Dkt. Mtahabwa: Wazazi na Watoto wao wawe pamoja na kushirikiana, la sivyo mzazi anajiandalia bomu

Dkt. Mtahabwa: Wazazi na Watoto wao wawe pamoja na kushirikiana, la sivyo mzazi anajiandalia bomu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema anaiona Tanzania ya neema ya watu wanaojitambua na wanaoshirikiana kupitia Montessori.

Kamishna wa Elimu.JPG

Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa

Ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Kongamano la 26 la Wana-Montessori Community of Tanzania lililofanyika Dar es Salaam.
Amesema baada ya kusikiliza na kuoneshwa namna Montessori inavyofanya kazi kuwaendeleza Watoto.

“Nimejiuliza, mbona hamjapiga jaramba kujitangaza zaidi kwenye runinga, redio na maeneo mengine ili watu wawajue?

“Ongeeni hata kwenye makanisa, misikiti ili Watoto waheshimiwe, naomba MTC muwe watu ambao mtaleta nuru kwenye Elimu ya Tanzania, tunapenda Wazazi na Watoto wao wawe pamoja na kushirikiana, na ‘Kumisiana’, la sivyo mzazi anajiandalia bomu,” amesema Dkt. Mtahabwa.

Amesema “Ni jukumu la Montessori Community of Tanzania kuwaelimisha Wazazi juu ya umuhimu wa "ku-Connect" na Watoto wao, ongeza uwekezaji ngazi ya awali.

Mtahabwa.JPG
“Naomba tuwe na MoU (Mfumo wa Makubaliano) tubainishe maeneo ya ushirikiano kati yetu, Wizara ya Elimu na Montessori Community of Tanzania (MCT)."

Sarah Kiteleja: Tunahitaji kujenga jamii yenye ubunifu, uadilifu katika kujenga nchi yetu
Upande wa Mkurugenzi wa Montessori Community of Tanzania (MCT), Sarah Kiteleja amesema mazingira ya taasisi hiyo, yanamwandaa mtoto tangu anapozaliwa hadi umri wa miaka 6 akisisitiza kuwa Wanalindwa na kupata elimu bora.

Ameeleza kuwa mbinu ya Shirika lake katika ufundishaji inazingatia uwezo asilia wa mtoto.

Sarah Kiteleja.JPG

Sarah Kiteleja
Amenukuliwa akisema “Bado tunahitaji kujenga jamii yenye ubunifu, uadilifu katika kujenga nchi yetu, hivyo mchakato huu huanza kumjenga Mtoto akianza mdogo. Mbinu hizi ni katika lugha, hisabati n.k.

“Shirika limefanikiwa kuwa na vyuo 8 vya kuwandaa Walimu katika mbinu hii ya ufundishaji ikiwemo: Mwanza, Mtwara, Lushoto, Moshi, Bagamoyo na Msimbazi.

Sarah.JPG
“Tuna vituo zaidi ya 2000, shule za msingi 45 zinazotumia mbinu ya Montessori ya ufundishaji, pia mbinu hii inawalenga hata Watoto wenye mahitaji maalum.”

Amesisitiza kuna changamoto kwa wakaguzi wa elimu kutofahamu mbinu ya Montessori, hivyo kumekuwa na migogoro kati ya Walimu na Wakaguzi wanaoufuata mbinu hii ya Montessori.

Wazazi pia wanaona Watoto wao wanakwenda tu kucheza hasa katika shule wanazotumia mbinu ya Montessori, lakini mbinu hii inawasaidia Watoto kuwa wabunifu na kutua changamoto zinazowazunguka."
 
Back
Top Bottom