Dkt. Musukuma: Hereni kwa ng'ombe zina faida gani?

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Your browser is not able to display this video.
Mbunge wa Jimbo la Geita Joseph Kasheku Musukuma amehoji Bungeni faida ya kuweka hereni kwenye ng’ombe na amemtaka Waziri wa Mifugo na Uvuvi kujinasua kwenye mtego huo.

Musukuma amesema hayo wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyoomba kiasi cha Shilingi 295,920,933,000. kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

“Mimi sipingani na maagizo ya Waziri mkuu tunaboresha hivi ng’ombe zikigombana kule poroni hereni ikadondoka mtaniambia anayepigana nae ni nani?, ng’ombe zangu zikiiibiwa zikapelekwa Mtwara mtanipigia Musukuma usiende Polisi fuata ziko Mtwara?, Waziri usiingie kwenye huu mtego sijui unanisikiliza au unachati?”
 
Heleni?

Ni uchafu na plastic inayolipwa na mfugaji kwa Maelfu ya shilingi
 
Huu mradi unashikiwa kidedea sana ni mradi wa kigogo gani ? Kwa sababu kuna namna unasukumwa mazingira tatanishi !!
 
Huu mradi unashikiwa kidedea sana ni mradi wa kigogo gani ? Kwa sababu kuna namna unasukumwa mazingira tatanishi !!
Unaandika ukidhani kila mtu anajua unachowaza? Unatakiwa uelezee ''heleni za ng'ombe'' ni nini na umesikia kutoka wapi
 
Mbunge wa Jimbo la Geita Joseph Kasheku Musukuma amehoji Bungeni faida ya kuweka hereni kwenye ng’ombe na amemtaka Waziri wa Mifugo na Uvuvi kujinasua kwenye mtego huo...
Elimu ni kitu cha thamani sana!

Hata kama ni Hoja basi ijengwe kwa uzito

Suala hapa siyo Hereni

Suala ni Utambuzi wa Mifugo.

Hereni ni Device bora kati ya Njia nyingi ikiwapo hiyo ya ya kizamani ya kuchoma ngozi kwa chuma cha Moto.

Lakini Ukisikia Mbunge anapinga Utambuzi basi nyuma yake kuna WAHAKUFU WA MIFUGO WASIOTAKA KAZI YAO IFE.

Wezi wa Mifugo wanapinga hili Zoezi kwa Nguvu zote!

Wanajua ikitokea limefanikiwa biashara yao imekufa!

Hilo ndo kubwa wala hakuna issue yoyote na watu hao ni wachache sana ila wana Nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…