Unahoji hata juu la hilo? Kanda ya Ziwa, wengi hawajui Kiswahili sanifu, na wengine hawafahamu kabisa Kiswahili. Ni kanda ambayo wengi wao muda mwingi huongea lugha zao za makabila, na hivyo kuwa na weledi mdogo kwenye Lugha ya Kiswahili. Tatizo hilo lipo kwa ndugu zangu wasukuma, na hata wahaya. Makabila yote ambayo muda mwingi wanaongea lugha za makabila yao, huwa wana tatizo katika kufahamu vizuri lugha ya Kiswahili. Usukumani mpaka leo, ndiyo sehemu pekee ambayo unaweza kwenda vijijini ukawakuta watu ambao hawajui kabisa lugha ya Kiswahili, yaani hata kile tunachokiita Kiswahili kibovu, hakuna. Huko ndiko nilishuhudia wakati wa mkutano na wananchi akatakiwa kupatikana mkalimani anayekifahamu Kisukuma na Kiswahili. Kwa sababu bila ya kufanya hivyo, wapo ambao hawatakuelewa unaongea nini. Na wao wakitaka kukuuliza, wanakuuliza kwa Kisukuma ambacho na wewe hufahamu.
Huko ndiko utaulizwa, 'ulikwendako? Utarudipo?'.
Kiswahili sanifu ni:
Ng'ombe hawa, siyo ng'ombe hizi.
Ng'ombe wangu, siyo ng'ombe zsngu.
Kuku wangu, siyo kuku zangu.
Mbuzi wale, siyo mbuzi zile.