wakanitafuta, nikawasiliana na Polisi Mwanza, wiki iliyopita baba mzazi wa kijana akasema wamempata kijana wao licha ya kuwa walishatangaza msiba.”
 
Hata Sabaya yuko gerezani kwa uhuni tu wa baadhi ya viongozi lakinj mahakama ilishamwachia huru.
 
Sasa kama ametambua uozo na upumbavu kama huo amechukua hatua gani kukomesha ili usijirudie tena,
 
walipoomba msaada Polisi ikawa kimya, wakanitafuta, nikawasiliana na Polisi Mwanza, wiki iliyopita baba mzazi wa kijana akasema wamempata kijana wao licha ya kuwa walishatangaza msiba.”
Wangapi wana nafasi hiyo ya kukupata? Wengi wanapotea kwa kweli. Hapa jirani yangu muuza matunda leo ni miezi kumi hajulikani alipo Kama ni Kweli unasaidia hivyo njoo hapa mskiti wa madina dar, huyu kijana amepotezwa kimya kimyaaaaa. Familia yake inateseka sana
 
Back
Top Bottom