Dkt. Mwigulu: Chanjo za Corona zimefanyiwa utafiti nchi za baridi zitawafaaje watu wa Dar es Salaam?

Dkt. Mwigulu: Chanjo za Corona zimefanyiwa utafiti nchi za baridi zitawafaaje watu wa Dar es Salaam?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360, Waziri Dkt. Mwigulu Nchemba amesema watanzania wanapaswa kujiuliza chanjo za watu wa nchi zenye baridi zinawezaje kuwasaidia watu wa Dar es Salaam kwenye joto.

Mwigulu amesema ndio maana watu waliotoroka wakaenda kuchanja kimya kimya zinawaletea matatizo.

Chanzo: Clouds 360

Maendeleo hayana vyama!
 
Shida kubwa ya nchi zetu ni pale wanasiasa wanapoamua kujifanya ni wataalam wa kila kitu na kuwapuuza wataalam, huku wataalam nao wakiamua kujitoa ufahamu kulinda ulaji wao.

Mambo mengine ni aibu kabisa kila mtu sasa anajifanya daktari ilimradi apate la kuongea kumuunga mkono JPM.
 
Haya mambo ya Corona yasimamiwe na wataalamu wa afya, siyo kila mtu awe msemaji wa Corona. Ni jambo la hovyo sana hata kumuona Bill Gate akizungumzia mambo ya gonjwa hili la Corona na chanjo yake.

Tuliambiwa katika siku za mwisho ni kutoweka kwa amana, na amana inaondoka pindi jambo linaposimamiwa na mtu asiyekuwa mbobezi wa jambo hilo hivyo tusubiri kiyama.
 
Aibu kwako Migulu Nchemba,PhD. Magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu hayakuwa magonjwa makubwa ya nchi maskini kama yetu.Yameanza kupamba moto baada ya style yetu ya maisha kubadilka.

Dawa za shinikizo la damu na kisukari mnazotumia zilifanyiwa utafiti wapi hapa Tanzania?
 
Huyu naye kadanganywa, huko penyewe chanjo haitoshi ndio maana wanaanza na watu muhimu kwanza tena wananchi wao.

Sasa watajuaje ubora wa chanjo bila jaribisha kwetu nchi za joto?
 
Hvi NIMRI wanafanya nn au nao wanajifukiza? Kwa nn maghufuli asiifute NIMR na kuwafukuza wote kazi ...mpak sa hv hawajaonyesha effort yyte ya wao nao kutafta chanjo ...wamekaa tu kusikiliza matamko ya Wana siasa
Wanayo chanjo ya matone inaitwa covidol unakunywa Kwa kutumia glass. Imethibitishwa na mkemia wa serikali.
 
Back
Top Bottom