Dkt. Mwigulu: Chanjo za Corona zimefanyiwa utafiti nchi za baridi zitawafaaje watu wa Dar es Salaam?

Dkt. Mwigulu: Chanjo za Corona zimefanyiwa utafiti nchi za baridi zitawafaaje watu wa Dar es Salaam?

"Mwigulu amesema ndio maana watu 'waliotoroka' wakaenda kuchanja kimya kimya zinawaletea matatizo"

Kwahiyo serikali inawaona wale walioenda kupata chanjo ni 'WALITOROKA'.????

Viongozi wamegeuka kama mashabiki wa mpira wa bongo pale timu yao inapokuwa imefungwa ,kila mtu anageuka kocha..

NCHI NGUMU HII...
 
Safi Sana
Serikali makini haijawahi tokea
Magufuli Ni chaguo la MUNGU
IMG_20210218_174254_207.jpg
 
Wanayo chanjo ya matone inaitwa covidol unakunywa Kwa kutumia glass. Imethibitishwa na mkemia wa serikali.
Kwa nini watu wasitangaziwe mbna ipo kimya kimya ...watangaze kwamba tuna chanjo yetu IPO poa wananchi tumieni
 
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360, Waziri Dkt. Mwigulu Nchemba amesema watanzania wanapaswa kujiuliza chanjo za watu wa nchi zenye baridi zinawezaje kuwasaidia watu wa Dar es Salaam kwenye joto.

Mwigulu amesema ndio maana watu waliotoroka wakaenda kuchanja kimya kimya zinawaletea matatizo.

Chanzo: Clouds 360

Maendeleo hayana vyama!
Hivi chanjo nyingine zimefanyiwa utafiti wapi kama si nchi za baridi? huu ujinga ujinga ni kwa ajili tu ya kumfurahisha mtu mmoja
 
Si wawaachie wataalamu wa tiba ndo WajadilI hilI suala kulingana na Ujuzi wao? Yani sasa hivi kwasababu mtu ni kiongozi basi anafahamu kila kitu, viongozi wetu wanajidhalilisha sana
 
Pale mwanasiasa anapojaribu kuingilia suala la kisayansi ili kulinda tu ugali wake.

Kwa hiyo Mwigulu anataka kutuaminisha ya kwamba yeye ana akili kuliko hao scientist?
Hana lolote.. ni mpuuzi mmoja tu ambaye amesema lakini hakuelimika.
 
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360, Waziri Dkt. Mwigulu Nchemba amesema watanzania wanapaswa kujiuliza chanjo za watu wa nchi zenye baridi zinawezaje kuwasaidia watu wa Dar es Salaam kwenye joto.
Na dawa zingine je
Ikija chanjo ya drum atasema hivyo?
 
Kwa nini watu wasitangaziwe mbna ipo kimya kimya ...watangaze kwamba tuna chanjo yetu IPO poa wananchi tumieni
Haha haaa....
Mkuu president alishaisemea hii. Ipo nimr watu wananunua machupa Kwa machupa.
Kuita chanjo nilikuwa natania tu, ni dawa ya maji mfano wa Ile ya Antananarivo sasa Kwa taasisi ya utafiti kama nimr badala ya kujihangaisha kutafuta chanjo yetu wenyewe wao Wana deal na tiba mbadala zaidi.
 
Anaongea kama mtoto mdogo alievaa pampasi ambae hajui la kufanya!Kwa hiyo kwa akili yake anafikiri kuwa wanasayansi wanaweza kutengeneza chanjo ambayo haifanyi kazi katika mazingira ya joto halafu wakurupuke na kusema kuwa hiyo chanjo ipelekwe Afrika?Hiyo ndiyo maana ya sayansi?

Yeye kikubwa alipaswa aongelee suala la tatizo la COVID-19 virus variants ambalo ki ukweli linaweza kuwa na uhusiano na hali za hewa ambalo tayari wanasayansi wa chanjo wanalijua vizuri sana na wanajua namna ya kupambana nalo.He is a creepy asshole fool ambae anaongea kama mtoto mdogo mwenye elimu ya chekechea.Halafu hawa ndiyo viongozi tunaotegemea watuvushe?Mimi huwa najiuliza sana,how possible Taifa lenye watu zaidi ya million hamsini tunaishia kupata viongozi vichaa kila kona kuanzia pale top?!
 
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360, Waziri Dkt. Mwigulu Nchemba amesema watanzania wanapaswa kujiuliza chanjo za watu wa nchi zenye baridi zinawezaje kuwasaidia watu wa Dar es Salaam kwenye joto.

Mwigulu amesema ndio maana watu waliotoroka wakaenda kuchanja kimya kimya zinawaletea matatizo.

Chanzo: Clouds 360

Maendeleo hayana vyama!

Hawa watu wanajiaibisha bure tu.
Can't they keep quite twende walivyoamua?
Atuambie chanjo iliyofanyika kwa nchi joto?
Anajua mnyororo wa mkondo baridi tangu chanjo inapozalishwa mpaka kumfikia mchanjwaji?
Hizi siyo siasa ni sayansi jamani?
Hata kama ingekuwa anavyowaza ni sawa basi wachukulie wa Lushoto, Makete, Mfundi, Kagera, Arusha na Kilimanjaro etc.
Unajibebesha zigo la misumari bure.
 
Si wawaachie wataalamu wa tiba ndo WajadilI hilI suala kulingana na Ujuzi wao? Yani sasa hivi kwasababu mtu ni kiongozi basi anafahamu kila kitu, viongozi wetu wanajidhalilisha sana
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
 
Back
Top Bottom