Dkt. Mwigulu: Deni la Taifa limeongezeka hadi Tsh. Trilioni 79.19, bado ni himilivu

Dkt. Mwigulu: Deni la Taifa limeongezeka hadi Tsh. Trilioni 79.19, bado ni himilivu

Aisee tuacheni utani hili ongezeko ni kubwa sana washkaji. Yaani fikiria katika kipindi tu cha mwaka mmoja ongezeko limekuwa 13% sasa hapo bado hatujui mpaka tun@fikia uchaguzi mkuu 2025 watakuwa wamekopa tena kiasi gani?

Ni ukweli kwamba huyu mama ni mkopaji mno kushinda marais wote tuliowahi kuwa nao na badly enough ni kwamba hana management nzuri ya hata fedha anazokopa. Ni muda sasa ajitafakari apunguze huu ukopaji holela kwani ni risk sana miaka michache ijayo tutagota kwenye eave na hapo ndipo tutakapoelewana vizuri.

Kwanini hajifunzi hata kwa mtangulizi wake ambaye alikopa kiasi kama hicho peke yake katika miaka yote mitano aliyokuwepo madarakani?. Tunakosa kabisa sera za kujitegemea kutwa tunategemea misaada na mikopo poor think-tank of these leaders
 
haa
 
Attachments

  • 20230615_140710.jpg
    20230615_140710.jpg
    107.2 KB · Views: 3
  • 20230615_140710.jpg
    20230615_140710.jpg
    107.2 KB · Views: 3
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Bungeni Dodoma amewasilisha Bungeni taarifa ya Hali ya Uchumi wa Kitaifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2023/2024 ambapo moja ya mambo aliyoyasema ni kwamba hadi kufikia mwezi Aprili 2023, deni la Serikali lilikuwa shilingi bilioni 79,100.19 sawa na ongezeko la 13.9% ikilinganishwa na Shilingi bilioni 69,440.01 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022.

“Kati ya kiasi hicho, deni la nje ni shilingi bilioni 51,162.60 na deni la ndani ni Shilingi bilioni 27,937.59, ongezeko la deni limetokana na kupokewa kwa fedha za mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme, elimu na afya, aidha tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikali iliyofanyika Desemba, 2022 imeonesha kuwa deni ni himilivu na viashiria vya deni viko ndani ya wigo unaokubalika kimataifa katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu”

“Machi 2023, kampuni za Fitch Ratings na Moody’s Investors Service zilianza zoezi la kuifanyia Nchi tathmini ya kukopesheka katika masoko ya fedha ya kimataifa, zoezi hilo lilikamilika ambapo kampuni ya Moody’s Investors Service ilichapisha matokeo ya tathmini hiyo Mei 2023 na kampuni ya Fitch Ratings mwezi Juni 2023, kwa mujibu wa matokeo hayo, Tanzania imewekwa katika daraja la B2 POSITIVE na Kampuni ya Moody’s Investors Service na daraja la B POSITIVE na Kampuni ya Fitch Ratings ambayo yanaashiria taswira chanya kwa Nchi kimataifa”

“Pamoja na mambo mengine, matokeo hayo yamechangiwa na mwenendo mzuri wa ukuaji wa uchumi, usimamizi makini wa deni la Taifa, kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa sekta binafsi, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa pamoja na kuleta maridhiano ya kisiasa ndani ya Nchi, kukamilika kwa zoezi hilo, kutaiwezesha Nchi kutambulika katika masoko ya fedha ya kimataifa na hivyo, kuongeza wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa Serikali na sekta binafsi”

Nakaribisha maoni!!!
 
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Bungeni Dododma amewasilisha Bungeni taarifa ya Hali ya Uchumi wa Kitaifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2023/2024 ambapo moja ya mambo aliyoyasema ni kwamba hadi kufikia mwezi Aprili 2023, deni la Serikali lilikuwa shilingi bilioni 79,100.19 sawa na ongezeko la 13.9% ikilinganishwa na Shilingi bilioni 69,440.01 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022.

“Kati ya kiasi hicho, deni la nje ni shilingi bilioni 51,162.60 na deni la ndani ni Shilingi bilioni 27,937.59, ongezeko la deni limetokana na kupokewa kwa fedha za mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme, elimu na afya, aidha tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikali iliyofanyika Desemba, 2022 imeonesha kuwa deni ni himilivu na viashiria vya deni viko ndani ya wigo unaokubalika kimataifa katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu”

“Machi 2023, kampuni za Fitch Ratings na Moody’s Investors Service zilianza zoezi la kuifanyia Nchi tathmini ya kukopesheka katika masoko ya fedha ya kimataifa, zoezi hilo lilikamilika ambapo kampuni ya Moody’s Investors Service ilichapisha matokeo ya tathmini hiyo Mei 2023 na kampuni ya Fitch Ratings mwezi Juni 2023, kwa mujibu wa matokeo hayo, Tanzania imewekwa katika daraja la B2 POSITIVE na Kampuni ya Moody’s Investors Service na daraja la B POSITIVE na Kampuni ya Fitch Ratings ambayo yanaashiria taswira chanya kwa Nchi kimataifa”

“Pamoja na mambo mengine, matokeo hayo yamechangiwa na mwenendo mzuri wa ukuaji wa uchumi, usimamizi makini wa deni la Taifa, kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa sekta binafsi, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa pamoja na kuleta maridhiano ya kisiasa ndani ya Nchi, kukamilika kwa zoezi hilo, kutaiwezesha Nchi kutambulika katika masoko ya fedha ya kimataifa na hivyo, kuongeza wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa Serikali na sekta binafsi”
Hawa jamaa sijui wanapata faida gani kwa kusem uongo.
Screenshot_20230615-151022.png
 
Kwahiyo katika bajeti yote wewe umeona sehemu ya deni tu, kwani hata Marekani Si wanakopa, au wewe mwenyewe una madeni kiasi gani, nyinyi watu mbona wajinga? Mmekiwa negative sana.
 
Kila kukicha tunaelezwa kuwa Rais anatitirisha matrilioni ya fedha hapa nchini. Hizo fedha zinazotiririshwa ni za misaada? Ninapenda tujue mpaka sasa deni la Taifa limefikia kiasi gani.

Je, tangu Rais wa Awamu ya Sita aingie madarakani mpaka sasa amekopa kiasi gani? Je, hizo hela zilizokopwa zimefanya kazi gani? Mbona miradi mikubwa kama SGR haisogei?

Daraja la Busisi kasi yake ni kidogo sana? Pia tujue safari ya kwenda India imegharimu kiasi gani ili tulinganishe na ujenzi wa madarasa, Vituo vya Afya n.k.
 
Back
Top Bottom